Nyaraka muhimu kwa Maombi ya Kazi; Barua, CV /Resume na Rejea

Mimi nafikiri CV haimaanishi kukutaka uwe na ukimo wa maelezo hapana bali unaandika maelezo yoyote ktj utendaji ambayo ulisha wahi kufanya ktk utendaji wako sehemu tofauti tofauti maeneo yake na uzoefu wako ktk vipindi tofauti na barua bila shaka huwa inasimamia ktk imbi zaidi na lengo la barua nikutaka kujua mwombaji uwezo wake hasa kiufahamu ndii maana barua nyingi zina pendekezwa kuandikwa kwa mkono.

morgnsety@gmail.com
 
Acheni mboyoyo mingi, najua wengi mmesoma na ku graduate na mpo mlioajiriwa.
Dogo amekiri kweli ni kilaza ndio maana kaja kuomba shavu. Cha msingi mtumieni cv zenu kama templates hata mkiweka majina feki na namba za magari haitadhuru. Walau adese maana ndicho hasa anachokitaka tusijifanye watu wa kuponda sana
 
naomba kuuliza

kama kampuni imetoa ajira, na kwenye hizo ajira kuna nafasi mbili unaweza kuzifanya.!

je, utaandika barua moja kusema unaweza hizo kazi mbili au utaandika barua mbili na kila barua ikisema nafasi husika.?
maamuzi ni yako either uandike barua moja ya kazi ambayo unajua uko vzuri zaid au uandike barua za kaz zote mbili kama zinaendana na ulichosomea

Sent using Jamii Forums for iPad.
 
Wakuu, ni kwa jinsi gani ntaweza kuandika barua mzuri kwa ajili ya ajira ya kujitolea?
 
Habary jaman samahani sana kama nitakuwa nje kidogo ya mada

Mm ni kijana Ni fundi umeme wa majumbani na viwandani

Nina uzoefu wa miaka miwili na nunu kiwandan na pia miaka mitatu kwa umeme wa majumbani nipo vizuri na napatikana kibaha

Nafanya kazi popote pale itakapo patikana
Napatikana kwa mawasiliano na 0674866209
 
Yan hakuna **** yoyote alienisaidia, wote pumba 2
Tatizo lako wewe ni mvivu hio haikuwa issue ya kuuliza wana JF hata wanafunzi wenzako karibu nawe wanaweza kuwa msaada kwako... ukiona haitoshi ingia google tafuta sample za CV na ujue vitu gani vya kuandika.
 
Acheni mboyoyo mingi, najua wengi mmesoma na ku graduate na mpo mlioajiriwa.
Dogo amekiri kweli ni kilaza ndio maana kaja kuomba shavu. Cha msingi mtumieni cv zenu kama templates hata mkiweka majina feki na namba za magari haitadhuru. Walau adese maana ndicho hasa anachokitaka tusijifanye watu wa kuponda sana

Bro huwa nakukubali sana so direct,big up
 
Manufacturer: Infinix

No. Sim Cards: 2

Screen: 5.5"

Camera: 13 MP

Memory: 16 GB ,2GB

Processor: 1.5GHz

Battery: 28 Hours

Connection Type: 4G

INAUZWA BEI SAWA NA BURE 160000 TU
(PHONE USED)
IMG_20200723_201707_1.jpg
IMG_20200723_201645_2.jpg
IMG_20200723_201628_8.jpg
IMG_20200723_201606_3.jpg
 
Wasifu binafsi ni maelezo yanayopambanua maarifa, ujuzi na uzoefu alionao mtafuta kazi kwa lengo la kumshawishi mwajiri kuwa anazo sifa na vigezo vya kuweza kufanya kazi iliyotangazwa.

[emoji117] kuandika wasifu binafsi, mambo saba ni ya muhimu kuzingatia:

1. Taarifa za msingi za mtafuta kazi
Weka taarifa zinazokutambulisha kama vile majina yako kamili, jinsia, hali ya ndoa, tarehe ya kuzaliwa, utaifa na njia muhimu za mawasiliano zinazoweza kutumiwa kukufikia.
Mfano:
Jina:
Utaifa:
Mahali pa kuzaliwa:
Tarehe ya kuzaliwa:
Hali ya Ndoa:
Anwani ya Posta:
Simu:
Barua pepe:

Hata hivyo, zipo taarifa nyinginezo zinazoweza kuwa muhimu lakini zisizo na ulazima wa kufahamika. Hizi ni kama kabila, dini, idadi ya watoto na mitazamo au ufuasi wa kisiasa.

Unaweza kuwa na aya moja yenye mhutasari wa wasifu wako, ukaeleza tunu zinazoongoza utendaji wako wa kazi. Aya hii inapoandaliwa vizuri hujenga taswira ya mtu anayejitambua.

