NYARAKA: Katiba Inayopendekezwa Oktoba, 2014 (Tanzania's Proposed Constitution)

NYARAKA: Katiba Inayopendekezwa Oktoba, 2014 (Tanzania's Proposed Constitution)

asante umenionesha unakoshinda, kumbe ndiyo sababu!!!!! mimi sio wa kiwango chako, nenda kwa wenzako mnaoshirikiana nao, after all, siku yako imeingia, kapumzike

Huna jipya mwanaume wewe ya katiba inyopendekezwa yamekushinda umebaki na mipasho tu kapumzike mwenyewe huna kitu.
 
haya siku yako imeingia, nenda kampumzike, usitumie nguvu nyingi sana, kwa ajili ya Katiba pendekezwa ambayo tayari imepita

Tatizo lako hujielewi,unapiga kelele sana afu huna jipya na hueleweki watz wotewangekua na akili kama yako wangekua wwameshauzwa!
 
KATIBA INAYOPENDEKEZWA NI BORA KULIKO YA SASA, HONGERA MH. RAISI, HONGERA WATANZANIA.

Katika historia ya uandishi wa katiba mpya duniani hakuna nchi yeyote ambayo iliwahi kuandika katiba mpya ikakidhi matakwa ya wananchi wote na taifa kwa 100%. Katiba si msaafu wala si biblia kwamba haiwezi kufanyiwa maboresho. Leo hii jambo ambalo tumeliona lina tija na manufaa kwa taifa na tukaliingiza kwenye katiba, kesho tutaliona halina tija na tutakubaliana kuliondoa au kuliboresha. Vilevile jambo ambalo leo tumeliona halina tija na kutoliingiza ndani ya katiba kesho tutaona umuhimu wake na tutakubaliana kuliingiza ndani ya katiba yetu.

Katiba inayopendekezwa imetambua haki za makundi mbalimbali kama vile wakulima, wafugaji, wafanyakazi, wasanii, vijana, wanawake na wengine. Pia katiba inayopendekezwa imetambua haki bunifu, mgombea, binafsi, maboresho katika muungano wetu sambamba na kuweka mfumo bora wa kusimamia rasirimali za taifa na kudhibiti mianya ya matumizi mabovu ya rasirimali. Kundi pekee ambalo linadhani halijatendewa haki katika katiba hii ni kundi la wanasiasa wachache ambao kwao tafsiri ya katiba bora ni ile inayokidhi maslahi yao ya kisiasa. Hili ni jambo ambalo watanzania hawana budi kulikataa.

Jambo la msingi ambalo kila mtanzania anapaswa kukubali ni kwamba katiba inayopendekezwa ni bora kuliko ile ya sasa. Wakati ambapo baadhi ya watu wakiipinga na kudai kwamba haiwezi kulivusha taifa letu, wapo watanzania tena asilimia kubwa ambao wanaiona katiba inayopendekezwa kuwa ni chombo madhubuti ambacho kitachochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hatuwezi kuwa na mtazamo mmoja, na ikifika wakati watanzania wote tukawa na mawazo yanayofanana basi tujue kwamba tunapaswa kujitazama upya. Kutofautiana kimtazamo ni jambo la kawaida na
hiyo ndiyo afya ya demokrasia iache ichukue nafasi yake. Tupingane kwa hoja bila kuhatarisha amani ya taifa letu.

Hongera Mh. Raisi Dr. Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa uliyoifanya. Hili ni jambo la kihistoria ambalo halijawahi kutokea katika historia ya Taifa. Hii ni mara ya kwanza kwa Taifa letu kuandika katiba yake kwa kushirikisha wananchi wake. Yapo mataifa ambayo yaliwahi kuandika katiba zao kwa kutumia Bunge la katiba pekee, wapo waliogeuza Bunge la kawaida na kuwa Bunge la katiba. Kwa taifa letu, mchakato umekuwa wa kidemokrasia zaidi kiasi kwamba wapo wanazuoni, wanasiasa na mataifa mbalimbali ambao wameishangaa Tanzania kwa kuruhusu demokrasia kwa kiwango hiki. Kwa hakika Mh. Rais anastahili pongezi na daima watanzania tutakukumbuka na jina lako haliwezi kufutika katika fikra zao.

Ni wajibu wetu kuiunga mkono katiba inayopendekezwa kwa Kuwa ni kwa manufaa ya taifa hili ,kimsingi tunawajibika kuelimishana ili wakati wa kuwapigia kura ukifika tumalize hili jambo kwa kupiga kura zetu,zitakazowezesha upatikanaji wa katiba hii bora kwa maslahi ya taifa
 
Tatizo lako hujielewi,unapiga kelele sana afu huna jipya na hueleweki watz wotewangekua na akili kama yako wangekua wwameshauzwa!
You wanted us to hear from you, yes, we have heard, now you can go and collect your package at peace
 
Huna jipya mwanaume wewe ya katiba inyopendekezwa yamekushinda umebaki na mipasho tu kapumzike mwenyewe huna kitu.
You wanted us to hear from you, yes, we have heard, now you can go and collect your package at peace
 
You wanted us to hear from you, yes, we have heard, now you can go and collect your package at peace

Mimi najitahidi kusoma mchango wako hata sikuelewi, maana jambo tunalolijadili hapa ni Katiba inayopendekezwa haya mengine yanatoka wapi, ni bora wana JF tukajikita kwenye mada ya msingi kuliko kushambuliana.
 
