Nyerere naweza kumlaumu kuwa mkoloni kwa sababu kuna sheria nyingi za kikoloni, kama za indefinite detention, na mfumo mzima wa kuifunga nchi isiwe huru, kama kupiga marufuku vyama vingi na kuzuia wapinzani wake kama kina Christopher Kasanga Tumbo na Joseph Kassela Bantu, alifanya hayo tangu awali kabisa.
Aliruhusu mfumo wa kikoloni uendelee tangu mwanzo wa utawala wake. Mambo mengi kama muungano, mabadiliko ya katiba, muelekeo wa nchi, Azimio la Arusha, mfumo wa Ujamaa na operesheni ya kuhamia Vijiji vya Ujamaa n.k, yalifanywa kikoloni koloni kwa maamuzi kutoka juu.
Ukisoma ripoti ya Justice Francis Nyalali alivyoandika mpaka sheria 40 kandamizi, utaona Nyerere alipinga sana sheria za kikoloni kabla hatujapata uhuru, lakini, tulivyopata uhuru, yeye mwenyewe akaendelea kuzitumia sheria hizo hizo za kikoloni wakati aliweza kuziondoa.
Hivyo, kwa muktadha huo, Nyerere ana makosa mengi na anaweza kuitwa kuwa aliendeleza mfumo wa kikoloni chini yake yeye mwenyewe.
Kuhusu Zanzibar, mara baada ya Nyerere kuunga mkono serikali ya Biafra iliyojitenga kutoka Shirikisho la Nigeria (kwa style ya kikoloni sana, baraza la mawaziri halikupata nafasi ya kujadili kwa kina kumpinga Nyerere katika hoja hii), kitendo kilichowashangaza wengi, kwa kuwa kilikuwa ni kinyume na muongozo wa OAU kuhusiana na "territorial integrity" na hata falsafa zake mwenyewe Nyerere zinazojulikana kama "The Nyerere Doctrine", Nyerere ilibidi ajieleze kwa jumuiya ya kimataifa, ana maana gani kuunga mkono kujitenga kwa Biafra kutoka Shirikisho la Nigeria.
Tarehe 13 Aprili 1968, Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza kuitambua serikali ya Biafra.
Nyerere aliandika makala ya Oppposite Editorial (Op-Ed) katika gazeti la The Guardian la London, akieleza kwa nini ameunga mkono Biafra kujitenga na Shirikisho la Nigeria.
Katika makala hiyo, Nyerere alielezea imani yake kwamba watu wa Biafra wameonewa sana na Nigeria na walikuwa na haki ya kuamua kujitenga. Alielezea kuwa hata Tanzania tuna muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kwamba, ikija siku watu wa Zanzibar wakakubaliana kwamba wameonewa na watu wa Tanganyika, wakaamua kujitenga, yeye Nyerere hatakuwa na jinsi bali kuwakubalia matakwa yao ya kujitenga.
Tatizo la Zanzibar si Nyerere. Tatizo la Zanzibar hata wao wenyewe Zanzibar hawajakubaliana kwamba wanataka kujitenga. Zanzibar ukienda Pemba utasikia habari moja, ukija Unguja utasikia habari tofauti.
Wazanzibari wenyewe hawajakubaliana wanataka nini.
Sasa hapo utamlaumu Nyerere vipi?
Soma
"Building A Peaceful Nation: Julius Nyerere And The Establishment of Sovereignty in Tanzania 1960-1964" cha Profesa Paul Bjerk.
Soma
"Nyerere and Africa: End Of An Era: cha Godfrey Mwakikagile.
Soma
"Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere" cha Petro D.M Bwimbo.
Soma
"Nyalali Commission Report". Justice Francis Nyalali, et al.
Soma
"International Law And The New States Of Africa" by Yilma Makonnen.
Mohamed Said
Poppy Hatonn