2. Sifa za kitaaluma
Kuna namna nyingi za uandikaji wa sifa hizi, lakini kilicho muhimu ni kueleweka. Anza na ngazi ya juu zaidi ya kitaaluma uliyofikia na shuka mpaka ngazi ya chini. Onesha mwaka yalipofanyika mafunzo hayo, tunuku ya kitaaluma (mfano cheti, Stashahada, shahada) na chini yake taja taasisi iliyotoa tunuku hiyo na mahali ilipo (mfano shule, chuo na kadhalika).
Mfano;
2011-2013: Shahada ya Sanaa katika Stadi za Mazingira
Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge, Moshi

Kwa kawaida, sifa hizi huwa ni zile zinazohusiana na mafunzo ya ujuzi yatolewayo kwa ngazi ya chuo kukupa utaalam. Lakini waweza pia kutaja ngazi ya Cheti cha Juu cha Elimu ya Sekondari na Cheti cha Elimu ya Sekondari.

3. Uzoefu na historia ya kuajiriwa

Onesha ajira ulizowahi kuzifanya iwe kwa ajira rasmi au kwa kujitolea. Orodhesha uzoefu wako kwa mtiririko wa aina ya ajira kuanzia ya hivi karibuni zaidi au uliyonayo, taasisi husika pamoja na mwaka wa kuanza na kumaliza kazi hiyo.

Kumbuka kuwa mwajiri makini hutafuta kuona maneno muhimu kama "kuzalisha/kuongeza (ufanisi)", "kupunguza/kuondoa (changamoto)", "kubuni", "kuanzisha", "kusababisha", "kubadili", "kuchangia mabadiliko", "kuwezesha" na mengineyo.

Kwa mfano,

2013-2015: Mwandishi wa Habari za Mazingira, Mwananchi Communications Ltd

Kwa kushirikiana na wenzangu, nilibuni utaratibu wa…ambao ulisaidia kuondoa changamoto ya…iliyokuwepo awali.

Usipoteze muda kueleza majukumu yako ya kila siku. Tafuta maeneo ambayo mchango wako ulionekana na yataje kwa kutumie vitenzi tulivyovitaja hapo juu.

4. Ujuzi na weledi

Katika sehemu hii onesha aina ya ujuzi na weledi uliowahi kuupata kupitia warsha, semina na makongamano yalivyokusaidia kuongeza ujuzi mwepesi unaoweza kukusaidia "kuzalisha", "kukuza", "kubuni", "kuanzisha", "kusababisha", "kubadili", "kuchangia mabadiliko" na "kuwezesha". Onesha mahali, mwaka, shughuli husika na malengo yake kwa mtiririko wa kuanzia hivi karibuni mpaka yale ya zamani.

5. Machapisho na tafiti

Kama kazi unayoomba inahusiana na masuala ya taaluma na elimu (mfano ualimu, ukufunzi, utafiti, uhadhiri), onesha machapisho na tafiti ulizowahi kuzifanya na kuziandika. Hapa, utaonesha jina la chapisho husika, mchapishaji na mwaka lilipochapishwa. Lengo ni kuonyesha ushiriki wako katika kutafuta majibu ya changamoto zinazoikabili jamii, ikiwa ni pamoja na kuchangia kukuza maarifa yaliyopo.

6. Tuzo au heshima

Mwajiri huvutiwa na mtu anayeweza kuonesha namna jitihada zake zilivyotambuliwa na wengine. Onesha namna bidii, na ari yako ya kazi ilivyowahi kutambuliwa katika ajira zilizopita. Si lazima iwe kazini tu, yaweza kuwa katika masomo, lakini ziwe tofauti na zile tunuku za kitaaluma moja kwa moja.

Maneno kama, "nilishinda", "nilituzwa" na "nilitambuliwa", kwa sababu ya shughuli, majukumu, jitihada zilizowahi kufanywa, yanakuongezea nafasi ya kukubalika.

7. Orodha ya wadhamini

Taja watu wanaoaminika wanaoweza kutoa ushuhuda wa uwezo na weledi wako. Orodhesha angalau watu watatu wenye nyadhifa zinazotambulika na wanaokufahamu vizuri iwe kwa sababu wamekufundisha au waliwahi kufanya kazi na wewe.

Ni vizuri kuwasiliana nao kabla ya kuwataja kwa kuwa wanaweza kuulizwa pasipo wewe kujua. Na wakati mwingine ni vyema kuwaomba kukuandikia barua ya utambulisho ukazitumia inapolazimika.

Zingatia

-CV nzuri hubadilika kukidhi matakwa ya kazi inayoombwa.

-Imeandikwa kwa ufupi na haizidi kurasa mbili

-Ina taarifa nyingi muhimu lakini kwa maelezo yanayoonekana kirahisi

-Imeandikwa kwa umakini na haina makosa ya kiuchapaji

-Haina taarifa zilizotiwa chumvi au uongo

-Haina picha ya mwombaji
Asante sana je nilazma iwetyped
 
Mkuu, kwa mtu aliyemaliza chuo kikuu lkn bado hajapata matokeo ya semista ya mwisho hvy hana cheti, naweza kuandika cv kueleza nmemaliza chuo kikuu.? Kama naweza, naandikaje.?
 
wadua habari ,naombeni msaada ni kampuni zipi ,zinasaidia kupata kazi katika ofisi mbalimbali,yani huwa wanatumiwa na taasisi mbali mbali kuwatafutia wafanyakazi ,mfano kuna dada anafanya kazi MSD ,alipata kazi kupita kampuni fulani inawafanyia usahili mkifaulu mnaajiliwa
 
Back
Top Bottom