Mohammed Khatibu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2018
- 1,170
- 1,617
Nguruvi3 umenena vyema!
Kuna wakati aliyekuwa Jaji Mkuu aligombea Urais kupitia CCM. Nani alijua kuwa Jaji alikuwa na kadi ya CCM!! HakunaInashangaza! Kwamba katiba aliyoilalamikiwa leo anaaminisha umma'' imefanyiwa kazi ''Hata kuziungumzia katika ''uzuri' aliouona hakuthubutu
!Hili nalirudia tena, ni mmoja wa walioamsha hamasa ya wananchi kushiriki siasa na kuhoji serikali bila woga.
Niliwahi kuandika hapa JF, uamuzi wa kuachana na Chadema kwa kutokubaliana na yanayoendelea ulikuwa ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu sana na mfano kwa vijana
Kwamba, kama kuna asiyeridhika na maamuzi ni vema akaheshimu msimamo wake na kusimama na kile anachoamini. Nilimpongeza
Baada ya hapo, Dr akaungana na akina Mwaky kwenda Sheraton kuzungumzia mambo tofauti na yale yaliyosababisha akaachia ngazi, hatua mbaya na mbovu kabisa.
Nilimweleza, heshima aliyoijenga kwa miaka na gharama kubwa itaporomoka.
Ni vema angetulia ili historia imhukumu.
Leo maneno yale yale yanamrudi kuliko mazuri mengi aliyofanya.
Kwa bahati mbaya hakujifunza kutokana na kosa la awali.
Dr Slaa aliwahi lalamikia vinasa sauti ktk godoro kule Dodoma. Umma ulilaani kitendo hicho.
Dr Slaa huyo huyo anaona mtu kupigwa risasi ni jambo la kawaida kuliko vinasa sauti alivyowekewa. Hapa ndipo heshima yake ilipofika 'rock bottom'
Kuandika kitabu kwa rekodi sioni tatizo ikiwa kufanya hivyo kutakuwa na tija katika jamii
Kama ni kwa biashara, timing ni mbaya.Hali ya kisiasa inakifanya kionekana ''uchochezi'' !!
Pili, akiwa na magwanda ya kijani kinachoeleza magwanda ya khaki si mkakati mzuri.
Tatu, kauli zake za hivi karibuni zinazopingana na kile alichosimamia hazisaidiii mauzo.
Kama ''abstract'' ni hiyo ya MM, nachelea kusema kitabu kitaongelea migogoro zaidi kuliko demokrasia aliyosimamia kwa nguvu. Tuna migogoro ya kutosha! Nahitaji kusoma kitu tofauti.
