Nunua gari Ndugu yangu. Aibu ndogo ndogo zinaepukika

Wewe nawe unatoka nje ya mada, muda wote unawaza mabalaa..!! Veggies sijui mkoje?
na kwasabb hiyo si unaona hata waliopata magari kwa njia za uchafu na kutweza utu wao wakipata mizinga barabarani inakua ni songombingo kweli hatoki mtu wa moto ni baridi tu.

Ni muhimu kutumia maarifa, bidii na nguvu zetu wenyewe kupata vitu vya ndoto zetu ikiwa ni pamoja na usafiri binafsi 🐒
 
Wewe mbona umepata kwa wizi wa kuiba kodi za wananchi? Umeanza kujifanya mtakatifu..!!
 
Mkuu boda ni chanzo kikuu cha umauti hapa mjini, drivers wa magari wanadharau watu wa pkpk na wanawaona wakorofi..so muda wowote wanakupelekea gari unaelekea akhera na kuacha familia ikiteseka.
Ndio maana ya kuandika hapo chini haya yote tumeyafanya na kuyaishi

Hata gari pia ni hivyo hivyo sauala la usalama ni Mungu ndio ana_tuepusha na mabaya yote.
 
Nakumbuka mwaka 1999 kuelekea 2000 wazazi wangu wote waliwili wakiwa wafanyakazi wa shirika moja la serikali libinafishwa kwenda kwa muwekezaji.

Walipewa Nyumba Bure,Umeme bure,Usafiri uliwafuata na kuwarudisha nyumbani.

Asilimia kubwa ya wafanyakazi wa lile shirika hawakujenga nyumba zao za kuishi,hata viwanja hawakuhusika navyo,wengi walinunua pikipiki na magari.

Alikuja muwekezaji na kupunguza wafanya kazi wengi.
Nakumbuka mama yangu alipunguzwa pia ,ila tulibaki kwenye nyumba ya kampuni kwa mgongo wa baba ambae alibakibaki kazini.

Mtaani kwenye kota zile ilikua aibu,watu hawana pa kwenda,na walipewa mafao yao.

Hawakua na kiwanja wala kibanda cha kujisitiri,kodi nje ya mji zilipanda maradufu.

Tulikua na pagala letu tumepaua na kuweka madirisha ya nondo, kuna rafiki yake baba aliomba kwenda kujishikiza hapo na familia yake.

Nilipata funzo kubwa sana la maisha.

Nilipopata ajira Dar, baada ya mwaka nikamwambia baba nimenunua kiwanja naomba uje ukione.

Mama alilia sana,akaniambia umekumbuka yaliyotukuta 2000 nikamwambia mama ndio mama.

Binafsi nilikataa kununua gari kupaki kituo cha mafuta

Nyumba husitiri ndugu zangu.

Legacy.
 
Kiukweli mi sijawa na gari japo uwezo wa kuwa nalo nnao hata leo,,kinachonishangaza ikifika tarehe 15-22 napigiwa sana simu za kukopwa hela na hao wenye magari mpaka najiuliza sasa huyu hiyo e.g 30m aliyonunulia gari si angeizungusha ili kuepukana na kuwa omba omba😅😅😅😇
 
Wew utafute pesa sana aissee,
HAkuna umri wa kununua gari,
Kama utapata una 50 sawa,
Ukipata na 30 vema
 
Hiv zile bei gani?
 
Wew utafute pesa sana aissee,
HAkuna umri wa kununua gari,
Kama utapata una 50 sawa,
Ukipata na 30 vema
Nimezungumzia vijana tuliotoka kwenye familia za watoto wa mama ntilie na sasa tupo middle upper class, nyinyi wenzetu mliovuka hapo hakuna tatizo.

BTW pesa ya kununua gari hata muda huu nikitaka ninayo ila nikisha nunua then what (hapa najizungumzia mimi) ?? Niwe naenda nalo kazini na kurudi nalo nyumbani?? Nipate heshima??!! Mimi bado sina sababu ya msingi ya kuwa na gari langu binafsi kwa sasa. Nikihiaji usafiri private nina uwezo wa ku afford uber pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…