Nyaraka muhimu kwa Maombi ya Kazi; Barua, CV /Resume na Rejea

Nyaraka muhimu kwa Maombi ya Kazi; Barua, CV /Resume na Rejea

Curriculum vitae ..... Elimu yako na kazi zako za kitaalam. Utaalam wowote ule, research papers, shule ulizopitia, ,jourals ulizoandika kwenye majarida ya kitaalam etc.. ni sawa na kueleza uwezo wako kitaalam na hutumiwa na watu waliosoma elimu za juu sana kama PhDs wakati wakomba kazi zinazohitaji utaalam mkubwa.

Wengi wetu tunapenda kufananisha hii na "Resume" ambayo ni historia yako kikazi na kielimu, kwa watu ambao wanatafuta kazi wakiwa na utaalam wa kawaida na katika fields ambazo siyo rare professions.

Kwa mfano, karani wa Benki huombwi CV ila resume. Mtafiti wa dawa ya Ebola, huombwa CV, siyo resume.
 
Namna ya kuandika CV bomba/nzuri.


CV yenye kujitosheleza ni njia muafaka ya kumfanya bosi wako mtarajiwa kukufahamu wewe. CV nzuri inakupa nafasi ya kung’aa katika kikundi na kupata fursa ya usahili na baadae kazi.

Pitia matangazo ya kazi

Unapopitia matangazo ya kazi katika magazeti, kuta za matangazo au barua pepe hakikisha unapitia matangazo hayo kwa umakini. Fanya maamuzi ya kipi kati ya ujuzi, sifa ama uzoefu utatumia katika kazi yako mpya.


Orodhesha vitu hivi na tumia maneno yenye kuonyesha vitendo kwa mfano : Mimi ni mtu mwenye mpangilio, ufanisi na mchapa kazi, nimeongoza na kusimamia watu na matukio. Nimesoma na kufikia ubora katika weledi na kumaliza shahada ya kwanza katika…..

Kua sahihi kwa kutoa maelezo mafupi yenye kueleweka
Usizidishe maelezo kwa kutoa maelezo yote kukuhusu wewe, hakuna anayetegemea wala kutaka kuyasikia hayo kwa hiyo usifanye hivyo.


CV inatakiwa kumwelezea mtu lakini si kama kitabu kinachoelezea wasifu wako lakini pia si aya/ibara ama kitabu unachoelezea hadithi ya maisha yako ya weledi! Hakikisha huweki taarifa zako binafsi ambazo hazihusiani na nafasi unayoomba.


Sema ukweli

Kua mkweli. Kwa kufanya hivyo unaonyesha kujiamini na mafanikio yako na hii itakusaidia inapokuja kukaa kwa ajili ya usahili. Huwezi kuzungumza kuhusu uzoefu wako kama mwanasayansi wa nyuklia kama hukufaulu masomo ya sayansi shuleni!


Epuka makosa haya

Vitu vichache vya kuepuka kufanya: Usidanganye, usizidishe chumvi, usiweke ahadi usizoweza kuzitimiza.


Vidokezo katika kujielezea

Orodhesha majumuisho yako.
Elezea CV yako katika lugha chanya.
Inasaidia kama utaandika sentensi fupi na zenye kuonyesha uhai na kuepuka kutumia vivumishi vingi.

Anza na mafanikio yako ambayo yanawiana na mahitaji muhimu ya kazi. Usimweleze mwajiri ni kwa vipi atakusaidia bali mueleze ni kwa vipi wewe utamsaidia.

Tia msisitizo katika uzoefu unaohusiana na biashara ama kazi husika. Kama una uhusiano mzuri wa kazi na wataalamu katika fani yako unaweza kuwaomba kuwatumia kama wadhamini.


Pata ushauri kabla hujatuma CV yako. Tafuta mtu unaemjua katika fani husika ili apitie CV yako. Jiandae kurekebisha vitu ulivyoandika.


Jaribisha CV yako kwa kuomba nafasi mbalimbali katika kiwango chako lakini pia kiwango cha juu kidogo. Hii itakusaidia kujua soko la ajira na thamani yako.


Isiwe sawa kila wakati

CV yako inabidi iwe inaendana na kazi unayoomba. Hivyo basi wakati unaomba kazi tofauti kwa kutumia CV ile ile ni vizuri ukajaribu kuiweka CV ikaendana na nafasi unayoomba.


Usikate tamaa

Tumia CV yako kuitwa kwenye usahili. Huko utapata fursa ya kuelezea mafanikio yako.
Kitu cha muhimu, USIKATE TAMAA! Kwa kila CV 100 unazotuma unaweza kuitwa kwenye usahili mara 10, na katika mara kumi hizi utapata kazi moja tu- kazi yako ipo inakusubiria. Kua makini na mwenye malengo na muda si mrefu utakua mmoja ya watu katika dunia ya kazi.

Chanzo: http://www.mywage.org/tanzania-sw/nyumbani/kazi/kutafuta-kazi/andika-cv-nzuri
 
Habari.

Nimekutengenezea CV. Nime ambatanisha mafaili matatu. Kuna cover letter, Resume na Reference ambayo ni referee.

Hata siku moja usiweke referee kwenye CV yako. na usije ukaandika Curriculum Vitae kwenye Resume yako, ni makosa. utaonekana sio professional.

Natumai nimekupa mwanga. Unaweza uka edit hizo attachments kutokana na ujuzi na kisomo chako.
 

Attachments

CV
Personal particulars
Name
Sex
Marital stastus
Address
Contacts i.e emails
Height
EDucation background
Unaanzia level ya elimu yako then unamalizia na level ya chini kabisa.
WORKING EXPERIENCE
unapangilia kama kwenye education background.
ADMINSTRATIVE EXPERIANCE(LEADERSHIP)
Hapa utaandika uzoefu wako katika uongozi.
OTHER SKILLS
Ujuzi ulionao aina yayote utaandika hapa.
HOBI
Utaandika hobi yako/zako
INTRESTI
.............
SEMINA, SIMPOZIAMU,
PRESENTATION
.. .. .
......

RESEARCH
.. .........
Referees
..andres na contacts zao.

NB:: CV huwa inabadilika na inafanyiwa marekeb
isho kutokana na uhitaji pia na muhuska kuendelea kupata maarifa mbalmbal.
Nilichotoa ni kama mfano wa mpangilio wa cv
 
Habari.

Nimekutengenezea CV. Nime ambatanisha mafaili matatu. Kuna cover letter, Resume na Reference ambayo ni referee.

Hata siku moja usiweke referee kwenye CV yako. na usije ukaandika Curriculum Vitae kwenye Resume yako, ni makosa. utaonekana sio professional.

Natumai nimekupa mwanga. Unaweza uka edit hizo attachments kutokana na ujuzi na kisomo chako.

Una busara sana. #Barikiwa
 
  • Thanks
Reactions: HMS
Samahani nitumie application ipi ili niweze kuzifungua?

Salaam.
Natumai ni mzima.
Hiyo ni microsoft office word 2014. hata word 2010 unaeza kufungua.
Ahsante.
 
Back
Top Bottom