Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete waliwahi kuvaa Magwanda ya JWTZ walipokuwa Marais?

Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete waliwahi kuvaa Magwanda ya JWTZ walipokuwa Marais?

Katiba ya JMT inasema wazi Rais halazimiki kuchukua ushauri wa mtu yeyote.

Maana ya kutii unaelewa? Unaposema Rais amtii Jenerali unaelewa unamaanisha nini?

Jenerali amekula kiapo cha utii Kwa Rais ila Rais hawezi kumtii Jenerali. Haya mambo yapo wazi Sana nashangaa unarefusha hoja.

Ila anapata ushauri
Ni Sawa na katiba inaruhusu watu kuandamana lakini still watu wakiandamana wanapigwa
 
Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza baada ya Tanganyika kupata Uhuru na Tanganyika ilipoungana na Zanzibar kuunda Tanzania.

Mwalimu yeye ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati wa vita ya Kagera na kwenye harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika.

Ukiachilia mbali Mwalimu, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete yeye alikuwa ni mwanajeshi kabla hajawa Rais.

Lakini sina kumbukumbu kama hao maris wanne wa Tanzania enzi wakiwa ni Marais wa Tanzania, waliwahi kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao.

Kama Kuna kumbukumbu za Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao, naomba niwekewe ili nibadili mafaili kwenye kumbukumbu za mbongo yangu.
Hawakuvaa kwa sababu hawakuwa wajinga kama hao wengine.
 
Umesema kitu cha kufikirisha sana. Inawezekana huu ndio MSIBA mkuu wa kihistoria wa Waafrika (historical tragedy of this continent).

Maelezo mengi ya kihistoria niliyosoma yanaonyesha wababe walipokuwa wakija Afrika kusaka watumwa, rasilimali na makoloni, waafrika badala ya kuungana kupambana kuwaondoa, walikuwa wakizungukana na kujikomba kwa wababe hao na kuwasaidia kuchukua ndugu zao utumwani pamoja na kuwabebea yote waliyotaka hadi kwenye merikebu zao.

Wakoloni waliwezeshwa sana na baadhi ya machifu na watu wao kujitwalia makoloni na kuwatumikisha maelfu ya Waafrika kitumwa katika shughuli za ujenzi, kilimo, uaskari, n.k. Bila machawa hao wa Kiafrika, wakoloni na wafanya biashara ya watumwa wangekwama sana katika harakati zao.

Hadi leo hii somo la demokrasia na haki za binadamu linashindikana kabisa Afrika. Wengi wanadai ni utamaduni wa Magharibi, kwamba ni janja ya kutaka kuiba rasilimali za Afrika! HAWAUTAKI. Wanachotaka ni kiongozi imara, mwenye maono na mwenye kujali wanyonge! Atapatikanaje? (kwa maombi na deep state!) Na uchawa kwa viongozi wababe ndio mtindo mkuu wa maisha na mafanikio kwa Waafrika wengi chini ya jangwa la Sahara. Sad.
Waafrika wengi wa aina hii wamechanganyikiwa.

Nilikuwa sehemu namsikiliza mtu anadai uhuru na demokrasia Tanzania, anaponda uongozi wetu, anataka katiba mpya. Anataka utawala wa sheria.

Muda wote huo kaweka avatar ya Captain Ibrahim Traore, mtawala wa kijeshi wa Burkina Faso aliyechukua madaraka kwa mtutu wa bunduki kwa makandokando mengi.

Contradiction.
 
Brother, amevaa mara ngapi?

Amevaa kwenye matukio gani?

Mbona mnatake Jambo la kawaida kuwa big ishu?

Possibly Sheria zimechange bila ww kujua so ulizia zaidi Kwa wahusika

Hii ishu ingekuwa ni hivyo unavyosema sidhani kama Rais angevaa
Mpaka sasa hujaelewa somo.

Jambo baya ni baya tu, mara ngapi si hoja.

Kama kuvaa magwanda ya jeshi kwa kiongozi w a kidemokrasia ni jambo baya, litakuwa baya tu bila kujali kavaa wapi.

Hilo jambo unaliona la kawaida kwa sababu wewe huelewi umuhimu wa "civilian control of the military". Unaonekana kabisa kuwa hili jambo ndiyo unalisikia leo na hata hutaki kulisoma.

Nina shaka hata kama unaelewa Kiingereza, maana nimekuwekea wiki ndefu imeelezea hata hujaigusia kabisa. Yani hata kuangalia picha sijui kama umeangalia, maana ungeangalia ungeona viongozi wa kisiasa wa kiraia wamevaa suti na wanajeshi wana nguo za kijeshi.

