Uchaguzi 2020 Nyehunge: Dkt. Magufuli amuamrisha Mfugale atangaze ujenzi barabara ya Sengerema-Nyehunge (KM 46) kisha amuulize hela za kujengea

Hivi Mheshimiwa anajua nini maana ya kampeni za uchaguzi wa Rais? Na pia anatambua nini kinachopaswa kufanyika wakati wa shughuli za kampeni? Na kweli alisoma kwa kina na kuzielewa kanuni na maadili ya wagombea kutokana na tume ya uchaguzi?

Rais wa Tanzania ni kama Mfalme kutokana na katiba yetu ya leo.
 
Hiyo ni rushwa alitakiwa awe ameijenga siku nyingi, hata kutoa ajira 13000 na kutoa bima ya afya wakati wa kampeni ni rushwa pia.

Bima si ni ahadi Mzee au keshatoa tayari?
 
ukisikia uhuni ndiyo huu!
 
Mgombea aliyekuwa madarakani lakini kampeni zinampeleka puta hadi hadi amepaniki, tatizo aliaminishwa kuwa anapendwa sana!

Mabango makubwa njiani utasema ndo anagombea mara ya kwanza!!
 
Sasa kwaakili za kawaida (usifikiri kiccm) unaona kuna uwanja sawa wa kushindana na vyama vingine vya siasa?
 
Kama anatoa pesa yake kuna tatizo gani
 
Miradi ipi inayoweza kuchukua miaka 20?
 
Ni tatizo la katiba Mgombea Urais wakati huo huo ni Rais ndo madhara yake haya.
Katiba ya marekani inasemaje maana uchaguzi ni mwaka huu na trump anaachia lini madaraka kabla ya uchaguzi.
 
Hii barabara ya Sengerema nyehunge nkome nzela inapita kandokando mwa ziwa na hasa eneo la nkome ni swamp, hii swamp inaenda kasamwa mgoma salawe hadi mwakitolyo. ikijengwa kwa lami haitadumu.

Mie napendekeza ijengwe kwa zege, kwanza tutakuwa tumeokoa fedha zetu za kigeni na itadumu muda mrefu sana kwani cement na maji ni kama pilau na kachumbari wanapendana sana.

Uhai wa barabara ya Zege ni miaka 45 tofauti na lami ni miaka minane unaanza viraka. Na kwa hii barabara ni miaka miwili tunaanza kuziba viraka.
 
Hii na ule ubwabwa wa Hashim Rungwe Spunda tofauti ni ipi? TAKUKURU wataingia chini ya carpet
 
Ni tatizo la katiba Mgombea Urais wakati huo huo ni Rais ndo madhara yake haya.
Sasa mbona mtu kama huyu kushindwa uchaguzi ni ngumu sana, hii ni rushwa.
 
Hivi Mheshimiwa anajua nini maana ya kampeni za uchaguzi wa Rais? Na pia anatambua nini kinachopaswa kufanyika wakati wa shughuli za kampeni? Na kweli alisoma kwa kina na kuzielewa kanuni na maadili ya wagombea kutokana na tume ya uchaguzi?
Wewe unayeyajua hayo upo wapi? Katiba bado inamtambua kuwa yeye ni rais mpaka atakapovunja baraza la mawaziri!

Fuatilia mazungumzo uone kama kuna mahali ametajwa kuwa ni mgombea! Hii ndio tz, kwingine kungetokea maandamano ya kudai pingamizi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…