Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete waliwahi kuvaa Magwanda ya JWTZ walipokuwa Marais?

Means waliopita they didnt need this, hawa wa sasa ndio wanaendekeza?
Sasa kule kwenye chama kimoja, hakukuwa na internet, hakujuwa na uhuru wa vyombo vya habari, unapiga kura Nyerere na kivuli uchague rais, hapo kick inayohitajika ndogo tu.

Siku hizi kuna ushindani zaidi, kick inayohitajika kubwa zaidi.
 
Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza baada ya Tanganyika kupata Uhuru na Tanganyika ilipoungana na Zanzibar kuunda Tanzania.

Mwalimu yeye ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati wa vita ya Kagera na kwenye harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika.

Ukiachilia mbali Mwalimu, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete yeye alikuwa ni mwanajeshi kabla hajawa Rais.

Lakini sina kumbukumbu kama hao maris wanne wa Tanzania enzi wakiwa ni Marais wa Tanzania, waliwahi kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao.

Kama Kuna kumbukumbu za Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao, naomba niwekewe ili nibadili mafaili kwenye kumbukumbu za mbongo yangu.
Hizo ni nguo tu. Hata majambazi wanavaa. Sioni shida zikivaliwa na Rais yeyote.
 
Rais aliyechaguliwa kidemokrasia kuvaa gwanda la kijeshi popote pale ni kuvunja misingi ya kanuni za "civilian control of the military".

Katika nchi za kidemokrasia, jeshi linamilikiwa na kuongozwa na raia. Ndiyo maana linaitwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Rais kuvaa kiraia ni symbolism ya kuonesha raia wapo juu ya jeshi, wanaliongoza jeshi.

Rais akivaa kijeshi ni symbolism ya kwamba nchi haiongozwi kiraia tena, inaongozwa kijeshi, kitu ambacho hakitakiwi katika nchi ya kidemoktasia.
Asipoelewa nahapa tena tumpopoe namawe hakika
 
Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza baada ya Tanganyika kupata Uhuru na Tanganyika ilipoungana na Zanzibar kuunda Tanzania.

Mwalimu yeye ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati wa vita ya Kagera na kwenye harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika.

Ukiachilia mbali Mwalimu, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete yeye alikuwa ni mwanajeshi kabla hajawa Rais.

Lakini sina kumbukumbu kama hao maris wanne wa Tanzania enzi wakiwa ni Marais wa Tanzania, waliwahi kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao.

Kama Kuna kumbukumbu za Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao, naomba niwekewe ili nibadili mafaili kwenye kumbukumbu za mbongo yangu.
kila zama na kitabu chake
 
Rais aliyechaguliwa kidemokrasia kuvaa gwanda la kijeshi popote pale ni kuvunja misingi ya kanuni za "civilian control of the military".

Katika nchi za kidemokrasia, jeshi linamilikiwa na kuongozwa na raia. Ndiyo maana linaitwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Rais kuvaa kiraia ni symbolism ya kuonesha raia wapo juu ya jeshi, wanaliongoza jeshi.

Rais akivaa kijeshi ni symbolism ya kwamba nchi haiongozwi kiraia tena, inaongozwa kijeshi, kitu ambacho hakitakiwi katika nchi ya kidemokrasia.
Asante kwa elimu
 
Sasa wewe unataka nipime uwezo kwa kumuangalia mtu wa mwisho darasani badala ya kumuangalia anayeongoza darasani?

Haya,

Afrika Kusini Rais Thabo Mbeki aliondolewa madarakani.

Inaonekana hujui historia.

Sisi tuna Aina yetu ya kuongoza mambo yetu

Sheria inaweza kuchange anytime Kwa ajili ya kuweka Jambo flan lifanyike

Nambie inch gani umewahi kuona kiongozi anaapushwa kuwa waziri kwanza then ndio anaanipishwa kuwa mbunge?

So Sisi tuna mambo yetu kivyetu vyeti

Katiba yetu inaruhusu watu kuandamana je watu wanaweza kukubaliwa kuandamana ?

That's why nakwambia usitoe mifano Kwa inchi ambazo hazipo kama inchi yetu
 
Ulitaka hao majenerali wafanye nini? Hivi kule kwenye nchi Marais wanatumia jeshi kuua raia zao huwa majenerali wanaona Sawa au si sawa?

Kimantiki Rais akitaka kuvaa gwanda la jeshi Jenerali anatumia mbinu Gani kumzuia asivae?

Generali anaweza kusema hapana na Rais akatii
 
Sisi tuna Aina yetu ya kuongoza mambo yetu

Sheria inaweza kuchange anytime Kwa ajili ya kuweka Jambo flan lifanyike

Nambie inch gani umewahi kuona kiongozi anaapushwa kuwa waziri kwanza then ndio anaanipishwa kuwa mbunge?

