1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
Rais aliyechaguliwa kidemokrasia kuvaa gwanda la kijeshi popote pale ni kuvunja misingi ya kanuni za "civilian control of the military".
Katika nchi za kidemokrasia, jeshi linamilikiwa na kuongozwa na raia. Ndiyo maana linaitwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
Rais kuvaa kiraia ni symbolism ya kuonesha raia wapo juu ya jeshi, wanaliongoza jeshi.
Rais akivaa kijeshi ni symbolism ya kwamba nchi haiongozwi kiraia tena, inaongozwa kijeshi, kitu ambacho hakitakiwi katika nchi ya kidemokrasia.
Una akili kubwa sana.
Kwa Muda mrefu sasa CCM wanaongoza nchi kijeshi .
Hata wanayoyafanya kwenye uchaguzi ni mapinduzi ya kiraia kutumia majeshi .
Nilipoona tu Dr.Samia akavaa magwanda ya Kijeshi kinyume kabisa na utaratibu wa tawala za kidemokrasia nikagundua kuwa yule mama ndani yake kuna udikteta mkubwa sana na anatamani kuongoza kwa kutumia mtutu wa Bastola.
Rais wa Marekani ni kama raisi wa Dunia. Taifa lenye jeshi kubwa na la kisasa kabisa duniani lakini hawezi kuvaa sare za kijeshi ili hali yeye ni Raia .
Rais anawakilisha wananchi kuongoza nchi na taasisi zote za serikali ikiwemo Jeshi . Kwa hiyo yule ni raia namba moja na sio mwanajeshi . Mwanajeshi namba moja ni CDF. Ndio maana Jeshi ni serikali mbadala muda wote . Kwa protocol za kijeshi kila cheo kina heshima yake . Na cheo kinavalishwa kwenye unifomu . Asiye na cheo kwenye unifomu basi atakua ndiye mdogo kabisa kwa cheo . Sasa wale madikteta uchwara sijui wanavaa vyeo gani kwenye unifomu zao ili wawe juu ya 4 star General.!!
Hii nchi, CCM kuna siku watampitisha kwa kishindo mgonjwa wa ubongo .Atavaa vip(as then it was) kichwani😂😂😂😂