Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete waliwahi kuvaa Magwanda ya JWTZ walipokuwa Marais?

Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete waliwahi kuvaa Magwanda ya JWTZ walipokuwa Marais?

Siwezi kubishana nawe kwa sababu huelewi dhana nzima za "civilian control of the military" na "justice must not only be done, it must seem to be done".

Amiri Mkuu wa jeshi si cheo cha kijeshi, hicho ni cheo cha kiraia cha rais kinachomuweka rais juu ya jeshi.

Najua hizi ni dhana ngumu kuelewa kama huna elimu ya uraia ya kutosha.

Kwamba wewe ndio unaelewa zaidi kuliko watu woooooote walioshiriki kwenye tukio la Rais kuvaa uniform za Jeshi?

Wengine wooooooote hawajui hiko unachosema au

Mbona Uhuru Kenyatta alikuwa anavaaa?
 
John Pombe Magufuli na Samia Suluhu Hassan wamevaa magwanda ya jeshi wakiwa marais.
Sawa and hakuna hata mmoja amewahi serve jeshini, maybe magufuli (JKT) kidogo.

Nadhani point ya mtoa mada umeisoma
 
Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza baada ya Tanganyika kupata Uhuru na Tanganyika ilipoungana na Zanzibar kuunda Tanzania.

Mwalimu yeye ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati wa vita ya Kagera na kwenye harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika.

Ukiachilia mbali Mwalimu, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete yeye alikuwa ni mwanajeshi kabla hajawa Rais.

Lakini sina kumbukumbu kama hao maris wanne wa Tanzania enzi wakiwa ni Marais wa Tanzania, waliwahi kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao.

Kama Kuna kumbukumbu za Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao, naomba niwekewe ili nibadili mafaili kwenye kumbukumbu za mbongo yangu.
Nyerere alikuwa na sababu zote kama angetaka kuvaa magwanda ya JWTZ.
Lakini hakuwa na hizo akili ndogo!
 
Huku nilipo wapi? Na kwa nini kuwe mfano?

Unaweza kuongea hoja in the abstract bila kuangukia kwenye "huko uliko"?

Kama kitu hakifai, kikiwa kinafanyika huku niliko ndiyo kitabadilika na kuwa kinafaa kwa sababu kinafanyika huku niliko?

Ukiona kiongozi namba moja wa inchi amefanya basi ujue kiko sawa
 
Kwamba wewe ndio unaelewa zaidi kuliko watu woooooote walioshiriki kwenye tukio la Rais kuvaa uniform za Jeshi?

Wengine wooooooote hawajui hiko unachosema au

Mbona Uhuru Kenyatta alikuwa anavaaa?
Wengine wooote wanamtega bi Chura. Akiingia kingi wanazama!
Kwamba Uhuru Kenyatta alivaa si sababu za bi Chura kuvalishwa!
Mbona Katiba Mpya mmegomea wakati Kenya walishafanya!?
 
Kwamba wewe ndio unaelewa zaidi kuliko watu woooooote walioshiriki kwenye tukio la Rais kuvaa uniform za Jeshi?

Wengine wooooooote hawajui hiko unachosema au

Mbona Uhuru Kenyatta alikuwa anavaaa?
Umeshindwa kufanya fikra dhahania, unaniangalia mimi badala ya kuangalia hoja.

Hoja hapa ni "civilian control of the military". Vitabu vimeandikwa kuhusu hoja hii. Kuna artickes online kuhusu hoja hii. Hoja hii ipo kabla mimi sijazaliwa. Usi personalize kwangu hili jambo, ni kubwa zaidi yangu mimi bibafsi.

Hoja imekuwapo miaka na miaka kabla sijazaliwa, hivyo si habari yangu mimi.

Pia, Rais anaweza kuwa anaelewa lakini anafanya kinachomfaidisha yeye tu.

Anaweza kuwa anaelewa kuwa kwenye nchi ya kidemokrasia hatakiwi kuvaa kijeshi, lakini anajua watu wake wengi wajinga, hawajui hilo, wanapenda kiongozi mbabe, wanapenda avae mavazi ya kijeshi, anawapa show ya kibabe wanayoitaka.

Inawezekana kabisa ndivyo walivyofanya Magufuli na Samia. Magufuki mpaka kasema anatamani kuwa IGP, wakati akiwa Amiri Jeshi Mkuu. Yani kaona ile kazi ya urais haina ubabe kama IGP, akatamani kuwa IGP.

Kwa hiyo hapo hoja ya mimi kuelewa zaidi kuliko wote haipo.

Labda tuseme wewe ndiye mwenye uelewa mdogo tu.
 
Sawa and hakuna hata mmoja amewahi serve jeshini, maybe magufuli (JKT) kidogo.

Nadhani point ya mtoa mada umeisoma
Kikwete ali serve jeshini.

Point ni kwamba kwenye nchi za kidemokrasia rais hatakiwi kuvaa magwanda ya kijeshi.

Lakini wanavaa.

Kwa nini?

Kwa sababu wananchi wanapenda ubabe. Rais akivaa magwanda ya kijeshi anapata kick. Na marais hawana mipango ya kueleweka ya kiuchuni, wanaishia kuuza sura, hivyo, wanaishia kuvaa magwanda ya kijeshi.
 
