Nyie wenye ndoa, mliwezaje kufanya maamuzi mpaka mkaingia ndani ya ndoa?

Hatuwezi kufanana huyo ni wewe huna wito wa ndoa.
 
Hayo yote uliyoyaandika juu ukijiuliza sio kikwazo cha ndoa,wito maana yake uwezo ulio juu ya mtu katika kubeba majukumu yaliyo mbele yake.
Kubeba majukumu huku huna hela?
Kwamba mnaenda kula mawe.
Kwamba mkiumwa hospital mnapeleka majani?
Kwamba maisha bila pesa YATASONGAJE?

#YNWA
 
Habari mkuu,hapo kitu kikubwa kinachokuumiza ni past history ya huyo mwanamke wako wa kwanza,pole sana ila nakuomba jitahidi kusahau,ni kweli psychological unakua tortured,ni kama wale watoto wa Kongo wanaowaua wazazi wao kwa amri za waasi,yaani wanakua hawaoni thamani ya kuishi tena,hio ni psychology tu,jitahidi sana mkuu kusamehe yapite,kuna nguvu kubwa sana mkuu kuhusu kusamehe hasa kwa viumbe zaifu kama watoto na wanawake.

Mi binafsi wanawake wangu wote wa nyuma either tumeachana kwa ugomvi ama kwa fujo,nafanyaga hivi:-
Naamini imeshatokea,na sitakiwi kuweka kisasi,yaani naondoa chuki,hata awe nashida nitamsaidia,dah imenifanya wawe wananiheshimu sana na kuniona mtu wa ajabu,ila moyo wangu una amani yaani Sina haraka,kila issue natumia akili na si hisia,unajua mukiachana kuna hali ya kushindana,binafsi naishi maisha yangu kadri mungu alivonijaalia,[emoji16][emoji16],sasa unaonekana kama mkaidi hivi,lakini kiukweli unakua unaishi kwa amani....we amini tu hakuna binadamu mkamilifu,msamehe mama mtoto wako,siku mtafute mtembelee wewe na mtoto,usijenge chuki hata ukienda akikutukana don't take it personally...,..yaani maisha hayahitaji uwe mtu flani hivi wa visasi,visirani[emoji16][emoji38],.....,yaani maisha yanahitaji mtu fulani hivi anayejifanya mjinga hana akili huku akijijali mwenyewe na akijali wenzake no matter what?,....jitahidi uishi hivi mkuu



=============

....nami naomba nikushauri kwenye mambo kama ulivoyapanga kulingana na stori yako.
1.kuhusu elimu sijajua upo kitengo gani.....lakini elimu ya master inatosha sana kutafuta mkate wako wa kila siku,labda tu riziki haijafunguka,endelea kumuomba mungu one day yes.....na mshukuru sana kwa kupata master ukiwa tu miaka 31.......kuhusu pHD hio usiwe na haraka nayo sasa,invest sasa kwenye aspect nyingine za maisha kama biashara,familia,afya yako ya mwili na akili......yaani ondoa ile zana kua mimi bila PhD siwezi kufanikiwa,ni psychology tu....tena kama upo serikalini ni rahisi maana PhD si kigezo saaana cha mshahara.
2.Kwenye Kazi hizo hustling unazofanya ndio zenyewe hizo,yaani hapo endelea kukaza fanya hata lobying uende ofisi kubwa kubwa,nakupa big up kwenye hilo

3.Investmet hapo nitakushauri kitaalam zaidi.
Kama zaidi ya 50% ya mshahara wako unatumia kuinvest hio ni hatari sana kiongozi......na kitu kikubwa nachokiona unainvest zaidi kwenye trees,trees ni highly risk,thuy why hakuna insurance inakubali kuhold trees.......na heka 1000 ni nyingi sana,....kuna mdau amekuita una tamaa hapo juu,yupo sahihi kwa namna fulani na nashauri usimzarau,chukua ushauri wake ufanyie kazi hata kama ameutoa katika namna ya kukashifu....kwenye uwekezaji wa shamba nashauri ungeanza hata na heka 50,kisha unaongeza kidogo kidogo kadri ya riziki na kipato chako.......hatuombei lakini ris zipo,imagine umehudumia shamba la miti miaka 10,kisha linaungua,unafanyaje?,
Kwenye kuwekeza mara zote diversify your portfolio,...usiwekeze kwenye kitu kimoja,kwa umri wako,jitahidi mkuu uwe na BONDS,STOCKS,CRYPTOS,REAL ESTATES(viwanja,mashamba etc),na sio kimoja tu Kati ya hivo)kama nilivoona kwenye bandiko lako.

