Nyambizi iliyopotea mpaka kesho saa 9 alasiri itaishiwa oxygen

Nyambizi iliyopotea mpaka kesho saa 9 alasiri itaishiwa oxygen

..
Interactive_Titan_submersive_June21_3-01-1687359688.jpg
 
Jamaa walijilaani Kwa kusema meli yao ni zaidi ya Mungu alivyoviumba vyote kuwa haiwezi zuiliwa na chochote kwenye bahari yaani kina cha Bahari si chochote Kwa meli hiyo

Pengine wakiokolewa hao waliopotea watasema chochote juu ya hasira ya Mungu
Meli ya Titanic haikuzama kwa sababu za hasira ya Mwenyezi MUNGU, ile ilikua ni inside job, iliyofanywa kwa lengo maalumu.
 
Na teknolojia zote zilizopo duniani bado matokeo ni hafifu tu ?, Kile kisa cha nyambizi ya Russia iliyopotea kinaelekea kulingana na hichi.

...bado 'field' ya teknolojia ya majini inahitaji ugunduzi mpya zaidi na akili kubwa.

T14 Armata
Uwezekano wa hao watu watano kutoka siuoni hata kwa kujilazimisha. At such depth, bahari ina joto la juu kidogo kuliko la binadamu, unaweza zirai ukizidiwa ila sio kufa ni kama 34 °C. Tatizo ni pressure kubwa hapo chini, zaidi ya tani 2.6 kwa square inch moja. Na matatizo yanaanza kukiwa na leakage nje hapo maji yanaingia kwa kasi kama leak ni ya katobo kadogo mfano wa msumari yale maji yakiingia yanaweza kukuchubua ngozi yakikutana na wewe. Kasi yake kubwa na ukizingatia kile ni chombo kidogo hakina compartments hivyo kinajaa mapema.

Na hewa iliyokuwa imebaki kabla ya tukio ilitajwa ni ya masaa 40, kifaa kinaweza beba hewa ya masaa 90. Maungio yake au dirisha dogo la kioo ndio yaweza kuwa chanzo cha matatizo. Kuna engineer alifukuzwa na kampuni ile ya OceanGate kwa kutaja udhaifu wa dirisha la kioo ambalo certification yake ni kuzama mita kadhaa kama nusu hivi ya walipo sasa, wao wanazidisha depth. Kuna mambo mengi hapo yanazungumzwa ni kama corporate greedy, safety halikuzingatiwa sana walikuwa wanawahi kupata faida kubwa hivyo hawakufanya development mpya kupata certification wasichelewe.

Kwenye hiyo Titan kuna gaming controllers wanatumia za Xbox kama sikosei, ila sio ajabu hata Marekani kwenye subs zao na zana nyingine wanatumia Xbox au PlayStation pads ili gamer mwanajeshi atumie kirahisi maana amezoea, chamsingi ni kuifanya iwe military grade.

Hiyo Kurks ya Warusi iliyozama 2001 kulikuwa na compartments alafu bahari ile sio deep sana, walifunga zilizojaa maji wakabaki moja wakakosa hewa wakafa baada ya siku tatu, ile nuclear sub iliundwa kwa uimara mkubwa sana ukizingatia torpedoes ndio ziliripuka ila haikuharibika yote. Russian Navy ilitaka kufa kisabuni, uwezo wa kuokoa haikuwa nao na modules zake za kuzama zilikuwa zinaisha battery kabla hazijafungua emergency door ya sub wakapuyanga mpaka mwisho wakati Waingereza waliwahi eneo la tukio na meli yao yenye uwezo, na Wamarekani walikuwa tiyari kusaidia ila Urusi ikaogopa itapata aibu kusaidiwa, na siri zake za submarine zinaweza vuja ikawatoa kafara crew ya watu kama 30 hivi. Kuna movie ya Kursk ninayo, ukitaka jaribu kutazama somehow it depicts the story.
 
Back
Top Bottom