Nyerere ndiye aliyeshauri umri wa kuanza shule uwe miaka 7

Nyerere ndiye aliyeshauri umri wa kuanza shule uwe miaka 7

Badala ya kuongeza idadi ya madarasa na walimu anawaambia wacheleweshwe kusoma ndiyo kwa wewe yupo sahihi? Daah!

Alikuwa anajenga utumwa mambo leo?
Ukiwa nje ya game ni rahisi sana kuona mapungufu ya mchezaji,lakini Sasa kimbembe kinakuja pale utakapopewa wwe jezi, hivi ingekuwa wwe ndiyo Nyerere kwa kipinde kile hali ya Nchi ilivyokua ungeweza kuja na wazo zuri sana kama lile la Mwalimu!?
 
Aliwasaidia watoto wengi kufaidi usingizi mtamu. wa siku hizi miaka miwili mitatu wanaamshwa saa kumi kujiandaa kwenda shule. Ndo maana vingi havina adabu vimeanza kupata stress mapema mno
Vi kina Junior hivyo!! Hahahaha! Nimecheka balaa!![emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwenye kitabu elimu ya kujitegemea Mwalimu Nyerere alitoa hoja nyingi juu ya mustakabali wa elimu yetu. Moja ya hoja yake ulihusu umri wa mwanafunzi kuanza shule.

Alisema kuwa kuanza shule na miaka 5 au 6 haifai sababu mtoto anamaliza na miaka 12-13. Umri ambao hawezi kuwa na manufaa yoyote kwa jamii. Kwanza nchi ya kijamaa inahitaji wafanyakazi(wakulima).

Mtoto wa 12 hawezi kuwa na manufaa yoyote. Pili asilimia kubwa sana ya watoto waliomaliza shule ya msingi enzi hizo, asilimia 87 walikuwa hawaendelei na sekondari, hivyo ni bora wabapomaliza shule ya msingi wawe na uwezo wa kufanya kazi.

Huo ndiyo mwanzo wa kuanza shule na miaka 7. Unaweza soma kitabu chake hicho na vingine vingi bure ndani ya maktaba app. Ipakue playstore.

View attachment 2163089
Nchi za Magharibi mtoto anaanza la kwanza akiwa na miaka 6/7, so hajakosea. Alikuwa sahihi.
 
Yap, hilo muhimu sana. Kuliko hawa wanaokariri mambo bila kujua hata sababu ya kwanini yanafanyika hivyo.

If you think small, you will small for a Life...

Hawa wa sasa hawana hata muda wa kukaa na kutafakari kizazi kijacho wanataka kiwe na maisha gani,, wao wanawaza kesho yao tu na kwenda na trend.. Wanasahau kuwa hili taifa wataliacha na hawatakumbukwa kwa lolote.
 
Aliwajaza watu ujinga kuwa eti miaka 12 au 13 ndio mwisho wa kusoma mtoto akianza kusoma mapema. Dah, huyu Mzee hapo alibugi sana tena sana.
Kulikuwa na shule za kuhamishiaa waliomaliza la saba kama ilivyo sasa(shule za kata)?
 
Unaongelea mwaka gani?

Hii "shule za kata" ni jina la utambuzi tu, mitaala ni ile ile mibovu iliyoachwa toka enzi za Nyerere.
Nilimaanisha kipindi chake(Nyerere) kulikuwa na shule chache mno za upili kiasi kwamba angechukua wanafunzi wengi primary asingeweza kuwapeleka shule za upili kama ilivyo sasa hivyo kulazimika kuweka vikwazo.

I Respect u FF
 
Si angejenga, kilimshinda nini kujenga shule?
 
Si angejenga, kilimshinda nini kujenga shule?
Si angejengaaa! Unafikiri kujenga ni sawa na kutamka tu halafu mambo yakatokea. Kama ni rahisi hivyo mbona mpaka leo shule za msingi mnajenga na bado na bado tutaendelea kujenga, ulitaka yeye ndiye ajenge kila kitu? Kwa uchumi upi aliorithi toka kwa mkoloni Nyerere angefanya hayo maajabu ya kujenga shule kila kijiji? Labda kama sekta nyingine zote zingesimama angalau kwa miaka mitano ndio angeweza kuthubutu kufanya hayo unayoyataka wewe. Ni uongo mkubwa kusema Nyerere hakujenga shule za msingi kipindi chake. Fanya utafiti wako kujua wakoloni waliach shule ngapi za msingi wakati wanaondoka na Nyerere aliacha shule ngapi za msingi nchini wakati anang'atuka madarakani 1985. MTU ANAYEMLAU NYERERE KWAMBA HAKULETA MAENDELEO MI HUWA NAMUONA DISH LIMEYUMBA KIDOGO! SISEMI KWAMBA NYERERE ALIKUWA PERFECT, NO.
 
Sikuhizi degree 18-20, na sisi tutafika kama wao
 
Nyerere alikuwa sahihi, hata hivyo zama zimebadilika. Hatuna budi kujitafakari kama kweli ni lazima kusubiri miaka 7 ndipo mtoto aanze elimu ya msingi. Nadhani tunaweza kubadili bila athari zozote kubwa, na tutachochea ari ya vijana kujitegemea mapema zaidi kwa kuchangia pato la taifa badala ya kuendelea kuwa tegemezi kwa wazazi wao.

