Huyo uliyemquote hapo juu kapotosha, in my post nilisema mawaziri 40, wote kwa ajili ya nini, Arobaoni ni wengi sana hawahitajiki. Ukaamua kutumia lugha ya kejeli dhaidi yangu. Mawaziri 40 wa nini. Leo kuna wizara zipo, hazikustahili kuwa wizara ila kwa kuwa mkubwa hajambi basi zipo. Tuwe wazalendo jamani kwa Taifa letu maskini, mnapokula good time mjini mkumbuke huku vijijini watu wanahangaika maji hakuna, pesa zipelekwe kwenye maendeleo ya jamii ya Kitanzania siyo kutunza mawaziri, na hilo linawezekana tukiwa na wizara chache, maana kumtunza waziri mmoja ni gharama kubwa sana kuliko mkurugenzi