Nyoka mwenye uwezo wa kuua kwa sekunde 5 apatikana

Nyoka mwenye uwezo wa kuua kwa sekunde 5 apatikana

Aliyempiga hii picha ye'hakufa?

Maana nimeona hakamatiki wala hafikiriki!

Ukimuona ni tatizo kubwa na ukimuwaza unaweweseka kwa wazimu ama kuanguka kifafa!

Nd'onajiuliza hii picha ilichukuliwaje na mwenye kuichukua bado yupo hai?

Na tulioiangalia hatutapata madhara yoyote kweli?
Labda kwa drones
 
Kwa sifa alizozitaja mtoa mada, unajiuliza mkwamba mtoa mada amewezaje kuzipata endapo hata kupata harufu yake tu unapata vidonda vya koo na kisha kufa. Kwa siga hizo ni wazi kuwa kila aliyemfanyia utafiti atakuwa alikufa.
Anyway yawezekana mtoa mada ana dawa ya sumu ya kumdhibiti nyoka huyo.
 
Uongo mtupu nyoka wa youtube hao


Umesema ukisikia harufu yake unakufa
Afu umkasema anawezo wa kusikia umbali km 10

Afu unatwambia nyoka huyo akisikia makelele ya binadamu vilio nk anakuja karibu kusikiliza nini kinaendelea kama mnamjadili kufa anakimbia

Mpaka amesogea hapo si wanakuwa washakufa wote?
Nyoka wa hivyo angekuwepo dunia ingekuwa hatare sana
 
Hii nadhani ni ya yule jamaa wa Moro kule FB ni muongo kapitiliza hizi fact zina walakini mkubwa

Anaweza kung'ata watu 250 ndani ya sekunde tano na wote wakafa ndani ya sekunde hizo.
3. Anaweza kubadilika anapohisi kuwa kuna adui karibu yake na kuwa mamba.
12. Hazalishi wala hazai kwa sababu nyoka huyu huteremshwa toka angani.
14. Anatabia ya kulipiza kisasi pale alijeruhiwa. Hutoka msituni na kuja kuleta fujo mtaani.

15. Ana Iman ya dini na hujishughulisha na ibada.
Mkuu una uhakika anayezungumziwa hapo ni nyoka

Nilitegemea ungefungua code hapo utufafanulie

Binafsi mpaka sasa sijaamini na wala sitaki kuamini kama anayezungumziwa hapo ni Nyoka kama Nyoka

Yaani mkuu sixth sense yangu imegoma kabisa kuamini kama anayezungumziwa ni Nyoka mdudu
 
Ni dawa ipi sahihi ya haraka kuzuia sumu ya nyoka ukiwa mbali na hospital kabla ya kufika hospital. Mfano ukiwa porini unaweza ukatumia au kujichoma.
Mkojo wako uunywe.
 
4. Anaweza kung'ata watu 250 ndani ya sekunde tano na wote wakafa ndani ya sekunde hizo.

5. Ana urefu wa mita 25 yaani robo ya uwanja wa mpira wa miguu.

6. Anaweza kuruka kwa urefu wa mita 75 yaani robo tatu ya urefu wa uwanja wa mpira wa miguu.

7. Sehem aliyepita na kisha binadamu akapita kwa muda huo, anaweza kupalalaiz yaani akapata strock.

8. Anaweza kurusha mate na yakaenda urefu wa mita 100.

9. Anaweza kusikia na kuona kitu kilicho umbali wa kilomita 10.
Tafadhali!!

Kaa naye hukohuko usituletee balaa huku
 
Back
Top Bottom