Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unafikiria kwa kutumia utumbo wewe, unabwabwaja tuu ili uingize siku.
Kama watu wenye uelewa wa namna hii wapo wengi hapa nchini,utawala bora utakuwa ni ndoto
Kwa hiyo unakubaliana nami kuwa katiba hiyo sio mpya bali ni ile ile ya zamani iliyofanyiwa marekebisho? Kwa msingi huo basi Kikwete alikuwa na haja gani ya kuunda tume ya katiba wakati alijua wazi kuwa anahitaji marekebisho ya katiba na sio katiba mpya? Au tafsiri ya upya kwenu ni kubadili kava la nje? Au ndo namna ya kuwadanganya wananchi na hao wanaojiita bunge la katiba kuwa wameweka historia ya katiba mpya kumbe ukweli wameweka historia ya kurekebisha katiba ya zamani?
Huwezi ukawa na katiba mpya yenye mfumo ule ule. Kama mahitaji yaliopo hayahitaji mfumo kubadilika basi hakukuwa na haja ya katiba mpya. Kilichotakiwa ni maboresho tu ya katiba iliopo. Kazi ilotakiwa ifanywe la bunge la jamuhuri.
Binafsi sioni haja ya mapendekezo haya kupelekwa kwa wananchi maana hayakidhi vigezo vya upya wa katiba.
Kama Hakuna mabadiliko ya mfumo hakuna katiba mpya.
WanaJF
Natumaini wote ni wazima na mnaendelea kulitumikia taifa letu.
Tunaomba mwenye Nakala ya Katiba inayopendekezwa airushe humu mjengoni ili tuanze kazi ya kufanya mahusianisho na ile ya Mhe. sana Mzee wetu Jaji Sinde Warioba. Nitahukumu BMK baada ya kuisoma hiyo katiba ili niweze kuwa na "grounds" za kuitetea au kuikataa. Tafadhali wadau irusheni. Jana Nilishamwona Mhe. Lissu akiwa nayo Arusha. Kama vipi Katibu wa Bunge Kashilila airushe kwenye mtandao wa Bunge au warudishe na zile document za Warioba warushe maana wameshamaliza mission yao.
...Hatuwezi kuwa na mtazamo mmoja, na ikifika wakati watanzania wote tukawa na mawazo yanayofanana basi tujue kwamba tunapaswa kujitazama upya. Kutofautiana kimtazamo ni jambo la kawaida na
...
KATIBA INAYOPENDEKEZWA NI BORA KULIKO YA SASA, HONGERA MH. RAISI, HONGERA WATANZANIA.
Katika historia ya uandishi wa katiba mpya duniani hakuna nchi yeyote ambayo iliwahi kuandika katiba mpya ikakidhi matakwa ya wananchi wote na taifa kwa 100%. Katiba si msaafu wala si biblia kwamba haiwezi kufanyiwa maboresho. Leo hii jambo ambalo tumeliona lina tija na manufaa kwa taifa na tukaliingiza kwenye katiba, kesho tutaliona halina tija na tutakubaliana kuliondoa au kuliboresha. Vilevile jambo ambalo leo tumeliona halina tija na kutoliingiza ndani ya katiba kesho tutaona umuhimu wake na tutakubaliana kuliingiza ndani ya katiba yetu.
Katiba inayopendekezwa imetambua haki za makundi mbalimbali kama vile wakulima, wafugaji, wafanyakazi, wasanii, vijana, wanawake na wengine. Pia katiba inayopendekezwa imetambua haki bunifu, mgombea, binafsi, maboresho katika muungano wetu sambamba na kuweka mfumo bora wa kusimamia rasirimali za taifa na kudhibiti mianya ya matumizi mabovu ya rasirimali. Kundi pekee ambalo linadhani halijatendewa haki katika katiba hii ni kundi la wanasiasa wachache ambao kwao tafsiri ya katiba bora ni ile inayokidhi maslahi yao ya kisiasa. Hili ni jambo ambalo watanzania hawana budi kulikataa.
Jambo la msingi ambalo kila mtanzania anapaswa kukubali ni kwamba katiba inayopendekezwa ni bora kuliko ile ya sasa. Wakati ambapo baadhi ya watu wakiipinga na kudai kwamba haiwezi kulivusha taifa letu, wapo watanzania tena asilimia kubwa ambao wanaiona katiba inayopendekezwa kuwa ni chombo madhubuti ambacho kitachochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hatuwezi kuwa na mtazamo mmoja, na ikifika wakati watanzania wote tukawa na mawazo yanayofanana basi tujue kwamba tunapaswa kujitazama upya. Kutofautiana kimtazamo ni jambo la kawaida na
hiyo ndiyo afya ya demokrasia iache ichukue nafasi yake. Tupingane kwa hoja bila kuhatarisha amani ya taifa letu.
Hongera Mh. Raisi Dr. Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa uliyoifanya. Hili ni jambo la kihistoria ambalo halijawahi kutokea katika historia ya Taifa. Hii ni mara ya kwanza kwa Taifa letu kuandika katiba yake kwa kushirikisha wananchi wake. Yapo mataifa ambayo yaliwahi kuandika katiba zao kwa kutumia Bunge la katiba pekee, wapo waliogeuza Bunge la kawaida na kuwa Bunge la katiba. Kwa taifa letu, mchakato umekuwa wa kidemokrasia zaidi kiasi kwamba wapo wanazuoni, wanasiasa na mataifa mbalimbali ambao wameishangaa Tanzania kwa kuruhusu demokrasia kwa kiwango hiki. Kwa hakika Mh. Rais anastahili pongezi na daima watanzania tutakukumbuka na jina lako haliwezi kufutika katika fikra zao.

Mkuu naona wewe ni member mpya mpya hapa kwenye jamvi. Hapa Kwa kawaida huwa hatuwasifii watu kufanya kazi waliomba kutaka kuifanya. Huwa hatumsifii baba kwa kumnunulia mtoto wake viatu. Kwa hiyo ni vizuri ukijisemea mwenyewe usiwasemee watanzania wote, si wote tunajikomba.
Tukiachana na hilo, tukiangalia undani wa katika yenyewe, sina hakika kama kwenye JK ndiye aliyfanya kazi ya kuandika katiba hadi astahili pongezi. Hata kama kweli utamsifu JK kwa katiba hii, inawezekana hata JK mwenyewe atakuona mj!nga, mtu yoyote mwenye akili timamu hata siku moja hawezi kusema katika hii ni nzuri. Uziru wa asilimia 80 wa katiba unaweza kusifiwa kwa nchi kama Somalia au jamhuri yoyote ya ndizi, sio Tanzania.
Kwa ulichoandika naona kabisa hata katiba yenyewe hujasoma, na hata hujui katiba yenyewe ya mwaka 1977, hujui randama ya kwanza, ya pili, na hata hii iliyochakachuliwa.
Jisemee mwenyewe usitusemee wote.