Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Aah umeruka mstari...
Chanuo kampa nani ? Chanuo kampa nani?
Kampa msusi kampa msusi....
Mafuta kampa nani? Mafuta kampa nani?
Kampa msusi kampa msusi...
Ahsante mkuu kwa kunikumbushia huo ubeti,si unajua kitambo sana
 
Kumbee mi mpka leo nilijua zile ndege za Urusi labda wamebadili teknolojia hahahaha!!! Nawakumbuka Sana hao mbayuwayu... Ww utakuwa mhenga lol
 


Umenikumbusha mbaali saana
 
Nasakaa mke wangu....nasaka mke wangu,haaapa hayupo haaapa hayupo...kaeeenda wapi?...kaeenda wapi?,kaeenda kusuka..kaeenda kasuka,kachukuaa... nini? na nini?,kachukuaa chanuuuo na mafutaa
mafuta kampa nani mafuta kampa nani.....kampa msusi kampa msusi
chanuo kampa nani chanuo kampa nani.......kampa msusi kampa msusi
 
Old School Re-union...
 
Mwenzenu mimiii eeeeeeeeeee mchumba wangu eeeeeeeeeee ni simatiiiii eeeeeeeeeeeeeee lol pronunciations za kitoto simati


Cc Smart911
 
Its complicated sijui nianzie wapi. Mnaozinga mko wawili, mnaowawinda wanakuwa wanazunguka kwenye umbo mstatili.

Hahahahaaa yaani wewe unakumbuka kabisaa na ilikuwa atakayecheza hadi kufikia 100 kwa kuhesabu vile vyumba vya mstatili kwenye kila pembe au kona anakuwa kawaokoa wengine wote waliobabuliwa. Mnaozinga msipokuwa na ushirikiano mtazinga hata mara tatu. Hapo ndo kubabuana mabomba kanaanza na mpira ujazwa mchanga hahahahhaaa ukibabuliwa la uso lazima ukae chini kwanza hahahahahaa.

Ila napenda kwasababu inakupa akili ya mahesabu na kufikiria nawamalizaje hawa kisha nami niingie kucheza,mie nilikuwa nikizinga nahakikisha nimewababua kwanza wanaojua kucheza wenye machejo. Halafu wale ambao hawana machejo aaah unawamaliza fasta. Aliyetoka wa kwanza na wa mwisho ndo wanazinga.

Sasa nikiingia kucheza nahakikisha napambana sibabuliwi wa kwanza na pia nachezaaa nikiona watu wanakaribia kuisha najibabulisha ili nisizinge hehehehehehehehee. Hesabu za kitaani hizo zinaitwa.

Sasa itokee waliobabuliwa ifike zamu yao kuzinga halafu wajidai wameitwa kwao weeeh lazima tuwababue kwa mpira na wakija siku ingine lazima waanzie kuzinga.

Na ikitokea mti kaja kakuta mchezo ushaanza na anataka kuingia basi anaambiwa aingie kuzinga kwanza kisha ndo acheze wakifanikiwa kuwababua wote.

Mkifika siku ingine ndo mnaanza mnapinga inkseeksooo mnakuwa wanne, wataonyanyua viganja juu timu moja wataofunika viganja timu ya pili weeeh ilikuwa raha. Hiyo tuliitumia kwe ye rede ya mateka. Daaah those days....
 
Vipi yange yange walishawahi kukupa kucha nyeupe? Wakipita juu tulikuwa tubaimba
Yange yange nipe kucha nyeupeee....
Cha ajabu kweli kwenye kucha kunatokea vidoa vyeupe!

Hahahahaaa daaah ungekuwa Nyani Ngabu ningekwambia fcuk you. .... unajua kwanini......
We nahisi tulikaa mtaa mmoja au ulikuja kuhamia mtaa ambao sie tulihama hahahahhahahaaa

Hiyo ya yangeyange nipe kucha nyeupe nimefanya sana. Tena nikiwa na kaka zangu, tukienda kwa babu yetu Upanga mtaa wa Malik sijui ule karibu na kwa baba taibali jioni wanapita yangeyange weengiii. Basi tunaanza yangeyange nipe kucha nyeupee hahahahahaha na kweli.....

Huwezi amini hadi sass hivi kucha zangu kama sijapaka hina au rangi ya kucha hizo alama nyeupe zinaonekana daaah

Hahahahahahahahahahaaaa
 

Aaahahahahahhahahahahahaaa aahahahahahhaahahhaahhahahahaa eehehehehehehehehheheheeeee yaani weweee umenifanya nicheke kwanguvu hapa nilipo loooh
Nimevuta taswira jinsi ulivokuwa unaimba huo wimbo kwanguvu bila wasiwasi unashangaa unavutwa ndani paaah paaah kichapo loooh.

Pole mwaya looh nimecheka hadi machozi looh.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…