So Sisi tuna mambo yetu kivyetu vyeti

Katiba yetu inaruhusu watu kuandamana je watu wanaweza kukubaliwa kuandamana ?

That's why nakwambia usitoe mifano Kwa inchi ambazo hazipo kama inchi yetu

This logical fallacy is called "argument from tradition".

Yani unapinga mabadiliko kwa kusema "huu ndio utamaduni wetu" hata kama utamaduni ni mbaya.

Suala si sisi tumezoea nini, suala ni hivyo tulivyozoea ni vizuri au vibaya? Kama ni vibaya, tunaweza kubadilisha au hatuwezi kubadilisha?

Kama unaongelea sisi tumezoea hivi tu, basi hakuna hata haja ya kujadili mambo JF ili kujiongeza, unajadili nini wakati ushasema sisi tumezoea hivyo?
 
Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza baada ya Tanganyika kupata Uhuru na Tanganyika ilipoungana na Zanzibar kuunda Tanzania.

Mwalimu yeye ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati wa vita ya Kagera na kwenye harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika.

Ukiachilia mbali Mwalimu, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete yeye alikuwa ni mwanajeshi kabla hajawa Rais.

Lakini sina kumbukumbu kama hao maris wanne wa Tanzania enzi wakiwa ni Marais wa Tanzania, waliwahi kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao.

Kama Kuna kumbukumbu za Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao, naomba niwekewe ili nibadili mafaili kwenye kumbukumbu za mbongo yangu.
Huo uvaaji ulianzishwa na Magufuli. Sijui sababu ilikuwa nini. Kagame na Museven ndio wavaaji wakubwa wa sare hizo na wao wanajulikana walitawala mwanzo kwa mapinduzi.
 
This logical fallacy is called "argument from tradition".

Yani unapinga mabadiliko kwa kusema "huu ndio utamaduni wetu" hata kama utamaduni ni mbaya.

Suala si sisi tumezoea nini, suala ni hivyo tulivyozoea ni vizuri au vibaya? Kama ni vibaya, tunaweza kubadilisha au hatuwezi kubadilisha?

Kama unaongelea sisi tumezoea hivi tu, basi hakuna hata haja ya kujadili mambo JF ili kujiongeza, unajadili nini wakati ushasema sisi tumezoea hivyo?

Mimi ningekuelewa kama hoja yako ingekuwa Rais amevaa cheo cha kijeshi na hajawahi kuwa mwanajeshi

Ila kuvaa uniform kwenye tukio la kijeshi shida Iko wapi?

Angekuwa anavaa offisini au kwenye ziara za kikazi hapo Sawa

So Rais akivaa jezi kwenye uzinduzi wa michezo ni tatizo?
 
Kwanza kabisa unafananisha vitu visivyofananishika. Unafananisha nguo za michezo na nguo za jeshi.

Inaonekana huelewi historia ndefu iliyopelekea kutenganisha jeshi na siasa ambayo haipo kwenye kutenganisha michezo na siasa.

Na kwa kukosa kuelewa historia hiyo, unakosa muktadha wa kwa nini principle ya "civilian control of the military" ni muhimu.

Na kwa kweli, mtu ambaye haelewi principle ya "civikian control of the military", ambayo ilipelekea wanajeshi waliokuwa katika siasa kina Makamba Sr, Kikwete, marehemu Ditopile Mzuzuri, marehemu Moses Nnauye, George Mkuchika etc, wapewe ultimatum ya kuchagua kuendelea na jeshi waache siasa ama waingie kwenye siasa waachane na jeshi.

Kama huelewi kanuni ya "civilian control of the military" na huelewi umuhimu wa symbolism ya mavazi katika uongozi, huwezi kunielewa.

Na inaoneoana dhana hizi huzielewi.

Hivyo, ni vigumu sana kunielewa.

Ila Benjamin Mkapa muandishi msomi alielewa dhana hizi, ndiyo maana hutapata picha ya Benjamin Mkapa kavaa nguo za kijeshi kama rais.

Kikwete aliyekuwa mwanajeshi na kuondoka jeshini ili aendelee kwenye siasa alielewa dhana hiii. Ndiyo maana sijaona picha ya Kikwete amevaa nguo za jeshi akiwa rais.

Mwalimu Ali Hassan Mwinyi alielewa hoja hii. Ndiyo maana hakuna picha yake akiwa kavaa magwanda ya kijeshi akiwa rais.

Mwalimu Nyerere mwenyewe,Rais pekee wa Vita Tanzania, hata wakati wa vita, aliishia kuvaa nguo za mgambo tu, akielewa kuwa mgambo ni militia si military.

Ni Magufuli na Samia tu waliotuletea ulimbukeni kwenye suala hili.
 
Back
Top Bottom