Wanajeshi na magwanda yao wanawapigia saluti viongozi wa kiraia wenye suti.

Unaoneshwa "civilian control of the military", wenye suti ndio wanaowa control waliovaa kijeshi.

Hata kama hujui kusoma, picha nazo huoni?

Sasa haya mambo mengine katika Kiswahili hayajaandikwa sana, kuelewana inabidi ujue Kiingereza angalau kidogo.

Ukishaanza na "Possibly sheria zimechange..." hapo unalazimisha kitu ambacho huna uhakika nacho. Sheria gani zimechange? Lini? Ziweke hapa.

Tatizo umemuweka rais juu sana kama hawezi kukosea kwa bahati mbaya au makusudi, wakati rais akiwaona raia wajinga kama wewe wako wengi wanamuamini sana ana abuse power zake tu.

Mnaamini sana viongozi. Hii ni sababu kubwa ya umasikini Afrika.

Jamii inayoamini sana na kuachia sana viongozi wafanye wanavyotaka ni jamii isiyo na accountability.

Jamii isiyo na accountability ni vigumu kuendelea.
 
Nyerere aliwahi kuvaa wakati gani? Mwalimu wakati anatenbea Kwa miguu toka Butiama mpaka Mwanza alivaa nguo kama za mgambo.

Lakini pia hakuvaa kuonesha kuwa yeye ni Amiri Jeshi Mkuu.

Huu Sasa ni uzushi mwingine. Amiri Jeshi Mkuu si cheo cha kijeshi kama alivyosema Kiranga .

Sasa Amiri Jeshi Mkuu alivaaje tena sare za jeshi zenye cheo cha Kanali? Unaelewa kuvaa huko kungefanya awapigie saluti Mabrigedia na majenerali wa jeshi?

Hizi hadithi ishieni nazo kwenye vijiwe vya stori mitaani.
Mbona Nyerere hajawai kuvaa Sare za chama wakati wengine wanavaa?
 
Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza baada ya Tanganyika kupata Uhuru na Tanganyika ilipoungana na Zanzibar kuunda Tanzania.

Mwalimu yeye ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati wa vita ya Kagera na kwenye harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika.

Ukiachilia mbali Mwalimu, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete yeye alikuwa ni mwanajeshi kabla hajawa Rais.

Lakini sina kumbukumbu kama hao maris wanne wa Tanzania enzi wakiwa ni Marais wa Tanzania, waliwahi kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao.

Kama Kuna kumbukumbu za Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao, naomba niwekewe ili nibadili mafaili kwenye kumbukumbu za mbongo yangu.
Nyerere yeye alikuwa anavaa nguo za mgambo, Kikwete yeye amehudumia jeshi kwa mda mrefu sana kwahiyo magwanda alivaa sana akiwa jeshini, mkapa ni mwanadiplomasia wanadiplomasia siyo watu wa mikiki na vita. Nimemaliza
 
Ulimbukeni ulioasisiwa na mzee wa chato kutafutia kiki.
Jiwe alikuwa ni Jiwe haswa alipaswa kuvaa combat. Amiri Jeshi Mkuu anatakiwa kuvaa combat. Ambao hawakuvaa ndio "malimbukeni"

Namkumbuka sana Jiwe. Rais anatakiwa kuwa kichaa kichaa tu asiyetabirika leo ataongea nini. Sio Rais mnajua kabisa kila siku speech zake ni kulia lia tu kama wananchi wake

Jiwe ilibaki kidogo tu angeendelea kuwa hai kuna siku angemwambia mtu Kmmk mbele ya camera
 
Allen Kilewella Nilikwambia. Ushahidi tunaupata hapahapa 🤣🤣🤣.
 
Nyerere aliwahi kuvaa magwanda ya mgambo wakati wa Vita vya Kagera.

Ila Nyerere ni "War President" . Ali mobikize majeshi wakati wa vita hivyo huyo kidogo ana rationale ya kuvaa nguo za kijeshi kwa muktadha huo.

Wengine wote ni kick.

Wanatakiwa kujua kanuni ya "Civilian Control of the Military".
Nyerere alikuwa mtu mmoja mwenye busara na hekima sana. Akielewa kwamba kulikuwa na askari wa mgambo walipelekwa vitani, hakutaka kuvaa sare za jeshi zenye nyota na madoido kama amri jeshi mkuu. Aliwaambia wampe magwanda wanayovaa askari wa mgambo uraiani, akajifanya yuko chini hata ya askari wa mgambo walio vitani. Sio wenzangu na mie hawa wanaopenda kujimwambafy na sare za jeshi hata kupiga mguu upande hawajui!
 
