Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 8,323
- 18,051
Ni kama unalazimisha kusawazisha ukweli ufanane na fikra zako jambo ambalo si kweli. Kwa sasa tuonger ukweli, women born from the late 1980's kuja huku 2000 lack that important characteristics set that makes them women to men.Wengi humu kinachowakuta ni kuutamani msiba wa wengi, kutafuta pa kupumulia baada ya kukutana na vipigo vya wanawake wa mjini. Tamanio la kiubinadamu kuwa si mimi tu, kuna yule na huyu na yule.
Ndo maana ukiingiza "mama" wanatoa exception za mama zao, utasikia ukitoa mama yangu, wanasahau kuwa huyo mama yake ni mwanamke wa baba yake si mwanamke wake, na pengine ameshawahi kuwa na mwanaume akamfilisi kabla hajakutana na baba yake na kuwa mama kwake.
Maisha hayapo fixed kuwa njia ni hii. Watu wanabadilika, Unakutana na mwanamke mhuni wa leo kwako ila ni malaika wa kesho kwa mwanaume mwingine.
Unakutana na mwanamke malaika wa leo kwako anageuka mhuni wa kesho kwa mwanaume mwingine au unakutana na malaika mwanzo mwisho au vice versa hakuna general rule.
Wapo wanaume wamefanikiwa kupitia wanawake, wapo wanaume wamefilisiwa na wanawake, wapo wanaume wamewadhulumu wanawake mali zao kwa jina la mapenzi.
Wapo wanawake wanataka fedha zako tu, na wapo wanawake wanataka uwe baba kwa familia na akakuvumilia hata ukiwa huna kitu na akanyanyuka na wewe unapokuwa na kitu.
Kizazi hiki cha sasa cha wanawake wanachokileta katika maisha ya mwanaume si support bali changamoto zao personal. Na ndio maana single mothers ni wengi sana na mabinti ambao wanajinasibu kuwa ni single ila behind the scenes wagongwa na wanaume hata watano kwa wakati m'moja ni wengi sana.