Nyongeza ya mshahara inakuja. CHADEMA msidandie gari kwa mbele

Madeni tu ya wazabuni na baadhi ya wakandarasi serikali imeshindwa kulipa! Itawezaje kuongeza mishahara kwa watumishi wakati waalimu na maaskari wanaidai mabilioni ya pesa? Halafu miradi gani ya kimkakati iliyokwisha? Reli ya dar Moro bado ni mtihani labda itaisha mwaka 2024!
 
nakushauri tafuta duka linalouza akili ukanunue, tofauti na hapo unakoelekea kwa akili hizo utakuwa mtu wa kudharauliwa milele.
 
CHADEMA wangejenga barabara. Madaraja. Mashule. Hosp kwa pesa za ndani bila ya kukopa. Maendeleo bila ya pesa, au utajiri wa makampuni kote duniani wanakopa.
 
Nyongeza gani inafanyika baada ya miaka 5?Hilo ni deni mlilodhulumu watumishi.
 
Kutolipwa mishahara sio kwamba hawatalipwa. Kumbuka mchakato wa serikali kulipa madeni mrefu sana.
Mrefu unaanzia wapi hadi wapi? Ulishahakiki watumishi na hawalipi madai yao ukiulizwa unasema unajenga madaraja sijui ujinga ujinga gani???
 
 
Hamna kitu hapo
 
Hao jamaa wa ufipa kwishilia mbali.
 
Hilo likitokea hata shetani watashangaa imewezekanaje na kimetokea nini.
 
Mradi wa maji Isaka to Tabora na stendi ya mabasi Mbezi.
Hizo ni baadhi tu ya huduma za msingi ambazo ni wajibu wa serikali kwa watu wake ,wala hivyo sii vitu vya kujisifia kama tunavyo jaribu kuvitumia kuwahadaa wasiojua.
 
Kwa kweli.. Kila mfanya kazi aliyetumikia kwa miaka mitatu bila kupanda daraja, apande daraja moja.. Wale waliokaa miaka mitano and above bila kupanda daraja, wapande madaraja mawili. Fedha zipoo!
Hazipo zingekuwepo tusinge sh hudia tuyaonayo hii Leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…