Jiwe alikuwa ni Jiwe haswa alipaswa kuvaa combat. Amiri Jeshi Mkuu anatakiwa kuvaa combat. Ambao hawakuvaa ndio "malimbukeni"

Namkumbuka sana Jiwe. Rais anatakiwa kuwa kichaa kichaa tu asiyetabirika leo ataongea nini. Sio Rais mnajua kabisa kila siku speech zake ni kulia lia tu kama wananchi wake

Jiwe ilibaki kidogo tu angeendelea kuwa hai kuna siku angemwambia mtu Kmmk mbele ya camera
Kuna siku angemwambia mtu ile kavu kavu sio
hahahhaah ahahhah
 
Mpaka sasa hujaelewa somo.

Jambo baya ni baya tu, mara ngapi si hoja.

Kama kuvaa magwanda ya jeshi kwa kiongozi w a kidemokrasia ni jambo baya, litakuwa baya tu bila kujali kavaa wapi.

Hilo jambo unaliona la kawaida kwa sababu wewe huelewi umuhimu wa "civilian control of the military". Unaonekana kabisa kuwa hili jambo ndiyo unalisikia leo na hata hutaki kulisoma.

Nina shaka hata kama unaelewa Kiingereza, maana nimekuwekea wiki ndefu imeelezea hata hujaigusia kabisa. Yani hata kuangalia picha sijui kama umeangalia, maana ungeangalia ungeona viongozi wa kisiasa wa kiraia wamevaa suti na wanajeshi wana nguo za kijeshi.

Wanajeshi na magwanda yao wanawapigia saluti viongozi wa kiraia wenye suti.

Unaoneshwa "civilian control of the military", wenye suti ndio wanaowa control waliovaa kijeshi.

Hata kama hujui kusoma, picha nazo huoni?

Sasa haya mambo mengine katika Kiswahili hayajaandikwa sana, kuelewana inabidi ujue Kiingereza angalau kidogo.

Ukishaanza na "Possibly sheria zimechange..." hapo unalazimisha kitu ambacho huna uhakika nacho. Sheria gani zimechange? Lini? Ziweke hapa.

Tatizo umemuweka rais juu sana kama hawezi kukosea kwa bahati mbaya au makusudi, wakati rais akiwaona raia wajinga kama wewe wako wengi wanamuamini sana ana abuse power zake tu.

Mnaamini sana viongozi. Hii ni sababu kubwa ya umasikini Afrika.

Jamii inayoamini sana na kuachia sana viongozi wafanye wanavyotaka ni jamii isiyo na accountability.

Jamii isiyo na accountability ni vigumu kuendelea.

Katiba inasemaje kuhusu Rais kuvaa nguo za Jeshi kwenye matukio ya kijeshi?
 
Jibu swali katiba inasemaje?

Je Rais kavunja katiba kuvaa uniform za Jeshi kwenye tukio la jeshi?
Inaonekana huelewi hata katiba ni nini.

Ndiyo maana unauliza swali hili.

Katiba ni nini?
 
Siwezi kubishana nawe kwa sababu huelewi dhana nzima za "civilian control of the military" na "justice must not only be done, it must seem to be done".

Amiri Mkuu wa jeshi si cheo cha kijeshi, hicho ni cheo cha kiraia cha rais kinachomuweka rais juu ya jeshi.

Najua hizi ni dhana ngumu kuelewa kama huna elimu ya uraia ya kutosha.
Huyo kichwa ngumu we mwambie tu "Amiri jeshi" inamaanisha Uraia uliochangamka, hapo atakuelewa
 
Huyo kichwa ngumu we mwambie tu "Amiri jeshi" inamaanisha Uraia uliochangamka, hapo atakuelewa
Hawa wengine wana ubishi wa tabia.

Ushakutana na mtu unafikiri ukimpa hoja za kimantiki atakuelewa, lakini kila unavyompa hoja ndivyo anavyozidi kukutungia hadithi za kukubishia tu?

Kuna mmoja nimempa muktadha, mantiki, historia, falsafa kedekede, ananijibu "Inawezekana sheria zimebadilishwa, rais hawezi kukosea".

Nikasema huyu ndezi, si bure.

Unasema hapa inawezekana napiga kelele na mtoto wa miaka 14, tena mtoto mjinga.

Mzee mzima unajipinda kufungua Clausewitz na Clark (just to stay in C) halafu kumbe mwenzako hata Kiingereza hajui. Unarudia rudia tu "civilian control of the military" kumbe mwenzako hata kuitamka tu hawezi!
 
Back
Top Bottom