Kuita watu ng'ombe katika mijadala inaweza kukuletea picha mbaya sana mahala pengine.
Tafadhali haya yasiwe ni mazoea yako.
Ila unapojadili masuala na mimi (
Mwanamaji ), unaweza kuendelea kuniita ng'ombe au kama hautojali chagua jina jingine baya zaidi. I will take it.
Unaposema kubadilisha mfumo wa
utawara (bila shaka ulitaka kuandika
utawala,) unamaanisha nini mkuu ?
NB: Msimamo wangu wa jumla ni kwamba, kama kuna changamoto au kero yoyote ya Muungano, tunayo fursa ya kuitatua na tukasonga mbele tukiwa wamoja.
Kama kubadilisha mfumo wa utawala (japokua sijajua umemaanisha nini haswa) ni miongoni mwa vitu vitakavyoboresha zaidi Muungano wetu, basi namimi naunga mkono juhudi hizo.