Kwamba wewe ndio unaelewa zaidi kuliko watu woooooote walioshiriki kwenye tukio la Rais kuvaa uniform za Jeshi?

Wengine wooooooote hawajui hiko unachosema au

Mbona Uhuru Kenyatta alikuwa anavaaa?
Kosa halifanyi kosa jingine kuwa halali.
 
Siwezi kubishana nawe kwa sababu huelewi dhana nzima za "civilian control of the military" na "justice must not only be done, it must seem to be done".

Amiri Mkuu wa jeshi si cheo cha kijeshi, hicho ni cheo cha kiraia cha rais kinachomuweka rais juu ya jeshi.

Najua hizi ni dhana ngumu kuelewa kama huna elimu ya uraia ya kutosha.
Bakuli sana wewe kudadeki
 
Nyerere aliwahi kuvaa magwanda ya mgambo wakati wa Vita vya Kagera.

Ila Nyerere ni "War President" . Ali mobikize majeshi wakati wa vita hivyo huyo kidogo ana rationale ya kuvaa nguo za kijeshi kwa muktadha huo.

Wengine wote ni kick.

Wanatakiwa kujua kanuni ya "Civilian Control of the Military".
ni ulimbukeni tu,hao maraisi wanaovaa sare za jeshi hawanatofauti na wale wanaovaa joho au gauni la graduation siku ya mahafali ili wapige picha kuonyesha na wao ni wahitimu
 
Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza baada ya Tanganyika kupata Uhuru na Tanganyika ilipoungana na Zanzibar kuunda Tanzania.

Mwalimu yeye ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati wa vita ya Kagera na kwenye harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika.

Ukiachilia mbali Mwalimu, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete yeye alikuwa ni mwanajeshi kabla hajawa Rais.

Lakini sina kumbukumbu kama hao maris wanne wa Tanzania enzi wakiwa ni Marais wa Tanzania, waliwahi kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao.

Kama Kuna kumbukumbu za Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao, naomba niwekewe ili nibadili mafaili kwenye kumbukumbu za mbongo yangu.
Looks childish !
 
Kosa Moja halifanyi na kosa jingine kuwa halali.

Mpaka majenerali na wakuu wa usalama wote wameridhia then ujue hoja yako haiko hivyo unavyohisi

Rais sio mtu ambae anavaa Tu nguo kaka Sisi watu wengine

Ukiona umevaa nguo ujue imazingatiwa mambo mengi, colour of the day, hafla gani anaenda

So kama akivaa uniform ujue wahusika wakuu wameelewa hakuna shida

Me ningeona tatizo kama angeweka vyeo kwenye mabega
 
Hapana,

This is a logical fallacy.

Argument from authority.

Rais Nixon wa Marekani alifanya uhuni Wamarekani wakawa wanaenda kumuondoa akajiondoa mwenyewe, kwa sababu alikosea.

Labda wewe mtoto wa 2000 hujaijua historia hiyo.

Bosi tunaongelea Africa

Toa mifano ya Africa yetu

Hao unaowatolea mifano wanatuzidi kila kitu
 
ni ulimbukeni tu,hao maraisi wanaovaa sare za jeshi hawanatofauti na wale wanaovaa joho au gauni la graduation siku ya mahafali ili wapige picha kuonyesha na wao ni wahitimu
Watanzania na wao kwa kiasi kikubwa wanapenda show za kibabe, zile za "Nitumbueee, nisitumbueeee?" Halafu wanajibu "Tumbuaaaaa".

Sasa mtu kama Jiwe alishawajulia hawa wanapenda show za kibabe, nawatengenezea maigizo kila siku, mara makinika, mara koroshow, na magwanda ya kijeshi juu.

Basi wakimuona hivyo roho kwatuu.

Waafrika wengi wanapenda sana viongozi wababe. Na hakuna mbabe kama mwanajeshi.

Wanasiasa wao washawajulia ukishindwa kuwa mwanajeshi vaa hata gwanda tu, utawachita wengi sana wajinga.

Wananchi wangekataa huo ujinga kusingekuwa na rais anafanya hayo maigizo.
 
Mpaka majenerali na wakuu wa usalama wote wameridhia then ujue hoja yako haiko hivyo unavyohisi
Ulitaka hao majenerali wafanye nini? Hivi kule kwenye nchi Marais wanatumia jeshi kuua raia zao huwa majenerali wanaona Sawa au si sawa?

Kimantiki Rais akitaka kuvaa gwanda la jeshi Jenerali anatumia mbinu Gani kumzuia asivae?
 
Kikwete ali serve jeshini.

Point ni kwamba kwenye nchi za kidemokrasia rais hatakiwi kuvaa magwanda ya kijeshi.

Lakini wanavaa.

Kwa nini?

Kwa sababu wananchi wanapenda ubabe. Rais akivaa magwanda ya kijeshi anapata kick. Na marais hawana mipango ya kueleweka ya kiuchuni, wanaishia kuuza sura, hivyo, wanaishia kuvaa magwanda ya kijeshi.
Means waliopita they didnt need this, hawa wa sasa ndio wanaendekeza?
 
Back
Top Bottom