Tangu kuanza kwa Sekondari za Kata, asilimia kubwa ya watanzania wanafanikiwa kupata Elimu ya sekondari. Hii inaongeza miaka mingine 4 vijana wakingali chini ya mfumo rasmi wa elimu wenye usimamizi wa karibu.

Mimi naona sio vibaya tukirudisha miaka 2 nyuma, watoto waruhusiwe kuanza shule na miaka 5 ili wamalize sekondari wakiwa na umri wa miaka 16.

Kwa jinsi elimu yetu ya sasa ilivyo, watu wanazeekea shuleni. Fikiria mtu anamaliza digrii na miaka 23-25!
Mtoto anayeanza shule akiwa na umri huu wa miaka 5 mara nyingi akili yake inakuwa haina uwezo wa kung'amua mambo na kuwaza kwa mantiki,mtoto katika umri huu bado hajatambiua kama anachokifanya kinategemeana na akili zake.

Fikiria mtoto wa miaka 9 anaanza kushika kanuni kubwa kubwa za kihisabati,anachanganyikiwa.
Kuna watoto primary anakuwa mzito sana katika kujifunza lakini akifika sekondary form three anakuwa active sana maana akili yake sasa ndo imepevuka vya kutosha.
Mimi ni mwalimu naongea kwa uzoefu wangu kutokana na wanafunzi ninaokutana nao .
Ingawa sio wote huwa wazito ila asilimia kubwa ni wazito yaani ¹/10
 
Age is nothing but a number. Watoto wa siku hiz wanapevuka mapema bora wawahi kuanza shule.
 
Mtoto anayeanza shule akiwa na umri huu wa miaka 5 mara nyingi akili yake inakuwa haina uwezo wa kung'amua mambo na kuwaza kwa mantiki,mtoto katika umri huu bado hajatambiua kama anachokifanya kinategemeana na akili zake.

Fikiria mtoto wa miaka 9 anaanza kushika kanuni kubwa kubwa za kihisabati,anachanganyikiwa.
Kuna watoto primary anakuwa mzito sana katika kujifunza lakini akifika sekondary form three anakuwa active sana maana akili yake sasa ndo imepevuka vya kutosha.
Mimi ni mwalimu naongea kwa uzoefu wangu kutokana na wanafunzi ninaokutana nao .
Ingawa sio wote huwa wazito ila asilimia kubwa ni wazito yaani ¹/10

mkuu unaongelea watoto wa zama zipi? watoto wa miaka mitatu wa sasa wanaperuzi android phones hata mimi mwenye siwawezi
 
Hakika ulikuwa ushauri mzuri zama hizi tumeanza kupeleka watoto shule wenye mwaka na nusu
Tofautisha shule ya kusoma na day are, hiyo ya watoto wa wadogo chini ya miaka minne ni daycare, na serikali inazitambua kuwa ni vituo vya malezi watoto wake hawatarajii maajabu ya kielimu katika umri huo
 
Bajeti ya kupiganisha nchi vita alikuwa nayo, bajeti ya kupeleka misaada Biafra alikuwa nayo, bajeti ya kupigana vita zisizokuwa zake alikuwa nazo, bajeti ya elimu ndiyo kakosa?

Maajabu hayo.
Hakuna nchi yenye bajeti ndogo kwenye ulinzi. Nadhani ndio inaongoza mpaka huko Saudi Arabia wanakoenda kuhiji,bajeti ya silaha usipime.
 
Ukiwa nje ya game ni rahisi sana kuona mapungufu ya mchezaji,lakini Sasa kimbembe kinakuja pale utakapopewa wwe jezi, hivi ingekuwa wwe ndiyo Nyerere kwa kipinde kile hali ya Nchi ilivyokua ungeweza kuja na wazo zuri sana kama lile la Mwalimu!?
Tena alitoa elimu bure mpaka chuo kikuu,kwa wale wenye uwezo wa kufaulu. Pamoja na yeye kuwa mkristo akanyang'anya shule za wakristo ili watanzania wote wasome bila kujali dini zao.
 
Si angejengaaa! Unafikiri kujenga ni sawa na kutamka tu halafu mambo yakatokea. Kama ni rahisi hivyo mbona mpaka leo shule za msingi mnajenga na bado na bado tutaendelea kujenga, ulitaka yeye ndiye ajenge kila kitu? Kwa uchumi upi aliorithi toka kwa mkoloni Nyerere angefanya hayo maajabu ya kujenga shule kila kijiji? Labda kama sekta nyingine zote zingesimama angalau kwa miaka mitano ndio angeweza kuthubutu kufanya hayo unayoyataka wewe. Ni uongo mkubwa kusema Nyerere hakujenga shule za msingi kipindi chake. Fanya utafiti wako kujua wakoloni waliach shule ngapi za msingi wakati wanaondoka na Nyerere aliacha shule ngapi za msingi nchini wakati anang'atuka madarakani 1985. MTU ANAYEMLAU NYERERE KWAMBA HAKULETA MAENDELEO MI HUWA NAMUONA DISH LIMEYUMBA KIDOGO! SISEMI KWAMBA NYERERE ALIKUWA PERFECT, NO.
hajawahi kujenga kila mkoa atajenga kila kijiji? Unaota wewe.
 
Back
Top Bottom