Dragunov Sniper
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 2,795
- 9
Kama kwenye eneo la maadili umeona kitu kizuri kilichoandikwa na Chenge, basi huu ni ushahidi tosha kuwa hukuisoma Rasimu ya Pili ya Tume ya Marekebisho ya Katiba. Ukisoma rasimu halafu ukasoma Katiba pendekezwa, ndipo utaona jinsi gani Ile ya Sitta na Chenge ilivyo ya hovyo hovyo tena haistahili kupigiwa kura ya ndiyo.
Katiba Pendekezwa haitoi dawa ya kuinua uchumi bali inadidimiza uchumi wa Nchi. Kwa kuruhusu watu/watawala kujiwekea utaratibu wa kuhamisha uchumi wa nchi bila soni. Hivi ww unakubaliana na katiba inayoruhusu viongozi tena wa umma kufungua account za benki nje ya Tanzania. Tume ya Maadili kuwa toothless dog. Mawaziri wa nchi maskini kama Tanzania kuwa arobaini. Katiba kutotaja majina ya Wizara stahiki katika nchi, madaraka kurundikwa kwa mtu mmoja (Rais), mawaziri kuwa wabunge, kuwepo kwa haki zisizodaiwa mahakamani. TUMEISOMA hiyo katiba na rasimu yake, mambo ya msingi kwa Taifa letu yameondolewa, umebaki upuuzi tu. Please give me a break!!!!!!!!!!!
MAJIBU YAKO HAYA HAPA:
Nenda kaisome tena hasa hasa SURA YA TATU, Sehemu ya 3; MALENGO YA KIUCHUMI, KIJAMII NA KIUTAMADUNI.
Pia kasome SURA YA NNE; IBARA YA 29-(1) vifungu (a) hadi (h) kisha utakuwa umepata majibu yako.
Kuhusu idadi uliyoisema ya Mawaziri kuwa 40 nadhani umeweka kinyume ama hujaielewa Katiba hiyo, kwasababu SURA YA NANE ya Katiba Inayopendekezwa katika kipengele (b) Baraza la Mawaziri IBARA YA 115-(1) hadi (5) kimefafanua wazi wazi kuwa "Kwa mujibu wa Ibara ndogo ya (1), Idadi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano HAITOZIDI AROBAINI". sasa wewe idadi hiyo ulosema wanazidi 40 umeisoma katika Katiba gani? ndo mana nakushauri uipitie kwa makini na kuielewa.
