Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete waliwahi kuvaa Magwanda ya JWTZ walipokuwa Marais?

Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete waliwahi kuvaa Magwanda ya JWTZ walipokuwa Marais?

Huo uvaaji ulianzishwa na Magufuli. Sijui sababu ilikuwa nini. Kagame na Museven ndio wavaaji wakubwa wa sare hizo na wao wanajulikana walitawala mwanzo kwa mapinduzi.
Putin na xi Jin ping huvaa
 
Kwanza kabisa unafananisha vitu visivyofananishika. Unafananisha nguo za michezo na nguo za jeshi.

Inaonekana huelewi historia ndefu iliyopelekea kutenganisha jeshi na siasa ambayo haipo kwenye kutenganisha michezo na siasa.

Na kwa kukosa kuelewa historia hiyo, unakosa muktadha wa kwa nini principle ya "civilian control of the military" ni muhimu.

Na kwa kweli, mtu ambaye haelewi principle ya "civikian control of the military", ambayo ilipelekea wanajeshi waliokuwa katika siasa kina Makamba Sr, Kikwete, marehemu Ditopile Mzuzuri, marehemu Moses Nnauye, George Mkuchika etc, wapewe ultimatum ya kuchagua kuendelea na jeshi waache siasa ama waingie kwenye siasa waachane na jeshi.

Kama huelewi kanuni ya "civilian control of the military" na huelewi umuhimu wa symbolism ya mavazi katika uongozi, huwezi kunielewa.

Na inaoneoana dhana hizi huzielewi.

Hivyo, ni vigumu sana kunielewa.

Ila Benjamin Mkapa muandishi msomi alielewa dhana hizi, ndiyo maana hutapata picha ya Benjamin Mkapa kavaa nguo za kijeshi kama rais.

Kikwete aliyekuwa mwanajeshi na kuondoka jeshini ili aendelee kwenye siasa alielewa dhana hiii. Ndiyo maana sijaona picha ya Kikwete amevaa nguo za jeshi akiwa rais.

Mwalimu Ali Hassan Mwinyi alielewa hoja hii. Ndiyo maana hakuna picha yake akiwa kavaa magwanda ya kijeshi akiwa rais.

Mwalimu Nyerere mwenyewe,Rais pekee wa Vita Tanzania, hata wakati wa vita, aliishia kuvaa nguo za mgambo tu, akielewa kuwa mgambo ni militia si military.

Ni Magufuli na Samia tu waliotuletea ulimbukeni kwenye suala hili.

Zile nguo zimetoka jeshini
So kama wao ndio wamempa then wanajua hakuna shida ya Rais kuvaa

Otherwise wasingekubali avae kama kungekuwa na shida
 
Rais anapata wapi ushauri wa mambo ya jeshi? And why anapata ushauri why asiamue tu
Katiba ya JMT inasema wazi Rais halazimiki kuchukua ushauri wa mtu yeyote.

Maana ya kutii unaelewa? Unaposema Rais amtii Jenerali unaelewa unamaanisha nini?

Jenerali amekula kiapo cha utii Kwa Rais ila Rais hawezi kumtii Jenerali. Haya mambo yapo wazi Sana nashangaa unarefusha hoja.
 
Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza baada ya Tanganyika kupata Uhuru na Tanganyika ilipoungana na Zanzibar kuunda Tanzania.

Mwalimu yeye ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati wa vita ya Kagera na kwenye harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika.

Ukiachilia mbali Mwalimu, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete yeye alikuwa ni mwanajeshi kabla hajawa Rais.

Lakini sina kumbukumbu kama hao maris wanne wa Tanzania enzi wakiwa ni Marais wa Tanzania, waliwahi kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao.

Kama Kuna kumbukumbu za Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao, naomba niwekewe ili nibadili mafaili kwenye kumbukumbu za mbongo yangu.
Huna akili,wakivaa kina Samia wanavunja sheria gani kwenye katiba? Kwan amir jeshi mkuu ina maana gani? au unahisi maana yake ni mkuu wa vyama vya siasa
 
Mwalimu Nyerere ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza baada ya Tanganyika kupata Uhuru na Tanganyika ilipoungana na Zanzibar kuunda Tanzania.

Mwalimu yeye ndiye aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati wa vita ya Kagera na kwenye harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika.

Ukiachilia mbali Mwalimu, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete yeye alikuwa ni mwanajeshi kabla hajawa Rais.

Lakini sina kumbukumbu kama hao maris wanne wa Tanzania enzi wakiwa ni Marais wa Tanzania, waliwahi kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao.

