Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete waliwahi kuvaa Magwanda ya JWTZ walipokuwa Marais?

Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete waliwahi kuvaa Magwanda ya JWTZ walipokuwa Marais?

Rais aliyechaguliwa kidemokrasia kuvaa gwanda la kijeshi popote pale ni kuvunja misingi ya kanuni za "civilian control of the military".

Katika nchi za kidemokrasia, jeshi linamilikiwa nankuongizwa na raia. Ndiyo maana linaitwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Rais kuvaa kiraia ni symbolism ya kuonesha raia wapo juu ya jeshi, wanaliongoza jeshi.

Rais akivaa kijeshi ni symbolism ya kwamba nchi haiongozwi kiraia tena, inaongozwa kijeshi, kitu ambacho hakitakiwi katika nchi ya kidemoktasia.
Kwani majeshi yote kwenye nchi za kidemokrasia huitwa 'jeshi la wananchi?..rais wa France de Gaulle alivaa sare za jeshi,rais wa urusi Putin huvaa,kadhalika wa china
 
Wanasiasa wanaharibu heshima ya jeshi kwa kufanya nafasi zao kisiasa kuwa juu zaidi ya jeshi, leo hii dogo wa 2000 akiwa mkuu wa wilaya tu anaweza pigiwa saluti na ofisa wa juu wa jeshi, wanasiasa kuvaa nguo kijeshi huku hawajapitia mafunzo si heshima ni dharau kwa jeshi.kuwe na mipaka.
Maisha ni siasa, bila siasa maisha hayaendi, siasa ndio kila kitu, siasa haikwepeki.
 
Uniform,mwanzo nilitumia neno sare ya jeshi,hukuuliza ndiyo kitu gani,Sasa hivi nimekuuliza elimu ya uraia ya nchi gani na ikiwa huko uliko hakuna rais aliyewahi vaa sare ya jeshi, unakuja na swali sare ya jeshi ndiyo kitu gani, unataka kuanza spinning?
Huku nilipo wapi? Na kwa nini kuwe mfano?

Unaweza kuongea hoja in the abstract bila kuangukia kwenye "huko uliko"?

Kama kitu hakifai, kikiwa kinafanyika huku niliko ndiyo kitabadilika na kuwa kinafaa kwa sababu kinafanyika huku niliko?
 
Elimu ya uraia uliyodai sinayo,ni ya nchi gani?..maana huku kwetu Marais wanne walivaa sare za jeshi,rais wa china,France na urusi walivaa,hiyo elimu ya uraia inapatikana darasa la ngapi ambalo wengine hatukufanikiwa kufika?
 
Siyo tu huna elimu ya uraia, huna hata uwezo wa kufikiri kimantiki ndiyo maana umefanya logical non sequitur fallacy hapa.
 
Sasa mtu kama Samia na huo mwili wake mnene kama pipa hata ukimuambia mguu pande hajui,eti nae anajifanya kuwa mwanajeshi
 
Kumbe. modi wanaweza kuua mada na kuidukua na kumpasisha mtu wao! Nilitoa mada kama hii jana ikauawa. Nilisema majeshi kwanini yasimpe u-field marshal. mtukufu rais daktari profesa, sheha, al hajat, maulana , hurulaini, maalima, ustadha, imamati, swaibat Samia Suluhu Hassan kama vyuo vinampa udaktari wa dezo. Nilipendekeza kanisa Katoliki lianzishe mchakato wa kumtangaza mtakatifu tokana na kufanya miujiza ya kiuchumi. Pandiko hili liliuawa kinamna. Sasa naona linarudishwa kinamna.
 
Siwezi kubishana nawe kwa sababu huelewi dhana nzima za "civilian control of the military" na "justice must not only be done, it must seem to be done".

Amiri Mkuu wa jeshi si cheo cha kijeshi, hicho ni cheo cha kiraia cha rais kinachomuweka rais juu ya jeshi.

Najua hizi ni dhana ngumu kuelewa kama huna elimu ya uraia ya kutosha.
👍👌👏🤝🙏
 
Kumbe. modi wanaweza kuua mada na kuidukua na kumpasisha mtu wao! Nilitoa mada kama hii jana ikauawa. Nilisema majeshi kwanini yasimpe u-field marshal. mtukufu rais daktari profesa, sheha, al hajat, maulana , hurulaini, maalima, ustadha, imamati, swaibat Samia Suluhu Hassan kama vyuo vinampa udaktari wa dezo. Nilipendekeza kanisa Katoliki lianzishe mchakato wa kumtangaza mtakatifu tokana na kufanya miujiza ya kiuchumi. Pandiko hili liliuawa kinamna. Sasa naona linarudishwa kinamna.
🤔
 
Po
Wanasiasa wanaharibu heshima ya jeshi kwa kufanya nafasi zao kisiasa kuwa juu zaidi ya jeshi, leo hii dogo wa 2000 akiwa mkuu wa wilaya tu anaweza pigiwa saluti na ofisa wa juu wa jeshi, wanasiasa kuvaa nguo kijeshi huku hawajapitia mafunzo si heshima ni dharau kwa jeshi.kuwe na mipaka.
Pole babaa eh. Hakuna popote Dunia yote jeshi lipo juu ya wanasiasa. Wanasiasa ndio huamua chochote Cha kufanywa na jeshi kutokana na hali flani. Ukienda tofauti na wanasiasa utafutika vibaya. Kwa mfano mwaka 2003 US iliingia vitani na Iraq kwasababu za ovyo tu za bwana Bush .
Nb. Dogo wa 2000 mkuu wa wilaya kupigiwa salyuti na general si ajabu hao ni wateule wa mh Rais . Kila umuonApo ficha sura yake mvalishe uso wa Rais salimia Kwa nidhamu. Tumeelewana?
 
Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza baada ya Tanganyika kupata Uhuru na Tanganyika ilipoungana na Zanzibar kuunda Tanzania.

Mwalimu yeye ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati wa vita ya Kagera na kwenye harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika.

Ukiachilia mbali Mwalimu, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete yeye alikuwa ni mwanajeshi kabla hajawa Rais.

Lakini sina kumbukumbu kama hao maris wanne wa Tanzania enzi wakiwa ni Marais wa Tanzania, waliwahi kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao.

Kama Kuna kumbukumbu za Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao, naomba niwekewe ili nibadili mafaili kwenye kumbukumbu za mbongo yangu.
Sioni shida kwa raisi yeyote kuvaa mavazi ya jeshi lolote, kuanzia Jwtz hadi fire kwani yeye ni amiri jeshi mkuu
 
Back
Top Bottom