Mfano kwenye mshahara unatoa laki 5,kuwekeza,........25%weka bonds,25%stocks,25%cryptos,25%real estates......hizo asset ni lower risk,na utakua umefanya divisible ya portfolio yako.
Ila pia tafuta biashara itakayokuweka busy kidogo,then kafaida saidia ndugu na jamaa wenye uhitaji......yaani tengeneza ile humanity ili uone umuhimu na nini maana ya kuishi na kukujengea utu.......usitumie faida yoote ya biashara kuwekeza......hata kumsaidia mtoto yatima ni kuwekeza kwa mungu,hata kufungua biashara hupati faida ni kuwekeza kwa wale wanaofanya kazi......usiyaangalie maisha yako wewe kama wewe,la hasha maisha ni pamoja na wenzako.

4.Mtoto
Huyo hana hatia,mlee katika maadili,jitahidi umpeleke kwenye Shule za dini ukipata uwezo,inshallah
5.Mifano
Uzoefu wa watu wengine hauna maana kwako,tunapitia mazingira tofauti sana na wote hatuwezi kufanana,kikubwa tafuta mwanamke muelewea mfatilie,ongea nao,onyesha nia naye,naamini mutaelewena tu.....kama ni wako atakusikiliza tu.
NOTE.
Binafsi sijaoa,Sina mtoto......ila naamini siku moja nitakuja kuoa na kua na familia........Maisha yana changamoto sio "straightway".....kikubwa ni Imani na uthubutu tu.
 
By 35 nitakua nishafunga kuzaa watoto 3 wanatosha,, anyway life is yours fanya unachoamini wewe!
[emoji16][emoji16]kuna wanawake wanafunga uzazi wakiwa na miaka 26......vijijini huku,dah wakati mi baba yangu alinizaa akiwa na 40+,.......duniani hatujaletwa kushindana......kikubwa mipango yetu isitupeleke kwenye zambi na kuvunja sheria kwa makusudi........time is relative to yourself and not other......wapo waliooa/kuolewa na miaka 20 lakini masikini wakutupwa kiasi matoto wamekua machokoraa wapo pia waliooa/kuolewa na miaka 40,masikini wa kutupwa watoto machokoraa......ila pia kinyume chake kinaweza tokea.......narudia tena,hatukuumbwa kushindana duniani
 
Wapo sahihi kwa muktadha wao.......binadamu hatuiangalii dunia wote sawa,kwa namna moja.......miaka 60 Tz mtu anastaafu Kazi.......u.s miaka hiyo mtu anagombea uraisi hana habari,imagine doctor wa Biden ana miaka 80,....yaani hana habari..........time is relative to yourself and not another
 
Mkuu unahisi kua na nyumba,gari ndio unakua umeshamaliza kila kitu duniani......nashauri ondoa hii mentality.........nyumba ni lazima kila binadamu aishi pazuri,gari ni means tu ya transport,......na sidhani kama ina uhusiano na mapenzi/ndoa.........Yaaani katika maisha take it easy,..........ni kama mtu anaejisifi anamiliki smartphone,au nguo mpya......wakati ideally ailibidi ajisifu purpose ya hizo items kusimplify maisha......lakini yeye anaona ndio utajiri wenyewe huu[emoji16][emoji16],......human resource ana umuhimu wake naye afananishwi na material resources.......take it easy.......invest for betterment of world......
 
Live the life you love, Love the life you live.
Ndugu yangu kaa ukijua kwamba "Marriage is a female institution, Man draws absolutely nothing from marriage, man have to sacrifice his ambitions, properties,Time,Plans etc"
na ndo mana unaona hata wenzako walipooa tu na mipango ya kurudi chuo ikafa. It means walisacrifice plans zao kwa sababu ya ndoa.
Wanawake wanafaidi sana ndoani kuliko wanaume ndo mana wanawake hua wanalilia sana ndoa.
 
Liverpool VPN mkuu naona sasa taratibu unaelekea kuoa. Nyuzi zako zamani ulikuwa unatukana waliooa ila tune sasa inabadilika unahoji. Mwendo huu ukiwa hivi naomba kukakiribishwa kwenye harusi, maybe within 2 years kutoka sasa.

Hata mimi mengi ya uliyoongea huwa najiuliza hivo hivo na huwa sina amani nayo.
 
