Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 32,639
- 42,908
Bado ni Rais japo anagombea hivyo hamna namnaHahaha mgombea anajenga barabara wakati wa kampeni?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bado ni Rais japo anagombea hivyo hamna namnaHahaha mgombea anajenga barabara wakati wa kampeni?
Hivi Mheshimiwa anajua nini maana ya kampeni za uchaguzi wa Rais? Na pia anatambua nini kinachopaswa kufanyika wakati wa shughuli za kampeni? Na kweli alisoma kwa kina na kuzielewa kanuni na maadili ya wagombea kutokana na tume ya uchaguzi?
aaaahh wapi !! sio kila mahala!TAKUKURU ng'ataaaaaaaaaaaaaa
Hiyo ni rushwa alitakiwa awe ameijenga siku nyingi, hata kutoa ajira 13000 na kutoa bima ya afya wakati wa kampeni ni rushwa pia.
ukisikia uhuni ndiyo huu!DKT. Magufuli akiwa anaendelea na kampeni za uchaguzi 2020, amepita kijiji cha Nyehunge akiwa anaelekea Geita ambapo kutoka Sengerema mpaka Nyehunge ni kilomita 46. Alisimama kuongea na wananchi waliokuwa wakimsubiri barabarani, wakati anaielezea barabara hiyo ghafla aliomba simu yake na kumpigia mtu ambae baadae alijulikana ni mkurugenzi mkuu wa TANROADS, Injinia Mfugale na mazungumzo yao yalikuwa hivi.
Magufuli: Hallo, Chief executive
Mfugale: Naam mheshimiwa Rais
Magufuli: Hujambo
Mfugale: Sijambo mheshimiwa
Magufuli: Uko wapi?
Mfugale: Niko Dar es Salaam TANESCO tunazungumzia habari ya Nyerere dam.
Magufuli: Haya, sasa mimi niko Nyehunge, kutoka Sengerema mpaka Nyehunge ni kilomita 46, hii barabara tumeshaifanyizia feasibility study na detail design, nimesimama hapa na wananchi, nataka hii barabara, mimi si ndio Rais?
Mfugale: Ndio mheshimiwa(Wananchi kicheko cha furaha)
Magufuli: Nyehunge Oyee, Unanielewa Chief? Basi hii barabara uitangaze kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami. Huu ni mwezi wa ngapi? (Mfugale: Mwezi wa tisa). Haya uandae document zote kabla ya mwezi wa 12 haujafika na kandarasi apatikane, niulize hela nitazitoa wapi. Sawa Mfugale?
Mfugale: Nimekuelewa mheshimiwa Rais
Magufuli: Umenielewa, mueleze na Waziri kwamba hayo ni maagizo yangu wala yasibadilike, Asante sana.
MWISHO WA MAONGEZI
Sasa kwaakili za kawaida (usifikiri kiccm) unaona kuna uwanja sawa wa kushindana na vyama vingine vya siasa?Hiyi ndo dhana halisi ya kuwa na vyombo vya dola kama alivyosema Katibu Mkuu wa CCM lakini Chadema wakapotosha kwamba chombo cha dola ni Polisi. Ukiwa kwenye madaraka unakuwa na advantage kubwa ya kushinda uchaguzi maana utatoa maagizo kama haya na sheria inakuruhusu kufanya hivyo
Kama anatoa pesa yake kuna tatizo ganiHapa ndipo umuhimu wa katiba mpya unapoonekana, kuwa Rais wa nchi halafu hapo hapo kuwa mwenyekiti wa chama cha siasa ni tatizo.
Hapo Magufuli anaamua kutumia kofia yake ya Urais kujinufaisha kisiasa kwenye kampeni zake, hiIi sio sawa.
Hizi bajeti siku zote zinatakiwa kupitishwa na bunge, sio mtu mmoja anajiamulia tu, hii nchi ina sheria na taratibu zake Magufuli akumbushwe kuzifuata.
Miradi ipi inayoweza kuchukua miaka 20?Huyu jamaa hata akishindwa uchaguzi hatoki madarakani atalazimisha kuendelea
Atadai miradi alioianzisha ni mingi kwa hiyo atalazimisha kuwa lazima aione ikiisha
Miradi mingine itachukua hadi miaka 20 ijayo sasa Mtanzania piga mahesabu
Tayari Tanzania imempata raisi wa maisha Dikteta wa maisha
Katiba ya marekani inasemaje maana uchaguzi ni mwaka huu na trump anaachia lini madaraka kabla ya uchaguzi.Ni tatizo la katiba Mgombea Urais wakati huo huo ni Rais ndo madhara yake haya.
Hii barabara ya Sengerema nyehunge nkome nzela inapita kandokando mwa ziwa na hasa eneo la nkome ni swamp, hii swamp inaenda kasamwa mgoma salawe hadi mwakitolyo. ikijengwa kwa lami haitadumu.DKT. Magufuli akiwa anaendelea na kampeni za uchaguzi 2020, amepita kijiji cha Nyehunge akiwa anaelekea Geita ambapo kutoka Sengerema mpaka Nyehunge ni kilomita 46. Alisimama kuongea na wananchi waliokuwa wakimsubiri barabarani, wakati anaielezea barabara hiyo ghafla aliomba simu yake na kumpigia mtu ambae baadae alijulikana ni mkurugenzi mkuu wa TANROADS, Injinia Mfugale na mazungumzo yao yalikuwa hivi.
Magufuli: Hallo, Chief executive
Mfugale: Naam mheshimiwa Rais
Magufuli: Hujambo
Mfugale: Sijambo mheshimiwa
Magufuli: Uko wapi?
Mfugale: Niko Dar es Salaam TANESCO tunazungumzia habari ya Nyerere dam.
Magufuli: Haya, sasa mimi niko Nyehunge, kutoka Sengerema mpaka Nyehunge ni kilomita 46, hii barabara tumeshaifanyizia feasibility study na detail design, nimesimama hapa na wananchi, nataka hii barabara, mimi si ndio Rais?
Mfugale: Ndio mheshimiwa(Wananchi kicheko cha furaha)
Magufuli: Nyehunge Oyee, Unanielewa Chief? Basi hii barabara uitangaze kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami. Huu ni mwezi wa ngapi? (Mfugale: Mwezi wa tisa). Haya uandae document zote kabla ya mwezi wa 12 haujafika na kandarasi apatikane, niulize hela nitazitoa wapi. Sawa Mfugale?
Mfugale: Nimekuelewa mheshimiwa Rais
Magufuli: Umenielewa, mueleze na Waziri kwamba hayo ni maagizo yangu wala yasibadilike, Asante sana.
MWISHO WA MAONGEZI
Sasa mbona mtu kama huyu kushindwa uchaguzi ni ngumu sana, hii ni rushwa.Ni tatizo la katiba Mgombea Urais wakati huo huo ni Rais ndo madhara yake haya.
Tundu Lissu
Wewe unayeyajua hayo upo wapi? Katiba bado inamtambua kuwa yeye ni rais mpaka atakapovunja baraza la mawaziri!Hivi Mheshimiwa anajua nini maana ya kampeni za uchaguzi wa Rais? Na pia anatambua nini kinachopaswa kufanyika wakati wa shughuli za kampeni? Na kweli alisoma kwa kina na kuzielewa kanuni na maadili ya wagombea kutokana na tume ya uchaguzi?