Kwanza ningependa mnieleweshe rasimu imesema rais wa znz ndo atakua makamo wa kwnza wa rais wa muungano je kama rais wa muungano katokea znz na huyu makamo wa rais nae atatokea serikali ya znz au ni njama za ccm tu kufanya mzanibari asiwe rais wa muungano ?

Njama unazo mwenyewe na wala usidanganye hapa nenda kasome vizuri kuanzia Ibara ya 99 mpaka 109 utaona nafasi uliyoitaja jinsi ilivyowekwa vizuri sana kwenye katiba Inayopendekezwa, kwa kukusaidia ni Ukurasa wa 86-92 Kwenye Katiba Inayopendekezwa.
 
You wanted us to hear from you, yes, we have heard, now you can go and collect your package at peace

Wewe ni Yuda Eskarioti kichwa yako inawaza vipande 30 nyie ndio mkipewa nchi mnatuuza wote,huna lolote zaidi ya kuwaza hela Katiba Inayopendekezwa hujaisoma unajifanya kuja na vihoja dhaifu na unaonekana sio mwaminifu hata kazini kwako, familia, kwa ndugu na jamaa the way unavyowaza hela mchumiatumbo wewe utakuja kuuzwa jiangalie!
 
Tatizo la wezi kila wanayekutananaye wanadhani ni mwizi kama wao, Leo hii ww unatetea katiba ipitishwe ile inayolinda wezi katika nchi, bila shaka ww utakuwa ni mojawapo wa mafisadi wanaoifisadi nchi hii, sio bure umetumwa ww kuhujumu TAIFA LETU ZURI. Leo iwe mwisho wako kuniquote hapa JF, unaonesha wazi ww ni mwizi wa raslim ali za umma, sio bure
 
Mimi najitahidi kusoma mchango wako hata sikuelewi, maana jambo tunalolijadili hapa ni Katiba inayopendekezwa haya mengine yanatoka wapi, ni bora wana JF tukajikita kwenye mada ya msingi kuliko kushambuliana.
Huwezi kuelewa kwa sababu umeamua kuiweka akili yako nzuri pembeni ili kutetea katiba pendekezwa maana kwako ni mradi, ila kwetu sisi katiba mpya na bora ni msingi kwa vizazi vyetu vijavyo. Aliwahi sema Jenerali ulimwengu kuwa kuna watu wanaakili ila kuna kipindi huweka akili yao pembeni ili kutetea nakulinda maslahi yao, sasa ww jiulize uko kundi gani.

Read all my posts about KATIBA, you will clearly understand my message, swali utaweza?
 
Tatizo la wezi kila wanayekutananaye wanadhani ni mwizi kama wao, Leo hii ww unatetea katiba ipitishwe ile inayolinda wezi katika nchi, bila shaka ww utakuwa ni mojawapo wa mafisadi wanaoifisadi nchi hii, sio bure umetumwa ww kuhujumu TAIFA LETU ZURI. Leo iwe mwisho wako kuniquote hapa JF, unaonesha wazi ww ni mwizi wa raslim ali za umma, sio bure

Mada uanzishe mwenyewe afu unajifanya kuruka tulia wewe si unajifanya unajua kuchonga, leo ndio unajifanya kujua UNA TAIFA LAKO ZURI TANZANIA ha ha ha ha ha ha usiwe kama Zombie, kugeugeu, wewe si unajifanya kupinga kila kinachopita mbele yako??? eeee? au sio wewe???? kweli siku hazigandi naona umeshaongozwa Sala ya Toba wewe karibu kwenye kundi la watu wema wenye matumaini ya kupata Katiba mpya itakayotokana na Katiba inayopendekezwa!!!
 
Huwezi kuelewa kwa sababu umeamua kuiweka akili yako nzuri pembeni ili kutetea katiba pendekezwa maana kwako ni mradi, ila kwetu sisi katiba mpya na bora ni msingi kwa vizazi vyetu vijavyo. Aliwahi sema Jenerali ulimwengu kuwa kuna watu wanaakili ila kuna kipindi huweka akili yao pembeni ili kutetea nakulinda maslahi yao, sasa ww jiulize uko kundi gani.

Read all my posts about KATIBA, you will clearly understand my message, swali utaweza?

