Nyumba iliyojengwa na Bushiri Ali Harthi bado iko Pangani mkoa wa Tanga

Huyu bushiri asili yake ni wa wapi?

Ova
Al Bashir ibn Salim al-Harthi also known by the name Abushiri was a wealthy merchant and plantation owner of Omani Arab parentage who is known for the Abushiri Revolt against the German East Africa Company in present-day Tanzania.Wikipedia

1635981568594.jpeg
 
Sidhani ameuza. Amenunua maana alihitaji watumwa ilhali biashara yake ilikuwa hasa kuendesha shamba lake lililolimwa na watumwa. Eneo lote la mdomo wa mto Pangano lilikuwa na eneo la kulima miwa na kuzalisha sukari kwa kuuza nje ya nchi.
Waliouza watumwa walikuwa machifu wa makabila ya ndani.
Simulizi hilo eti Waarabu wabaya walikamata Waafrika maskini ni kitoto kidogo, sivyo? Maana kimsingi si kweli (au angalau nusu kweli tu)
Bila shaka Waarabu kuwa tayari kununua watumwa wengi ilihamasisha watawala wengi wa Kiafrika kuongeza idadi ya wafungwa. Ama kwa njia ya vita dhidi ya majirani ili wapate wafungwa, au kwa kutumia malaka zao za kuhukumu watu wao utumwani kwa makoso yoyote.
Ila tu utumwa katika Afrika haukuanza kwa sababu ya Waarabu kuwa wateja.
You can never protect Arabs from slave trade period. Hata huyo Bwana mwenye jengo nae alikuwa Mwarabu. Acha theory zako potofu. Wajerumani walikuja hapa na kufuta biashara ya watumwa ambayo ilishamiri wakati wa utawala wa Waarabu. Hawasafishiki kirahisi hivyo.
 
Nyumba ya Bushiri Ali Harthi, iliyojengwa kwa Matumbawe na udongo, bado ina nguvu kama ilivyo, inayopatikana Pangani, mkoani Tanga. Nyumba ina basement, ambapo mazungumzo ya watumwa yamefichwa.

Bushiri alipigana vita na Wajerumani (Bushiri Revolt 1888 - 1889) na kushindwa sana, kukamatwa na kuhukumiwa hukumu ya kifo, kunyongwa tarehe 15 Dec 1889 huko Pangani.

_________

Bushiri Ali Harthi's House, built from Coral and clay, still strong as it is, found in Pangani, Tanga region. The house has basement, where a chattel of slaves hidden.

Bushiri fought a war with Germans (Bushiri Revolt 1888 - 1889) and desperately defeated, apprehended and sentenced to a death sentence, hanged on 15th Dec 1889 in Pangani.
Promotion ya site kama hizi ni ndogo sana
 
Sidhani ameuza. Amenunua maana alihitaji watumwa ilhali biashara yake ilikuwa hasa kuendesha shamba lake lililolimwa na watumwa. Eneo lote la mdomo wa mto Pangano lilikuwa na eneo la kulima miwa na kuzalisha sukari kwa kuuza nje ya nchi.
Waliouza watumwa walikuwa machifu wa makabila ya ndani.
Simulizi hilo eti Waarabu wabaya walikamata Waafrika maskini ni kitoto kidogo, sivyo? Maana kimsingi si kweli (au angalau nusu kweli tu)
Bila shaka Waarabu kuwa tayari kununua watumwa wengi ilihamasisha watawala wengi wa Kiafrika kuongeza idadi ya wafungwa. Ama kwa njia ya vita dhidi ya majirani ili wapate wafungwa, au kwa kutumia malaka zao za kuhukumu watu wao utumwani kwa makoso yoyote.
Ila tu utumwa katika Afrika haukuanza kwa sababu ya Waarabu kuwa wateja.
Unaosha mkaa kwa sabuni?
 
DO NOT DISTORT THE East African HISTORY! THE ARABS WERE SLAVE TRADERS.
Kaka soma nilichoandika. Kweli kabisa walikuwepo Waarabu waliofanya biasharaya watumwa. Walikuwa muhimu sana kwa biashara hiyo. Ila katika kila biashara kuna angalau pande mbili. Anayenunua na anayeuza, sivyo?
Upande wa wauzaji Waafrika walikuwa wengi.
Kwenye miaka ya nusu ya pili ya karne ya 19 kuna pia taarifa za Waarabu waliokamata wafungwa (Kongo, Malawi), lakini ukitazama miaka yote hii haikuwa kawaida. Biashara hiyo inajulikana kuwepo tangu karne nyingi.

Idadi kubwa ya wafungwa waliuzwa na watawala wa bara, walikuwa ama wafungwa wa vita au watu waliohukumiwa kwa makosa mbalimbali.
Ila wakati faida ya kuuza watumwa iliongezeka pamoja na njaa ya bidhaa za nje, watawala walitumia sababu yoyote kumhukumu mtu awe mtumwa.
Ukiwa na habari tofauti, lete!
 
Ndugu zanguni,
Ikiwa mnataka historia ya utumwa ni vizuri sana mkasogea mbele na kusoma The Across Atlantic Slave Trade na Belgian Congo Slave Trade.
Mzee mheshimiwa,
kama ulitaka kudokeza kwamba katika kilio kuhusu biashara ya Waarabu (Waislamu) tusisahau biashara kubwa zaidi ya Wazungu (Wakristo), hii ni sawa ila biashara ya Kongo si mfano mzuri sana kwa kusudi lako.
Maana hapa tunamkuta Hamad bin Muhammad bin Juma bin Rajab el Murjebi (amejulikana zaidi kwa jina la Tippu Tip) kuwa sio mfanyabiashara ya watumwa pekee, lakini pia mvindaji wa watumwa katika Kongo (ambayo haikuwa kawaida kwa Waarabu), na pia yeye yule kama gavana wa mfalme wa Ubelgiji katika mashariki ya Kongo.

Mwana...
Ungechukua muda ukasoma historia hizo ungepata maarifa mengi na usingerudi hapa na hayo uliyoandika.

Ungeandika hapa maneno mazito kushinda hayo ya Tippu Tip.
Bahati mbaya umekuwa na haraka ya kunjibu.
 
Nyumba ya Bushiri Ali Harthi, iliyojengwa kwa Matumbawe na udongo, bado ina nguvu kama ilivyo, inayopatikana Pangani, mkoani Tanga. Nyumba ina basement, ambapo mazungumzo ya watumwa yamefichwa.

Bushiri alipigana vita na Wajerumani (Bushiri Revolt 1888 - 1889) na kushindwa sana, kukamatwa na kuhukumiwa hukumu ya kifo, kunyongwa tarehe 15 Dec 1889 huko Pangani.

_________

Bushiri Ali Harthi's House, built from Coral and clay, still strong as it is, found in Pangani, Tanga region. The house has basement, where a chattel of slaves hidden.

Bushiri fought a war with Germans (Bushiri Revolt 1888 - 1889) and desperately defeated, apprehended and sentenced to a death sentence, hanged on 15th Dec 1889 in Pangani.
Nilifika hapo Dada
 
Back
Top Bottom