Ulizauliza
Sent using Jamii Forums mobile app from my Android phone
Bro naomba nielekeze namna ya kuandika/kuandaa izo project.Cv yangu siku zote inakuwaga na page nzima ya PROJECTS hapo huwa naelezea viproject vyangu na jinsi ya kuviimplement kazini thank God nimeitwa kwingi kwenye interview kutokana na hizo projects nnazoandikaga....
Sent using Jamii Forums mobile app
Hello bro project za somo gani ingawa zinaendana katika uandikaji ila nataka nikupe project ambazo nimeziandika na kuitwa interview nadhan niliyotumia kupata ajira
maamuzi ni yako either uandike barua moja ya kazi ambayo unajua uko vzuri zaid au uandike barua za kaz zote mbili kama zinaendana na ulichosomeanaomba kuuliza
kama kampuni imetoa ajira, na kwenye hizo ajira kuna nafasi mbili unaweza kuzifanya.!
je, utaandika barua moja kusema unaweza hizo kazi mbili au utaandika barua mbili na kila barua ikisema nafasi husika.?
Tatizo lako wewe ni mvivu hio haikuwa issue ya kuuliza wana JF hata wanafunzi wenzako karibu nawe wanaweza kuwa msaada kwako... ukiona haitoshi ingia google tafuta sample za CV na ujue vitu gani vya kuandika.Yan hakuna **** yoyote alienisaidia, wote pumba 2
Acheni mboyoyo mingi, najua wengi mmesoma na ku graduate na mpo mlioajiriwa.
Dogo amekiri kweli ni kilaza ndio maana kaja kuomba shavu. Cha msingi mtumieni cv zenu kama templates hata mkiweka majina feki na namba za magari haitadhuru. Walau adese maana ndicho hasa anachokitaka tusijifanye watu wa kuponda sana
Hakika mkuu! Watu wanajitoa akiliBro huwa nakukubali sana so direct,big up
Asante sana je nilazma iwetypedWasifu binafsi ni maelezo yanayopambanua maarifa, ujuzi na uzoefu alionao mtafuta kazi kwa lengo la kumshawishi mwajiri kuwa anazo sifa na vigezo vya kuweza kufanya kazi iliyotangazwa.
[emoji117] kuandika wasifu binafsi, mambo saba ni ya muhimu kuzingatia:
1. Taarifa za msingi za mtafuta kazi
Weka taarifa zinazokutambulisha kama vile majina yako kamili, jinsia, hali ya ndoa, tarehe ya kuzaliwa, utaifa na njia muhimu za mawasiliano zinazoweza kutumiwa kukufikia.
Mfano:
Jina:
Utaifa:
Mahali pa kuzaliwa:
Tarehe ya kuzaliwa:
Hali ya Ndoa:
Anwani ya Posta:
Simu:
Barua pepe:
Hata hivyo, zipo taarifa nyinginezo zinazoweza kuwa muhimu lakini zisizo na ulazima wa kufahamika. Hizi ni kama kabila, dini, idadi ya watoto na mitazamo au ufuasi wa kisiasa.
Unaweza kuwa na aya moja yenye mhutasari wa wasifu wako, ukaeleza tunu zinazoongoza utendaji wako wa kazi. Aya hii inapoandaliwa vizuri hujenga taswira ya mtu anayejitambua.
2. Sifa za kitaaluma
Kuna namna nyingi za uandikaji wa sifa hizi, lakini kilicho muhimu ni kueleweka. Anza na ngazi ya juu zaidi ya kitaaluma uliyofikia na shuka mpaka ngazi ya chini. Onesha mwaka yalipofanyika mafunzo hayo, tunuku ya kitaaluma (mfano cheti, Stashahada, shahada) na chini yake taja taasisi iliyotoa tunuku hiyo na mahali ilipo (mfano shule, chuo na kadhalika).
Mfano;
2011-2013: Shahada ya Sanaa katika Stadi za Mazingira
Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge, Moshi
Kwa kawaida, sifa hizi huwa ni zile zinazohusiana na mafunzo ya ujuzi yatolewayo kwa ngazi ya chuo kukupa utaalam. Lakini waweza pia kutaja ngazi ya Cheti cha Juu cha Elimu ya Sekondari na Cheti cha Elimu ya Sekondari.
3. Uzoefu na historia ya kuajiriwa
Onesha ajira ulizowahi kuzifanya iwe kwa ajira rasmi au kwa kujitolea. Orodhesha uzoefu wako kwa mtiririko wa aina ya ajira kuanzia ya hivi karibuni zaidi au uliyonayo, taasisi husika pamoja na mwaka wa kuanza na kumaliza kazi hiyo.
