Nyerere ndiye aliyeshauri umri wa kuanza shule uwe miaka 7

Nyerere ndiye aliyeshauri umri wa kuanza shule uwe miaka 7

Kwa wakati huo alikuwa sahihi kwa kiasi fulani. Alisema kuwa ni asilimia 13 tu ya wanafunzi ndiyo wanaweza kwenda sekondari. Hivyo ni bora elimu yetu iiangalie jinsi ya kuwatumia hawa 87%
Badala ya kuongeza idadi ya madarasa na walimu anawaambia wacheleweshwe kusoma ndiyo kwa wewe yupo sahihi? Daah!

Alikuwa anajenga utumwa mambo leo?
 
Badala ya kuongeza idadi ya madarasa na walimu anawaambia wacheleweshwe kusoma ndiyo kwa wewe yupo sahihi? Daah!

Alikuwa anajenga utumwa mambo leo?
Kwenye hicho kitabu anasema kuwa bajeti ya elimu ilikuwa tayari kubwa kupita kiasi, (kama milioni miamoja na kadhaa hivi.) Hivyo alisema haiwezekani kuongeza bajeti. Tena ingetakiwa kupungua. Kwahiyo kwake suala la kuongeza madarasa lisingewezekana.
 
Bajeti ya kupiganisha nchi vita alikuwa nayo, bajeti ya kupeleka misaada Biafra alikuwa nayo, bajeti ya kupigana vita zisizokuwa zake alikuwa nazo, bajeti ya elimu ndiyo kakosa?

Maajabu hayo.
 
Aliwasaidia watoto wengi kufaidi usingizi mtamu. wa siku hizi miaka miwili mitatu wanaamshwa saa kumi kujiandaa kwenda shule. Ndo maana vingi havina adabu vimeanza kupata stress mapema mno
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Badala ya kuongeza idadi ya madarasa na walimu anawaambia wacheleweshwe kusoma ndiyo kwa wewe yupo sahihi? Daah!

Alikuwa anajenga utumwa mambo leo?
Wewe akili zimo kweli?? Unaongelea kuongeza madarasa miaka ya 60 ku cover asilimia 87 wakati mpaka sasa miaka 60 baadae bado tumeshindwa kucover watoto wote??plan ya muda mfupi ilikuwa ni hiyo huku tukisubiri tufikie uwezo wa kuaccomodate watoto wote ambao angalu sasa miaka 60 tunakaribia kufNikiwa
 
Siku hizi hata. Kitoto Cha miaka mitatu kipo darasa la 1
 
Kwenye kitabu elimu ya kujitegemea Mwalimu Nyerere alitoa hoja nyingi juu ya mustakabali wa elimu yetu. Moja ya hoja yake ulihusu umri wa mwanafunzi kuanza shule.

Alisema kuwa kuanza shule na miaka 5 au 6 haifai sababu mtoto anamaliza na miaka 12-13. Umri ambao hawezi kuwa na manufaa yoyote kwa jamii. Kwanza nchi ya kijamaa inahitaji wafanyakazi(wakulima). Mtoto wa 12 hawezi kuwa na manufaa yoyote. Pili asilimia kubwa sana ya watoto waliomaliza shule ya msingi enzi hizo, asilimia 87 walikuwa hawaendelei na sekondari, hivyo ni bora wabapomaliza shule ya msingi wawe na uwezo wa kufanya kazi. Huo ndiyo mwanzo wa kuanza shule na miaka 7. Unaweza soma kitabu chake hicho na vingine vingi bure ndani ya maktaba app. Ipakue playstore.View attachment 2163089
Sawa! Alikuwa sahihi kwa karne iliyopita.kiukweli Sasa hivi hata mtaala wetu unahitaji mabadiliko makubwa sana ili uendane na millennium age! (Karne ya sayansi na teknolojia) maarifa mengi yanayotolewa yako nyuma ya wakati.Wakati akitoa wazo lake elimu ya msingi ilikua basic wakati sasa hivi elimu basic ni kidato cha NNE.
 
Nyerere alikuwa sahihi, hata hivyo zama zimebadilika. Hatuna budi kujitafakari kama kweli ni lazima kusubiri miaka 7 ndipo mtoto aanze elimu ya msingi. Nadhani tunaweza kubadili bila athari zozote kubwa, na tutachochea ari ya vijana kujitegemea mapema zaidi kwa kuchangia pato la taifa badala ya kuendelea kuwa tegemezi kwa wazazi wao.

Tangu kuanza kwa Sekondari za Kata, asilimia kubwa ya watanzania wanafanikiwa kupata Elimu ya sekondari. Hii inaongeza miaka mingine 4 vijana wakingali chini ya mfumo rasmi wa elimu wenye usimamizi wa karibu.

Mimi naona sio vibaya tukirudisha miaka 2 nyuma, watoto waruhusiwe kuanza shule na miaka 5 ili wamalize sekondari wakiwa na umri wa miaka 16.

