Nyongo ya mamba ni sumu kali inayouwa kwa haraka zaidi




Mkuu, siyo kweli kwamba nyongo ya Mamba ni Sumu.

Ni kutokana na imani zilizozagaa sehemu mbalimbali za Afrika ya mashariki na kusini kwamba nyongo ya mamba ni sumu ndipo wanasayansi wakaamua kufanya utafiti juu ya hiyo nyongo, kuna mtafiti mmoja alichukua hiyo nyongo na kuwapa panya na nyani kitaalamu na wala hawakufa isitoshe huko mto zambezi kuna wachina wao kazi yao ni kuchukua nyongo ikiwa ndani ya (gall bladders) na kuikausha kisha kuipeleka China ikatumike kama dawa ya nguvu za kiume.

Nyongo ni kimiminika kinachozalishwa na ini kisha kuhifadhiwa katika kifuko kiitwacho gall bladder, kazi ya nyongo ambayo ipo kwa binadamu pia, ni uyeyeshaji wa mafuta yanayoingia na chakula katika utumbo mwembamba.

Watafiti wa mambo ya tiba na uganga wa asili wanasema nyongo ya mamba siyo sumu bali waganga wa miti shamba huchukua hiyo nyongo na kuchanganya na miti-shamba wanayoijua ambayo ni sumu, hivyo utaona kwamba sumu siyo hiyo nyongo bali sumu ni hiyo miti-shamba.
 
Kama umenisoma vizuri hatutofautiani sana,soma tena,niliandika inachanganywa na miti ya kiasili kutengeneza sumu inayojulikana kama nyongo ya mamba.
 
Hivi kuna watu wanakula chatu na mamba na wako dunia hii hii jamani
Hii sumu IPO sana mwambao Wa z Tanganyika kama hutaki kausha Mzee.
 
Hivi kuna watu wanakula chatu na mamba na wako dunia hii hii jamani


Ethiopia wanakula sana mamba kutoka mto Nile. Wachina nao wanakula sana Mamba na chatu na nyi
Kama umenisoma vizuri hatutofautiani sana,soma tena,niliandika inachanganywa na miti ya kiasili kutengeneza sumu inayojulikana kama nyongo ya mamba.



Angalia heading yako; "Nyongo ya mamba ni sumu kali inayoua kwa haraka zaidi".


Ni hiyo heading ndiyo naipinga, hapo kinachoonekana ni kwamba Sumu kuu ni hiyo nyongo licha ya kwamba ili ifanye kazi ni muhimu ichanganywe na kitu kingine.
 
Nikweli usemacho na ikitokea mamba amekufa na nyongo haionekani basi kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya haitalala aisee hiyo kitu ninoma huu Uzi Ni mzuri ila Kuna watu wanaleta utoto Kama huyo anayesema inauchachu
 
Muongo mkuu wa mwaka 2019
 
Mbona hizo picha A&B ni kende na dushelele?

Ini gani lenye sura ya mgawanyiko wa namna hiyo?

Halafu sasa kuna electric wire zimeunganishwa, imekaaje hii, ni model?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muongo mkuu wa mwaka 2019


Nyongo ya Mamba siyo sumu, ni uzushi na uongo uliozoeleka miongoni mwa jamii za kishirikina, sio kweli hata kidogo kwamba Nyongo iwe sumu.

Sasa wewe niambie kazi ya hiyo nyongo ya mamba mwilini mwa mamba ni ipi???

Nyongo ipo kwa binadamu, kwa kuku, mbuzi nk, kazi yake ni kumeng'enya mafuta ndani ya utumbo mwembamba, ndani ya utumbo mwemba ndimo usagaji wa chakula hufanyika.

Mamba hula vyakula vyenye protein na mafuta hivyo nyongo inamsaidia kuyeyusha mafuta yatokanayo na vyakula anavyokula.

Nyongo (bile) ni digestive juice.

Watu wengi wenye imani kwamba nyongo ya mamba ni sumu hao utakuta wamekulia katika imani za kishirikina na uchawi.

Kama nyongo hiyo ingekuwa ni sumu mbona yeye mwenyewe mamba si angekufa kabla ya kuua watu wengine au hata nyama yake isingekuwa inaliwa au hata kinyesi chake kingekuwa ni hatari na sumu kubwa.

Tumieni akili kuliko kupinga kijinga kwa kufuata mkumbo tu.

Angalia ndani ya Google uone watu waliofanya hizo tafiti.

Crocodile bile lethal poison??
 
Sasa mtu akikupa kinywaji halafu baada ya dakika 10 ukakata moto watu si wataanza kudeal na aliyekupa kinywaji?
Hii sumu si kwamba mshirikina peke yake anaitumia isipokua hata mtu baki anaweza kutumia kuhusu ufanyaji kazi inaenda kushambuliwa Ini,hapa katika ini hutofautiana na wingi wa sumu akitaka ufe taratibu anakuwekea kidgo maximum hhuwezi kuzidi miezi 9,unafariki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…