Kumbuka kuwa mwajiri makini hutafuta kuona maneno muhimu kama "kuzalisha/kuongeza (ufanisi)", "kupunguza/kuondoa (changamoto)", "kubuni", "kuanzisha", "kusababisha", "kubadili", "kuchangia mabadiliko", "kuwezesha" na mengineyo.
Kwa mfano,
2013-2015: Mwandishi wa Habari za Mazingira, Mwananchi Communications Ltd
Kwa kushirikiana na wenzangu, nilibuni utaratibu wa…ambao ulisaidia kuondoa changamoto ya…iliyokuwepo awali.
Usipoteze muda kueleza majukumu yako ya kila siku. Tafuta maeneo ambayo mchango wako ulionekana na yataje kwa kutumie vitenzi tulivyovitaja hapo juu.
4. Ujuzi na weledi
Katika sehemu hii onesha aina ya ujuzi na weledi uliowahi kuupata kupitia warsha, semina na makongamano yalivyokusaidia kuongeza ujuzi mwepesi unaoweza kukusaidia "kuzalisha", "kukuza", "kubuni", "kuanzisha", "kusababisha", "kubadili", "kuchangia mabadiliko" na "kuwezesha". Onesha mahali, mwaka, shughuli husika na malengo yake kwa mtiririko wa kuanzia hivi karibuni mpaka yale ya zamani.
5. Machapisho na tafiti
Kama kazi unayoomba inahusiana na masuala ya taaluma na elimu (mfano ualimu, ukufunzi, utafiti, uhadhiri), onesha machapisho na tafiti ulizowahi kuzifanya na kuziandika. Hapa, utaonesha jina la chapisho husika, mchapishaji na mwaka lilipochapishwa. Lengo ni kuonyesha ushiriki wako katika kutafuta majibu ya changamoto zinazoikabili jamii, ikiwa ni pamoja na kuchangia kukuza maarifa yaliyopo.
6. Tuzo au heshima
Mwajiri huvutiwa na mtu anayeweza kuonesha namna jitihada zake zilivyotambuliwa na wengine. Onesha namna bidii, na ari yako ya kazi ilivyowahi kutambuliwa katika ajira zilizopita. Si lazima iwe kazini tu, yaweza kuwa katika masomo, lakini ziwe tofauti na zile tunuku za kitaaluma moja kwa moja.
Maneno kama, "nilishinda", "nilituzwa" na "nilitambuliwa", kwa sababu ya shughuli, majukumu, jitihada zilizowahi kufanywa, yanakuongezea nafasi ya kukubalika.
7. Orodha ya wadhamini
Taja watu wanaoaminika wanaoweza kutoa ushuhuda wa uwezo na weledi wako. Orodhesha angalau watu watatu wenye nyadhifa zinazotambulika na wanaokufahamu vizuri iwe kwa sababu wamekufundisha au waliwahi kufanya kazi na wewe.
Ni vizuri kuwasiliana nao kabla ya kuwataja kwa kuwa wanaweza kuulizwa pasipo wewe kujua. Na wakati mwingine ni vyema kuwaomba kukuandikia barua ya utambulisho ukazitumia inapolazimika.
Zingatia
-CV nzuri hubadilika kukidhi matakwa ya kazi inayoombwa.
-Imeandikwa kwa ufupi na haizidi kurasa mbili
-Ina taarifa nyingi muhimu lakini kwa maelezo yanayoonekana kirahisi
-Imeandikwa kwa umakini na haina makosa ya kiuchapaji
-Haina taarifa zilizotiwa chumvi au uongo
-Haina picha ya mwombaji
AsanteeeHabari zenu wana-JF?
Naomba msaada wa jinsi ya kuandaa CV yangu..
Mie ni mwanafunzi wa mwaka wa mwisho Computer science, nataka kuandaa CV yangu vizuri.
Shukrani!
Mifano ya Barua ya Maombi, Wasifu (Resume) na Rejea (Reference):
Kwa hisani ya HMS
Mkuu, kwa mtu aliyemaliza chuo kikuu lkn bado hajapata matokeo ya semista ya mwisho hvy hana cheti, naweza kuandika cv kueleza nmemaliza chuo kikuu.? Kama naweza, naandikaje.?Wasifu binafsi ni maelezo yanayopambanua maarifa, ujuzi na uzoefu alionao mtafuta kazi kwa lengo la kumshawishi mwajiri kuwa anazo sifa na vigezo vya kuweza kufanya kazi iliyotangazwa.