Kwa jinsi elimu yetu ya sasa ilivyo, watu wanazeekea shuleni. Fikiria mtu anamaliza digrii na miaka 23-25!
Hio mbna siku hiz ni kawaida watoto wa Miaka mitano wanaanza drs la kwanza. Mitatu wapo chekechea
 
Aliwajaza watu ujinga kuwa eti miaka 12 au 13 ndio mwisho wa kusoma mtoto akianza kusoma mapema. Dah, huyu Mzee hapo alibugi sana tena sana.
Wewe umebugia mazima bila hata kutafuna. Mbona humlaumu babu yako kwamba alibugi kwa kutokuwa tajiri wakati mababu wengine walikuwa matajiri? Nyambafu.
 
Badala ya kuongeza idadi ya madarasa na walimu anawaambia wacheleweshwe kusoma ndiyo kwa wewe yupo sahihi? Daah!

Alikuwa anajenga utumwa mambo leo?
Siwezi kumlaumu Nyerere kwa hilo. Kabla hujalaumu fuatilia historia kwanza. Kama tu familia zinawashinda kuendesha utaweza kuendesha nchi kirahisi hasa nchi maskini iliyokuwa imetopea umaskini wa kutupwa?. Kila jambo lina wakati wake tupo bize kusifia vya wenzetu tukidhani tuonavyo maendeleo yao leo ndivyo walivyokuwa miaka 100+ huko nyuma. Kila kitu lazima kiwe na mwanzo we bibi.
 
Aliwasaidia watoto wengi kufaidi usingizi mtamu. wa siku hizi miaka miwili mitatu wanaamshwa saa kumi kujiandaa kwenda shule. Ndo maana vingi havina adabu vimeanza kupata stress mapema mno
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Siwezi kumlaumu Nyerere kwa hilo. Kabla hujalaumu fuatilia historia kwanza. Kama tu familia zinawashinda kuendesha utaweza kuendesha nchi kirahisi hasa nchi maskini iliyokuwa imetopea umaskini wa kutupwa?. Kila jambo lina wakati wake tupo bize kusifia vya wenzetu tukidhani tuonavyo maendeleo yao leo ndivyo walivyokuwa miaka 100+ huko nyuma. Kila kitu lazima kiwe na mwanzo we bibi.
Mlidanganywa kuwa Tanzania ni masikini mkadanganyika. Familia ipi iliyoshindwa kujiendesha? Labda ya baba'ko na mama'ko.

Soma wewe historia uelewe Nyerere alipokabidhiwa Tanganyika ilikuwaje. Kama huelewi, Tanganyika ilikuwa ndiyo nchi ya kwanza katika Afrika inayosafirisha mazao kwa wingi. Kama ulikuwa huelewi, Tanganyika ilikuwa inaajiri wageni kutokea nje ya Tanganyika, kuanzia Wanyarwanda, Wajaluo (asili ya Nyerere?) mpaka Wanyasa ( Malawi. Soma kuhusu manamba.

Unataka kuongelea historia wakati huielewi historia, ujuha huo. Uliza tukujuze historia usikurupuke kutaka kuongelea usivyovielewa.
 
Wewe umebugia mazima bila hata kutafuna. Mbona humlaumu babu yako kwamba alibugi kwa kutokuwa tajiri wakati mababu wengine walikuwa matajiri? Nyambafu.
Utajiri ni "subjective". Uliwahi kusikia babu yangu kakosa kusoma au kafata ujinga mliojazwa nao ninyi wa kuomba omba mpaka leo bado unalalamika lalamika kuomba omba.
 
Kuna research iliyofanyika kuhusu umri wa mtoto kuanza shule, iligundulika watoto wa USA wanaoanza shule na umri wa miaka 3-4 wanapata matatizo ya concentration ikiwemo Attention Deficity Hypertension Disorder (ADHD).

Scandinavia wanapeleka watoto shule mapema kwasababu ya kusaidia wazazi childcare cost pia kumfanya mtoto azoee kucheza na wenzake. Watoto wengi wa Ulaya huzaliwa watoto pekee hivyo kukosa mtoto wa kucheza Naye.

Watoto hawa wanacheza tu na wanaanza rasmi academic life wakiwa na miaka mitano. Research imeonyesha Scandinavia matatizo ya ADHD yako kidogo sana kulinganisha my USA.

Hata hivyo miaka saba ni kumchelewesha mtoto kuanza academic life.
 
Kama hatuwezi kupunguz umri wa mtoto kuanza shule lets say pengine aanze na miaka 5 basi tupunguze madarasa kidgo

Elimu ya Tz imezeeka inahitaji maboresho makubwa sana ,ili kuyafanya haya inahitaji ki9ngozi mweny uelewa siyo huyu wa sasa
 
Back
Top Bottom