NYARAKA: Katiba Inayopendekezwa Oktoba, 2014 (Tanzania's Proposed Constitution)

NYARAKA: Katiba Inayopendekezwa Oktoba, 2014 (Tanzania's Proposed Constitution)

The problem l is not about the contents of our new proposed constitution. How was it progressed? How about procedures in common house or constitution parliament, were they democratic on grounds of vote, right to privacy and e. t. c. If these rights were ultra vired to representatives in common house i think it quash the definite of katiba bora.. But you have ma vote.. What am trying is to capture your views hypothetically..
 
kwa kweli wanaosema katiba inayopendekezwa ina dosari au kasoro ni wanafiki na hawafai ktk taifa hili,mana katiba imezingatia mambo yote ya msingi kwa mujibu na mustakabari wa maendeleo ya taifa letu la tanzania,nawaomba watanzania wenye lengo la kuendleza nchi yetu tuipokee katiba na muda ukifika tukapgie kura ya ndio,katiba yetu ni nzuri sana naomba tuipokee,kweli sita ni simba dume amehmiri sana kurupushan za bunge la katiba,hongera rahis kikwete kwa jitihada zako za kuwezesha bunge la katiba,

Wewe ndo mnafiki na wenzako wana ccm wez wakubwa nyie mpaka tuwachome moto cc hatutawapeleka kwenye chombo cha sheria maana nao n wez walewale bali moto ndo unawatosha saaaaana
 
Chenge tutamwanzia kumchoma moto make ameiba hela nying saana na jk wake
 
Naweza kutumiwa rasmu ya katiba pendekezwa ya jaji Warioba na hii mpya ya bunge kwenye email yangu ambayo ni mejaeunho@gmail.com
 
Katiba inayopendekezwa ni nzuri sanaaaa kwa mara ya kwanza kabisa katiba imeweka wazi haki za makundi mbalimbali katika jamii... Baadae zitatungwa sheria za kuzilinda ibara hizo my. Ibara ya 51.. Kuna ibara inayoongelea suala la vijana kwa mara ya kwanza.. Katiba inatamka uwepo wa Baraza la vijana la Taifa ili kuwaleta vijana wa Kada mbalimbali pamoja na kujadili changamoto zao... Tuipigieni kura ya ndioooo katiba hii
 
Haya ndio mawazo yako ila kama ni kweli wewe ni mdau wa katiba mpya tuambie kuna tofauti gani kati ya rasimu ya mwisho ya katiba na katiba inayopendekezwa
 
Nimejitahidi kusoma katiba pendekezwa. Tofauti yake na ile ya 1977 ni ndogo sana. Bado Rais anaendelea kuwa na madaraka makubwa, yaani Rais anateua watendaji wengi ambapo Wananchi hawawezi kuwaondoa, Rais ameendelea kuwa mfalme.
Waziri kaendelea kuwa Mbunge wa kawaida
Wateule wa Rais hawadhibitishwi na Bunge kama ilivyo kuwa katika Rasimu ya Warioba
Wabunge wameongezwa zaidi, hii ni mzigo kwa walipa kodi


Kwa ujumla ni propaganda tu za kusema eti haki za wafugaji. Hii katiba pendekezwa imekidhi matakwa ya watawala na wala si Raia wa kawaida

Vipengele vyote vimepitiwa na matakwa ya wananchi kwenye katiba hii yamezingatiwa.Na hata sheria mbovu zilizolalamikiwa zitapoteza nguvu
 
hiv ni kwanini mtu ukimuuliza tofauti kati ya katiba mpya na ya warioba atakimbilia madaraka ya Rais?
 
Huna hoja wewe hapa tunazungumzia issues, kama huna hoja kaa kimya waachie wengine wachangie ambao wameisoma na kuielewa najua hujaisoma wewe!
 
Wewe ndo mnafiki na wenzako wana ccm wez wakubwa nyie mpaka tuwachome moto cc hatutawapeleka kwenye chombo cha sheria maana nao n wez walewale bali moto ndo unawatosha saaaaana


Wewe ndio mwizi na kwenye mjadala huu hautakiwi kuingia kwa sababu unawaza uhalifu,na hata jambo lako unalolipigania linafanana na wewe na maamuzi yako ya kujichukulia sheria mkononi, watu kama nyie mnatakiwa mfukuzwe nchini, unakula, unalala na kwenye ardhi ya Tanzania afu unaongea mambo yasiyoeleweka.
 
Suala la miiko na maadili ya Viongozi na Watumishi wa Umma, Katiba Inayopendekezwa imeanisha vizuri sana katika Sura ya Nne, ambapo sehemu ya kwanza inaongelea maadili ya uongozi na utumishi wa umma na sehemu ya pili inagusia miiko ya uongozi wa Umma.

