Nyerere alikurupuka kuleta mfumo wa Muungano ambao haupo sehemu yoyote Duniani, na hakuna nchi itakayojaribu kuiga

Tuaiuvunje ila tuweke sawa..ardhi iwe sawa..mamlaka ya nchi iwe moja rais wa huko awe makamu JMT..pia iwepo equal opportunities kwa wote mana serikali iwe moja.

#MaendeleoHayanaChama
Na sisi tupewe haki sawa kule Zanzibar atoke mtu bara akagombee kule kama wao wanavyofanya huku kwetu
 
Kama bahari sio rasilimali muhimu, basi mimi naishia hapa mkuu.
 
Hakuna aliyesema uzalendo ni kukubali kwenda na Muungano Kama ulivyo.

Sijui umesoma wapi hilo andiko.

Kama kuna changamoto zozote, zitatuliwe ili kuboresha muungano lakini sio "letting go of Zanzibar."
 
Mkuu, kwanza mimi siko well informed juu ya mambo ya muungano. Niko well informed kwenye mambo ya bahari.

Kabla sijakujibu swali lako la kwanza naomba kujua manufaa ya Muungano unayotaka kuyajua ni ya mwaka huu 2022 hadi 2025 (within scope of your naked eyes) au manufaa ya Tanzania kubwa ya miaka 100, 200 au 300 ijayo ?
 
Hakuna aliyesema uzalendo ni kukubali kwenda na Muungano Kama ulivyo.

Sijui umesoma wapi hilo andiko.

Kama kuna changamoto zozote, zitatuliwe ili kuboresha muungano lakini sio "letting go of Zanzibar."
"...Kama huu muungano unakukera, nadhani unatakiwa kujifunza kuuvumilia. Bado upo sana..."

"...Mkuu, kwanza mimi siko well informed juu ya mambo ya muungano. Niko well informed kwenye mambo ya bahari..."

Kama hayo umeandika mwenyewe; Basi sawa.
Hatimaye Tumejua tatizo lilipo jikita!
 
Mkuu huwezi ku project mambo ya miaka 100 injao dunia inabadilika kwa kasi kubwa science end technology inakua kila siku na kubadili mitizamo mahitaji na mipango ya nchi na watu, wewe tuelezee faida ya huo muungano kiuchumi kwa kizazi hiki cha sasa
 
Usichokielewa hapo ni nini mkuu ?
Muungano upo sana. Hii kwako inamaanisha kwamba "upo kama ulivyo".

Ukiambiwa huu muungano upo sana, unataka anayesema hivyo awe amesomea mambo ya miungano ?

Hujui ni kwanini yule kiongozi wa upinzani visiwani (marehemu kwa sasa) alikua "hapewi" nchi licha ya "kushinda" ?

Unataka watangaze hadharani haya mambo ?

Nadhani kama viwango vya kuelewa mambo, au kuelewana kati yangu na mimi wewe viko chini kiasi hiki, basi tuishie hapa.
 
Tuko pamoja mkuu..nisamehe stress tu za maisha...ila kuna maboresho yanaenda kufanyika kwenye huu muungano..ili kila mtanzania apate usawa popote iwe visiwani au bara.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mkuu huwezi ku project mambo ya miaka 100 injao dunia inabadilika kwa kasi kubwa science end technology inakua kila siku na kubadili mitizamo mahitaji na mipango ya nchi na watu, wewe tuelezee faida ya huo muungano kiuchumi kwa kizazi hiki cha sasa
Really?
Mipango ya NCHI haitakiwi kuangalia miaka 100 mbele ?

Siwezi kuelewa hili, tutakesha bure hapa.
Au sijui kusoma umeandika mipango ya mtu au familia ?

Mipango ya nchi isiangalie miaka 100 mbele ?

Tutabishana bure, wewe ni ndugu yangu.

Uwe na asubuhi njema.
 
El Comandante baba wa taifa Mwalimu J.K Nyerere alikuwa sahihi mno kutuletea huu MUUNGANO BORA NA ADHIMU DUNIANI......

Si lazima TUIGE aina ya kuungana kwa wengine na pia si lazima wao waige kutoka kwetu....

Ulazima UNAPATIKANA wapi?!!!!

#Hasta La Victoria El Comandante JKN🙏
#Siempre El Comandante JKN🙏
 
🤣🤣🤣👍
 
Acha kutishia watu kunyamaza wasihoji..ingependeza zaidi kuziweka bayana hizo sababu..mana unaonekana unazifahamu.

Ni haki ya msingi kuhoji mana hakuna usawa katika huu muungano.

#MaendeleoHayanaChama
 
Na sisi tupewe haki sawa kule Zanzibar atoke mtu bara akagombee kule kama wao wanavyofanya huku kwetu
Utawala uwe mmoja wenye haki pande zote..za kumilia ardhi..kuchagua na kuchaguliwa na mengineyo..hii ni nchi moja hii mipaka inayowekwa inawekwa kwa faida ya nani?ili hali sote tu watanzania.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mkuu sijamaanisha hilo wewe tupe faida na mnafaa ya huo muungano kwasasa na kwa badaye tu, kama Tanganyika imefaidika na nini kwa miaka 50 ya huo muungano.....kama huwezi kutoa takwimu toa mifuano ya nchi jilani ambazo hazina muungano tunavo zi zidi kimaendeleo, ki elimu, science and technology ki usalama nk in short relate muungano hu na maendeleo ya Tz kwasasa na kwa badaye.
 
Acha kutishia watu kunyamaza wasihoji..ingependeza zaidi kuziweka bayana hizo sababu..mana unaonekana unazifahamu.

Ni haki ya msingi kuhoji mana hakuna usawa katika huu muungano.

#MaendeleoHayanaChama
Hayupo mtu anayeweza kumtisha mwingine kwa sababu kutishika ni hiari. Ukiona umetishika, ujue wewe ndiyo mwenye makosa
Sina mamlaka ya kumtisha mtu na hayupo mtu mwenye mamlaka hayo, isipokuwa tu labda katika uchhangiaji mwishowe inapelekea watu kujitisha wenyewe na kusingizia wengine
 
Utawala uwe mmoja wenye haki pande zote..za kumilia ardhi..kuchagua na kuchaguliwa na mengineyo..hii ni nchi moja hii mipaka inayowekwa inawekwa kwa faida ya nani?ili hali sote tu watanzania.

#MaendeleoHayanaChama
Kwanza Zanzibar uwe ni mkoa ndani ya Tanzania
 
Mleta mada hujui historia ndo maana unaleta uzi kama huu. Si kweli kwamba hakuna mfano popote duniani wa aina hii ya muungano. Mfano huu upo Uingereza (United Kingdom) unaojumuisha mchi za England, Scotland, Wales na Northern Ireland.
 
Nimesoma maoni ya wachangiaji na nimefahamu, kwa ufahamu wangu, kwamba watu hatujui kwamba huu muungano ni jambo la kisheria na unapaswa kushughulikiwa kisheria. Kosa kubwa lililofanywa, na ambalo linaendelea kufanywa, ni kufanya maamuzi kinyume na makubaliano ya muungano, au kwa lugha nyepesi, kutokuyafuata makubaliano ya muungano.
 
Mleta mada hujui historia ndo maana unaleta uzi kama huu. Si kweli kwamba hakuna mfano popote duniani wa aina hii ya muungano. Mfano huu upo Uingereza (United Kingdom) unaojumuisha mchi za England, Scotland, Wales na Northern Ireland.
uingereza ni nchi yenye utawala wa kifalme, rudi darasani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…