Brother, amevaa mara ngapi?
Amevaa kwenye matukio gani?
Mbona mnatake Jambo la kawaida kuwa big ishu?
Possibly Sheria zimechange bila ww kujua so ulizia zaidi Kwa wahusika
Hii ishu ingekuwa ni hivyo unavyosema sidhani kama Rais angevaa
Mpaka sasa hujaelewa somo.
Jambo baya ni baya tu, mara ngapi si hoja.
Kama kuvaa magwanda ya jeshi kwa kiongozi w a kidemokrasia ni jambo baya, litakuwa baya tu bila kujali kavaa wapi.
Hilo jambo unaliona la kawaida kwa sababu wewe huelewi umuhimu wa "civilian control of the military". Unaonekana kabisa kuwa hili jambo ndiyo unalisikia leo na hata hutaki kulisoma.
Nina shaka hata kama unaelewa Kiingereza, maana nimekuwekea wiki ndefu imeelezea hata hujaigusia kabisa. Yani hata kuangalia picha sijui kama umeangalia, maana ungeangalia ungeona viongozi wa kisiasa wa kiraia wamevaa suti na wanajeshi wana nguo za kijeshi.
Wanajeshi na magwanda yao wanawapigia saluti viongozi wa kiraia wenye suti.
Unaoneshwa "civilian control of the military", wenye suti ndio wanaowa control waliovaa kijeshi.
Hata kama hujui kusoma, picha nazo huoni?
Sasa haya mambo mengine katika Kiswahili hayajaandikwa sana, kuelewana inabidi ujue Kiingereza angalau kidogo.
Ukishaanza na "Possibly sheria zimechange..." hapo unalazimisha kitu ambacho huna uhakika nacho. Sheria gani zimechange? Lini? Ziweke hapa.
Tatizo umemuweka rais juu sana kama hawezi kukosea kwa bahati mbaya au makusudi, wakati rais akiwaona raia wajinga kama wewe wako wengi wanamuamini sana ana abuse power zake tu.
Mnaamini sana viongozi. Hii ni sababu kubwa ya umasikini Afrika.
Jamii inayoamini sana na kuachia sana viongozi wafanye wanavyotaka ni jamii isiyo na accountability.
Jamii isiyo na accountability ni vigumu kuendelea.