Hivyo kuna haja kubwa ya Watanzania kuzisoma kwa makini Sura mbalimbali za Katiba hiyo badala ya kutoa kasoro ama hoja zisizo na mashiko, kwani itakuwa jambo la aibu kudanganya Umma kuwa suala fulani halimo au limetolewa pasipo kuisoma vizuri na kuielewa kwasababu naamini mtu yeyote ambaye ameisoma kwa makini atakuwa na majibu ya hoja mbalimbali zinazoendelezwa na watu mbalimbali, mimi binafsi yangu mwanzo sikuielewa vizuri lakini nimejitahidi kuipitia kwa makini tena mara mbili mbili mpaka nimepata kugundua mambo kadha wa kadha yenye tija kwa maendeleo ya nchi yetu.
 
Kweli kabisa kuna watu wanatumika kupotosha wenzao kwa makusudi kwa kutoa kauli zisizojenga ili kuwaaminisha wengine wao copy za Katiba pendekezwa wanazo halafu wanasema hawajaelewa kisa hawajapata muda wa kusoma,hii tabia haijengi na wala haitatufikisha kokote usipoisoma wewe waache wenzako wasome, kama hauelewi omba msaada kuliko kupiga kelele ili tu tuyaamini maneno yako yasiyo na maana na wakati mwingine copy ya katiba umefungia ndani hata hujui ilipo afu unakua wa kwanza kupiga kelele tuache hizo tutakuja juta.
 
Suala la miiko na maadili ya Viongozi na Watumishi wa Umma, Katiba Inayopendekezwa imeanisha vizuri sana katika Sura ya Nne, ambapo sehemu ya kwanza inaongelea maadili ya uongozi na utumishi wa umma na sehemu ya pili inagusia miiko ya uongozi wa Umma.

Hivyo kuna haja kubwa ya Watanzania kuzisoma kwa makini Sura mbalimbali za Katiba hiyo badala ya kutoa kasoro ama hoja zisizo na mashiko, kwani itakuwa jambo la aibu kudanganya Umma kuwa suala fulani halimo au limetolewa pasipo kuisoma vizuri na kuielewa kwasababu naamini mtu yeyote ambaye ameisoma kwa makini atakuwa na majibu ya hoja mbalimbali zinazoendelezwa na watu mbalimbali, mimi binafsi yangu mwanzo sikuielewa vizuri lakini nimejitahidi kuipitia kwa makini tena mara mbili mbili mpaka nimepata kugundua mambo kadha wa kadha yenye tija kwa maendeleo ya nchi yetu.
Kama kwenye eneo la maadili umeona kitu kizuri kilichoandikwa na Chenge, basi huu ni ushahidi tosha kuwa hukuisoma Rasimu ya Pili ya Tume ya Marekebisho ya Katiba. Ukisoma rasimu halafu ukasoma Katiba pendekezwa, ndipo utaona jinsi gani Ile ya Sitta na Chenge ilivyo ya hovyo hovyo tena haistahili kupigiwa kura ya ndiyo.

Katiba Pendekezwa haitoi dawa ya kuinua uchumi bali inadidimiza uchumi wa Nchi. Kwa kuruhusu watu/watawala kujiwekea utaratibu wa kuhamisha uchumi wa nchi bila soni. Hivi ww unakubaliana na katiba inayoruhusu viongozi tena wa umma kufungua account za benki nje ya Tanzania. Tume ya Maadili kuwa toothless dog. Mawaziri wa nchi maskini kama Tanzania kuwa arobaini. Katiba kutotaja majina ya Wizara stahiki katika nchi, madaraka kurundikwa kwa mtu mmoja (Rais), mawaziri kuwa wabunge, kuwepo kwa haki zisizodaiwa mahakamani. TUMEISOMA hiyo katiba na rasimu yake, mambo ya msingi kwa Taifa letu yameondolewa, umebaki upuuzi tu. Please give me a break!!!!!!!!!!!
 
Nenda kaisome tena hasa hasa SURA YA TATU, Sehemu ya 3; MALENGO YA KIUCHUMI, KIJAMII NA KIUTAMADUNI.

Pia kasome SURA YA NNE; IBARA YA 29-(1) vifungu (a) hadi (h) kisha utakuwa umepata majibu yako.

Kuhusu idadi uliyoisema ya Mawaziri kuwa 40 nadhani umeweka kinyume ama hujaielewa Katiba hiyo, kwasababu SURA YA NANE ya Katiba Inayopendekezwa katika kipengele (b) Baraza la Mawaziri IBARA YA 115-(1) hadi (5) kimefafanua wazi wazi kuwa "Kwa mujibu wa Ibara ndogo ya (1), Idadi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano HAITOZIDI AROBAINI". sasa wewe idadi hiyo ulosema wanazidi 40 umeisoma katika Katiba gani? ndo mana nakushauri uipitie kwa makini na kuielewa.
 
Back
Top Bottom