Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Sheki ilikuwa ya vyumba sita kila na kila mstari anakaa moja na ule wa katikati anakuwepo mmoja anaitwa centre.

Timu ya nje inakuwa na watu sawa mnaaza kuingia na mnawazunguka kwa kuwapiga chenga.

Rede ni mchezo wa kumpiga mtu na mpira, tena mipira ya soxi na neno rede linatokana na neno ready.

Kuna mtu humu amesema ready ya chupa, yaani ulikuwa unapigwa na mpira, ukiukwepa unakimbilia kujaza chupa kwa mchanga hadi ijae.

Ukiudaka unautupa mbali ili apoteze muda ili ujaze mchanga na hilo kwako ni goli.

Ya kuchora mstari Kati?ikoje hiyo? istilahi ya rede sheki ni mpya nidadavulie
 
Ulikosa vitu vingi kimaisha. Mimi kama wewe nimekulia mitaa kama hiyohiyo ya uzunguni yaani Masaki, Oysterbay, Bugando, Capri Pint, Upanga.

Nilikuwa likizo lazima niende Mwananyamala kwa mjomba maana hii michezo yote kule ndiko chuo kikuu na kimsingi yote hii ni kama ilianzia huko.

Niliona tofauti mtoto wa Uzunguni na Mwananyamala.

Watu wanadhani kukulia Uzunguni kuna raha, kuumbe si sahihi sana. Ukiachilia mbali mazingira ya kusoma lakini kwa furaha ya mtoto mazingira kama Mwananyamala yenye michozo kama hii inamjenga mtoto ujasiri.

Taabu ni kwamba mtoto anatakiwa akae kwa muda tu aondoke na arudi kusoma na kiukweli mitaa kama Mwananyamala haifai kwa mtoto kusoma.

Ndiyo maana binafsi ninayajua maisha ya aina zote yaani uswahilini na uzunguzi. Katika michezo ya watoto hakuna mahali pazuri kama uswahilini.

Katika kuanza kusoma mahala pazuri ni Uzunguni.

Sasa tabu yenu wenzangu mkishakuwa mnataka kuwa wabunge wa uswahilini ambako hamkukulia.

Huku kwetu masaki hatujuagi ayo....wa uswahili peaneni
 
Bado uko kule Mwanza hasa Kisesa au Bujora.

Hivi ule utamaduni wa mangongoti(mtaalam anayevaa kama dude la kutisha huku akitembea juu ya miti miwili kumfanya aonekanae mrefu kama giant) imepotelea wapi these days?, i relly miss it
 
Kuna nyimbo za michezo ya watoto na ndizo wengi wanazikumbuka na hizi wengi tuliozicheza hatutazisahau.

Huu wa mabata madogo madogo ndiyo ulikuwa wa kitoto lakini ulikuwa kwa wanafunzi.

Nimesoma karibu page zote sijaona wimbo wa

"mabata makubwa makubwa yanaogelea, yanaogelea katika mto

Yanapokuwa yanaoga kwa kwa kwa kwa kwa,
Kwa kwa kwa kwa kwa,

Kwa kwa kwa kwa kwa"
 
Tena umenikumbusha golori. Kwenye mpira ukishinda unapata pointi. Lakini golori ukishinda unapata "nyama". Hivyo ukiidungua golori unahesabu "nyama moja, moja mbili".

Kuna watu walikuwa balaa kulenga gololi. Anakudungua moja kisha anakaribia shimo, sintawasahau kwa majina.

Nilikua siupendii huu mchezo eti mtu anaingia kati anakata viuno yaan ilikua wakianza nasepa, bora nikacheze goroli tu.
 
Ilikuwa inaitwa nageeee.

Kawaida mlikuwa mnarushiana mpira kwa utaratibu. Lakini mkishakasirishana mnaanza kubabuana na mpira.

Hahahahaaa sheki rede mpira ukienda mbali unazunguka kwenye vyumba na kuhesabu. Pia kulikuwa na rede ya chupa. Aahahahahahahhahahahaaaa
 
Kwani mzee na wewe hizo nyimbo si ulizikuta hata kama umezaliwa 500BC lakini ulizikuta
 
..taambalaleeee nyeng'u nyeng'u X2..tambuuuu tambu nsitambu tambuuu tambu nsutaambu matumbuke singonya ngonya..aingonyonya ya mwaka jana...pete na rundoooo na rundo leo shetan kajamba mbaaaaaa......
 
Namtafuta mkewanguu namtafuta mkewaguu...hapa hayupo hapa hayupo
Kaenda wapi kaenda wapiiii..kaenda kusuka kaenda kusuka

~Dada yangu ni rehema malaya anapenda kula chps na vijana,asbh na mapema sitendi kununu lile basi mologia...

~Ukuti ukuti wa nazi wana nziiii,mwenzetu kagongwa na nn na garii tumpeleke mnazi mmjoa asije kusema kwa baba yake piiiii piii pi mambo bado.

Zingine za kilugha
..hapo kwenye namtafuta mke wangu...mwisho ipo..huu mti gan..wa mchoma..ukiukataaa..haukatiki..hata kwa shoka haukatiki hata kwa panga haukatik..wakat mkeo yupo ndan kazingwa kwa kushikana mikono..ww inakata mikono iliyoshikana ukikatika unamkimbiza mkeo huyoooooo kwenye matuta ya viaz...sasa kitakachofuata huko n za kinguo nguo...n aaaashiiiiii aaashiiii...
 
Kuna wimbo uliimba hivi

Kimanumanu, kina manyoya manyoya

na mwingine uliimba hivi,

Sunday na mpira Sunday na mpira, kashuti gooo.

Anayekumbuka zote please.
 
Halafu redioni kulikuwa na wimbo unaniudhi,

Ulikuwa unaomba hivi

"Ukumbuke afya yako sanasana eeh
Uoge kila siku, safisha meno yako, mtu ni afyaaaaa
"

Sasa mimi kwa sababu michezo ilikuwa ni mingi narudi nyumbani nimechafuka halafu sipendi kuoga, nikiusikia tu huo waimbo natamani kuzima redio maana lazim mama atakukumbusha "Unaona hadi redio zinakuimba".

Mbaya zaidi wimbo huo ulikuwa unaimbwa kila ikifika saa moja jioni yaani wakati wa kuoga.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Back
Top Bottom