Unaweza kuwa una tatizo la kisaikolojia kutokana na childhood maana kila mtu ana tatizo lake. Kwako wewe familia na malezi uliyopitia yanakupa Gamophobia (fear of marriage).

Kwa kuwa hukukua kwenye familia ya wazazi basi una priority ya pesa kuliko kitu kingine. Yawezekana utotoni ulikuwa unaamini furaha yako utaitafuta mwenyewe pale utakapokuwa na pesa. Na huwezi tosheka hela sasa. Nami naongeza juhudi, OA!
 
Ukikuta siyo mama wala Baba yako anataka uoe jua anakosa maslahi kwako Kwa kuwa huna mke , na anajua ukipata mke possibly maslahi yake atapata

Panga mambo yako mweleze Mungu mipango yako, muombe akitangulie. Naamini hivyo wasikupoteze kbs
 
Nikupongeze walau kwa kuona ni bora uulize mambo yakoje humu ndani kabla ya kuingia,
Pamoja na kwamba ni kweli kuoa ni jambo jema na muhimu lakini pia ni vema kujua yanayojiri humu ndani,
bahati nzuri kwako ni kwamba umeanza vizuri kwa kujiwekea miradi, hii itakusaidia kupata direction ya maisha,
Kifupi ni kuwa, wanawake (hasa wa sasa) ni matatizo makubwa sana, ndio maana wanaume wengi huishia kuugua magonjwa ya moyo na sukari, (tumewaona wengi), wanawake walikuwa zamani, kwani waliwaheshimu na kuwatii waume zao, hawa wa sasa hivi (majority) unavyowasikia wanaongea mitaani na mitandaoni ndivyo walivyo haswa, unakuta mke wa mtu hawezi hata kumtengea mumewe chakula, hawawezi siku hizi hata kupiga pasi nguo za mume, kijumla mnakuwa ndani wote kama mtu na jirani yake, ndio maana wanasema hujanioa bali tumeoana, kwa hiyo sisemi kwamba usioe bali nasema endelea kutafakari, asilimia kubwa sana ya wana ndoa wanaishi kwa mikwaruzano ya kila siku na bahati mbaya huwa wanajaribu kuficha yasionekane nje, ukiona mtu anatoka kwenye shughuli zake anaamua kupitia baa anakaa huko mpaka usiku mrefu ndio anaenda nyumbani kwake, ujue huyo nakwepa maneno ya mkewe, kwa hiyo anaona ni heri aende akakae baa pumzishe akili yake na kwa sababu kule hakuna rabsha kuliko kuenda nyumbani kwake mapema, yaaani anafika nyumbani anakuta mkewe ameshalala, anaondoka asubuhi mkewe hajaamka, ukiwa single unaweza kuyakwepa haya yote, lakini kumbuka umri nao unasonga mbele, endelea kutafakari.
 
1. Kulelewa bila wazazi haimaniishi hujalelewa maisha ya ndoa.

Unaweza kuchukuliwa na mlezi ukamkuta ana ndoa nzuriii na wakakulea kama mtoto wao.

2. Pesa ndio kila kitu ndugu "If you think money does not bring happiness go and ask Homeless and Jobless"

#YNWA
 
Braza ngoja nitafute helaa...
Sijakataa kuoa ila huwa napinga Mwanaume KUOA MAPEMA.

Angalau hata miaka 35 hivi.

#YNWA
 
Unahitaji mwanamke ambae mnaendana kifikra, kimawazo, kimtazamo na most of all, you share your dreams together, mbali na hapo itakua ni ngumu kutimiza ndoto zako

Usiogope kuoa, Mwombe Mungu akupatie mwanamke wa kufanana na wewe.
 
Nakubali mkuu kwa asilimia nyingi sana ... very very true
 
Unahitaji mwanamke ambae mnaendana kifikra, kimawazo, kimtazamo na most of all, you share your dreams together, mbali na hapo itakua ni ngumu kutimiza ndoto zako

Usiogope kupa, Mwombe Mungu akupatie mwanamke wa kufanana na wewe.
Mtu kama Diamond Platnumz akipata mwanamke anaefanana nae tabia. Itakuaje hapo? Baba ana watoto 4 kwa mama tofauti, Mama nae ana watoto 4 kwa baba tofauti. Baba leo ana scandle ya kutoka na fulani, Mama nae kesho anajibu mapigo kama Palestina na Israel. Noma na nusu.


Sidhani kama namba zitasoma.[emoji16][emoji3][emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…