Kama Kuna kumbukumbu za Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete kuvaa sare za JWTZ kuonesha uamiri jeshi Mkuu wao, naomba niwekewe ili nibadili mafaili kwenye kumbukumbu za mbongo yangu.
Japo sio muhimu na wala haina maana yoyote, sijawahi kumuona hayati J.K.Nyerere katika gwanda za kijani za CCM na ndie alikua mwenyekiti wa CCM taifa 🐒
 
Watanzania na wao kwa kiasi kikubwa wanapenda show za kibabe, zile za "Nitumbueee, nisitumbueeee?" Halafu wanajibu "Tumbuaaaaa".

Sasa mtu kama Jiwe alishawajulia hawa wanapenda show za kibabe, nawatengenezea maigizo kila siku, mara makinika, mara koroshow, na magwanda ya kijeshi juu.

Basi wakimuona hivyo roho kwatuu.

Waafrika wengi wanapenda sana viongozi wababe. Na hakuna mbabe kama mwanajeshi.

Wanasiasa wao washawajulia ukishindwa kuwa mwanajeshi vaa hata gwanda tu, utawachita wengi sana wajinga.

Wananchi wangekataa huo ujinga kusingekuwa na rais anafanya hayo maigizo.
Umesema kitu cha kufikirisha sana. Inawezekana huu ndio MSIBA mkuu wa kihistoria wa Waafrika (historical tragedy of this continent).

Maelezo mengi ya kihistoria niliyosoma yanaonyesha wababe walipokuwa wakija Afrika kusaka watumwa, rasilimali na makoloni, waafrika badala ya kuungana kupambana kuwaondoa, walikuwa wakizungukana na kujikomba kwa wababe hao na kuwasaidia kuchukua ndugu zao utumwani pamoja na kuwabebea yote waliyotaka hadi kwenye merikebu zao.

Wakoloni waliwezeshwa sana na baadhi ya machifu na watu wao kujitwalia makoloni na kuwatumikisha maelfu ya Waafrika kitumwa katika shughuli za ujenzi, kilimo, uaskari, n.k. Bila machawa hao wa Kiafrika, wakoloni na wafanya biashara ya watumwa wangekwama sana katika harakati zao.

Hadi leo hii somo la demokrasia na haki za binadamu linashindikana kabisa Afrika. Wengi wanadai ni utamaduni wa Magharibi, kwamba ni janja ya kutaka kuiba rasilimali za Afrika! HAWAUTAKI. Wanachotaka ni kiongozi imara, mwenye maono na mwenye kujali wanyonge! Atapatikanaje? (kwa maombi na deep state!) Na uchawa kwa viongozi wababe ndio mtindo mkuu wa maisha na mafanikio kwa Waafrika wengi chini ya jangwa la Sahara. Sad.
 
Kumbe. modi wanaweza kuua mada na kuidukua na kumpasisha mtu wao! Nilitoa mada kama hii jana ikauawa. Nilisema majeshi kwanini yasimpe u-field marshal. mtukufu rais daktari profesa, sheha, al hajat, maulana , hurulaini, maalima, ustadha, imamati, swaibat Samia Suluhu Hassan kama vyuo vinampa udaktari wa dezo. Nilipendekeza kanisa Katoliki lianzishe mchakato wa kumtangaza mtakatifu tokana na kufanya miujiza ya kiuchumi. Pandiko hili liliuawa kinamna. Sasa naona linarudishwa kinamna.
lipandishe tena mkuu
 
Zile nguo zimetoka jeshini
So kama wao ndio wamempa then wanajua hakuna shida ya Rais kuvaa

Otherwise wasingekubali avae kama kungekuwa na shida
Bado hujaelewa somo na at this point nafikiri labda si tu hujaelews somo, labda huna uwezo wa kuelewa somo.

Nguo kutoka jeshini si hoja.

Kwa sababu kinachofanya rais wa kidemokrasia kuvaa nguo za jeshi kuwa jambo baya si nguo zinatoka wapi.

Kinachofanya rais wa kidemokrasia kuvaa nguo za jeshi kuwa kitu kibaya ni kwamba rais analeta muonekano wa nchi kuongozwa kijeshi wakati nchi inatakiwa kuonekana inaongozwa kiraia.

Civilian control of the military, amiri jeshi mkuu anatakiwa kuvaa nguo za kiraia ili ionekane nchi inaongozwa kiraia, jeshi linapewa amri na raia.

Rais akivaa magwanda ya jeshi inaonekana kuwa wanajeshi ndio wanaongoza nchi. Nchi haipo katika uongozi wa kiraia, ipo katika uongozi wa kijeshi.

Nina shaka kama unaweza kuelewa.

Brother, amevaa mara ngapi?

Amevaa kwenye matukio gani?

Mbona mnatake Jambo la kawaida kuwa big ishu?

Possibly Sheria zimechange bila ww kujua so ulizia zaidi Kwa wahusika

Hii ishu ingekuwa ni hivyo unavyosema sidhani kama Rais angevaa
 
Back
Top Bottom