Najua tu hatakua na muda wa kusoma post zako!!! anayezisoma anatakiwa awe na uso wa ndimu maana ukakasi kibao afu haueleweki hoja zigzag, swaga tupu!!!!
 
Hivi mtu utaelewa kitu ambacho hujawa tayari kukielewa? Tuache propaganda humu jf na tuisome katiba inayopendekezwa ili tuielewe vzr na hivyo tutaepuka upotoshaji unaofanywa na watu wachache
 
Hivi mtu utaelewa kitu ambacho hujawa tayari kukielewa? Tuache propaganda humu jf na tuisome katiba inayopendekezwa ili tuielewe vzr na hivyo tutaepuka upotoshaji unaofanywa na watu wachache

Ni kweli, hawa vinara wa upotoshaji ndiyo vimbele mbele wa kuupotosha umma wa Watanzania. ILI kuondoka kwenye udanganyifu huo, nashauri watu waisome Katika Inayopendekezwa ili kuondoa upotoshaji wa makusudi wanaoufanya watu wachache kwa malengo wanayoyajua wao wenyewe na sii malengo ya taifa letu.
 
Najua tu hatakua na muda wa kusoma post zako!!! anayezisoma anatakiwa awe na uso wa ndimu maana ukakasi kibao afu haueleweki hoja zigzag, swaga tupu!!!!
Mpaka waka wa jana unaisha, ulikuwa umenunua vitabu vingapi vya kujisomea?
 
Mpaka waka wa jana unaisha, ulikuwa umenunua vitabu vingapi vya kujisomea?
Jiulize wewe, usiwanange wenzio, kusoma hiyo Katiba yenyewe hutaki afu unabishabisha sasa unadhani utaelelwa? Mambo ya vitabu si mahala pake hapa, tunaelmishana kuhusu hii katiba na sie mijadala isiyokuwa na maana, weka hoja ya maana ujibiwe.
 
Nilitaka kujua kama ni msomaji wa vitabu, nawe pia umeonesha sio msomaji wa vitabu ndiyo maana umeona kuwa namnanga/nakunanga. Huu pia ni ushahidi tosha kuwa ww na wenzako mnachokifanya ni mradi maalumu, mmeelekezwa cha kufanya. Tena hata dhamira zenu zinawashtaki kwa kukosa uzalendo kwa Taifa lenu. Nina wasiwasi sijui hata hiyo katiba mnaelewa mnapoisoma hiyo katiba pendekezwa.maana Nimewaona hamna mawazo huru.

Ndiyo maana mnashabikia yale ambayo hayana manufaa kwa nchi ila yamo kwenye Katiba Pendekezwa, mtu akiuliza kwanini tuwe na mawaziri 40, majibu yenu ni walioweka hivyo wanaakili kuliko tunaolalamika; kwanini katiba iliruhusu viongozi kuwa na akaunti nje ya nchi, majibu yenu ni walioweka hivyo wanaakili kuliko tunaolalalmika, na hamjui kuwa huo ni uhujumu wa uchumi wa nchi, halafu kama pesa hizo ni za halali kwanini uogope kuziweka ktk nchi yako, ili wananchi wenzako wananufaike na pesa hizo kwa kuzikopa ktk benki uliyoweka!!!!!!; kwanini maadili yamewekwa hovyo hovyo, majibu yenu ni walioweka hivyo wanaakili kuliko tunaolalamika eti sisi tunaosema hivi hatujasoma hilo andiko, tena sio wazalendo tena hatulitakii mema Taifa letu; mbona madaraka ya rais yako hivi, ubunge na sifa zao dhaifu kwanini iwe hivi, majibu yenu ni walioweka hivyo wanaakili kuliko tunaolalamika; etc.

Huwezi kukosoa usichokijua, mimi nasema haya kwa sababu nimeisoma na kuielewa...Sio kwamba yote yaliyomo ni mabaya no, mazuri yapo na mabaya yaliyowekwa kwa makusudi yapo, hayo ndiyo tunayosema katiba isipitishwe yafanyiwe marekebisho kwanza, but our cry has fallen on deaf ears. Ila cha kufurahisha ni kuwa hiyo katiba itapita na haitadumu, as the cry for new constitution will not stop mpaka ipatikane inayozingatia maoni ya wananchi sio ya watetea maslahi yao. Inawezekana kupatika Katiba Bora Kabisa hapa Tanzania tukiwa wazalendo wa kweli sio wa kinafiki
 
You wanted us to hear from you, yes, we have heard, now you can go and collect your package at peace
Mwakaboko you look like having a corrupt mind that's why you keep telling others to receive their package as if you are the one who is paying them. Wahenga wanasema kuwa kimtokacho mtu ndicho kiujazao moyo wake. Sol if every time you keep repeating mshiko you are the one who is receiving that mshiko or rather you are fighting for it. Stop that remain in the topic. Vote YES for Katiba Inayopendekezwa and you will be safe.
 
Back
Top Bottom