Nyaraka mpya za Kagoda zawalipua Rostam, Manji

Nyaraka mpya za Kagoda zawalipua Rostam, Manji

Nakubaliana na wewe kabisa, lakini kwanini hii habari ije wakati huu?
Kuna ajenda gani?
Ukifuatilia posts zangu, hamna sehemu yoyote nimeitetea CCM.
Ishu ya Kagoda kila mtu anaifahamu, imekuwa masikioni kwetu kwa miaka sasa! Hakukuwa na sababu yoyote ya kuifanya big deal.
Kama ishu ya kagoda inafahamika na kila mtu kwa nini basi uwe na wasiwasi kuletwa wakati huu?
 
There are currently 300 users browsing this thread. (88 members and 212 guests)


Hapo kwenye red hao 212 lazima ROSTAM na MANJI watakuwa wanakula info kupitia JF

Na Fisadi Kikwete, Lowassa na Mafisadi wengine watakuwa wanachungulia nje ya uwanja, Mzee Mwanakijiji yupo kama hayupo unahitajika hapa kutoa maoni yako.
 
Lakini Rejao naona hii taarifa imeitakasa CCM na hata Rostam mwenyewe ametakaswa kwa kuwa hakuna mahala ambapo anaonekana kwamba ni mwanzilishi wala mmiliki wa kagoda. Wacha wakamatwe hao akina Kato na Tabu na hata huyo mwanasheria Sanze.
Ha ha ni kweli CCM haihusiki kwa vile pesa hizi ziliibwa Bank of Kenya chini ya ODM party, just thinking aloud.
 
Hawa ni mafataki wa pesa kweli kweli,niliishasema hawa wezi wa mali zetu dawa yao ni kuteketeza na kuziharibu mali zao
 
kama mawasiliana ya kutoka BOT na kagoda yapo na ushahidi mkubwa wote huu basi inatakia bwana feleshi afanye fasta kuwapeleka mahakamani ...
 
Hawa wakurugenzi wanajulikana na mawakili wao pia ni maarufu hapa mjini,kwa nini hawakamatwi na kufikishwa mahakamani, badala ya kusema KAGODA HAWAJULIKANI, ilimradi watu wanawajua nivizuri mkurugenzi wa mashitaka na serikali kwa ujumla wonyeshwe ili wakamatwe.

Baada ya hapo najua mengi yatafahamika.
 
huy tabu omari na hwa kina kato ndo wa kukamatwa na haraka wafikishwe mahakamani na huko ndo watatajana ilikuwaje na nani aliwatuma maana ccm......kumbe manji nae ni jizi kubwa hivi?
 
Ameanzisha anataka mseme kisha aje kumalizia

Atakuwa anatafakari kama vile Wassira anavyotafkari Bungeni. Akija atakuja na nondo za maana hapo ndio utakapoona otofauti kati ya Wassira na Mwanakijiji. Wassira amejichokea na anatumia Masaburi, Mwanakijiji mchukiaji ufisadi kama Watanzania wengine wanavyochukia ufisadi, na mpenda Taifa lake kuliko Wassira au Kikwete.
 
Hawa wakurugenzi wanajulikana na mawakili wao pia ni maarufu hapa mjini,kwa nini hawakamatwi na kufikishwa mahakamani, badala ya kusema KAGODA HAWAJULIKANI, ilimradi watu wanawajua nivizuri mkurugenzi wa mashitaka na serikali kwa ujumla wonyeshwe ili wakamatwe.

Baada ya hapo najua mengi yatafahamika.

Mkuu nadhani hata wewe katika nafsi yako unaamini kuwa Rostam kupitia Kagoda ndiye aliyeiba pesa za EPA kwa ajili ya kuisaidia CCM katika uchaguzi wa 2005. Sasa ije kuwa wanaokamatwa kuhusiana na Kagodo ni Kato na Tabu kweli utaamini? Lakini ndivyo inatakiwa iwe kwa kuwa wao ndio wakurugenzi na RA haonekani kwenye nyaraka!! Hivi ulifuatilia kidogo kesi kati ya Mengi na Manji? Kuna kipengele Manji alimkamata pabaya Mengi baada ya kusema yeye (Manji) si mmiliki wa quality finance bali ni muajiriwa tu!! Na kweli document zinasema yeye ni mwajiriwa. Kesi iliahirishwa sijui hadi lini!!! Na kwenye Kagoda RA si mmiliki wala mwajiriwa lakini tunaamini ndiye alichukua pesa zetu na wala siyo Tabu ama Kato!! Kuthibitisha hilo kisheria ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu a sindano!!! Ukizijua sheria raha mstarehe!!
 
Hakuna jipya hapa, hizi ni kampeni za Igunga zimeanza kwa staili ya MAJITAKA.
Sishangai.....ndivyo CDM walivyo. Lakini hamna madhara, wataishia kuwa chama cha WANUNG'UNIKAJI'.
Wataishia kuwa chama cha wanung'unikaji kama waislamu(by JK).
 
Nyerere tunakumis sana.Njoo ujionee huku kwenye Nchi uliyoasisi watu wanavyokula pesa kama njugu.Maskini wanakufa na matumaini ya maisha bora yametoweka.Mungu simama usikie kilio cha watanzania
 
Jamani hii sasa ni kali,nchi hii sijui tunaipeleka.Tumsubiri huyu DPP kilaza atafanya nini maana ushahidi kashapata
 
msemakweli tunashukru sana kwa taarifa zilizojitosheleza tatizo wanasheria wanchi yetu hawana uzalendo ndio muda mwafaka wakuungana nakushitaki hili group la walanguzi wa uchumi wetu na wahuni wa nchi hii
 
Tunashukuru sana Msemakweli kwa kauli za kizalendo na matendo yanayofuatana nayo. Tunatambua kutakuwa na gharama kubwa ya kulipa kwa upande wako. Tunajua Mungu aweza kukulinda...la sivyo akiamua kutokukulinda unafia Taifa lako.
Serikali imeshaona haya na wasiwasi wetu ni lile jukumu wanalojipa a kupelekea mafisadi taarifa ili ushughulikiwe. Jipe moyo kwa hilo kwani tunakuombea.

Mheshimiwa Mwanyika ataingia aibu kwani sina shaka anao ushahidi huu ila alidhani anao yeye peke yake kwa hiyo akataka kufunika.
Hatari ni kwamba nchi yetu inaliwa na viongozi na wao ndiyo wanaofichana. Ni lazima watanzania sasa tuamue kuchukua maamuzi magumu juu ya taifa letu kama tunataka kupona.

Ubarikiwe sana ndugu Msemakweli
 
Back
Top Bottom