Nyumba iliyojengwa na Bushiri Ali Harthi bado iko Pangani mkoa wa Tanga

Nyumba iliyojengwa na Bushiri Ali Harthi bado iko Pangani mkoa wa Tanga

Madam Sky,

Hivi hawa Kina Bakari na Juma Harith (Harthi) Mwapachu sio masalia ya huyu Al Bashir kweli ? Please if you can dive below headlines and enlighten us !
Hapana Harthi ni jina tu watu wengi wanalitumia.
 
Mungu katupa subra na upendo
Imagine kama tungeamua kulipa kisasi
Yaani jamaa walijua kuwatesa na kuwadhalilisha binadamu wenzao

Haitoshi na waliowachukua wakawaharibia mila na desturi zao

Inauma sana
Mutalipa kisasi kwa wangapi wakati hata machifu ambao baadhi ni mababu zenu walishiriki kwa kiwango kikubwa tu katika kuuza wenzao?

Tena wakiwauza kwa vipande vya vitambaa vya kaniki enzi zile.
 
Sidhani ameuza. Amenunua maana alihitaji watumwa ilhali biashara yake ilikuwa hasa kuendesha shamba lake lililolimwa na watumwa. Eneo lote la mdomo wa mto Pangano lilikuwa na eneo la kulima miwa na kuzalisha sukari kwa kuuza nje ya nchi.
Waliouza watumwa walikuwa machifu wa makabila ya ndani.
Simulizi hilo eti Waarabu wabaya walikamata Waafrika maskini ni kitoto kidogo, sivyo? Maana kimsingi si kweli (au angalau nusu kweli tu)
Bila shaka Waarabu kuwa tayari kununua watumwa wengi ilihamasisha watawala wengi wa Kiafrika kuongeza idadi ya wafungwa. Ama kwa njia ya vita dhidi ya majirani ili wapate wafungwa, au kwa kutumia malaka zao za kuhukumu watu wao utumwani kwa makoso yoyote.
Ila tu utumwa katika Afrika haukuanza kwa sababu ya Waarabu kuwa wateja.
Afadhali umeeleza vizuri maana hapa lawama zinakwenda upande mmoja tu. Sidhani kama ni sahihi. Lawama ziende kwa washiriki wote, watafutaji watumwa (machifu wa vijiji), wanunuzi na watumiaji.
 
Kaka soma nilichoandika. Kweli kabisa walikuwepo Waarabu waliofanya biasharaya watumwa. Walikuwa muhimu sana kwa biashara hiyo. Ila katika kila biashara kuna angalau pande mbili. Anayenunua na anayeuza, sivyo?
Upande wa wauzaji Waafrika walikuwa wengi.
Kwenye miaka ya nusu ya pili ya karne ya 19 kuna pia taarifa za Waarabu waliokamata wafungwa (Kongo, Malawi), lakini ukitazama miaka yote hii haikuwa kawaida. Biashara hiyo inajulikana kuwepo tangu karne nyingi.

Idadi kubwa ya wafungwa waliuzwa na watawala wa bara, walikuwa ama wafungwa wa vita au watu waliohukumiwa kwa makosa mbalimbali.
Ila wakati faida ya kuuza watumwa iliongezeka pamoja na njaa ya bidhaa za nje, watawala walitumia sababu yoyote kumhukumu mtu awe mtumwa.
Ukiwa na habari tofauti, lete!
Waarabu wote walikua wanafanya biashara ya watumwa kama si kuuza walikua wananunua na wengine walikua wanakusanya watumwa. Kwahiyo hamna mwarabu hapa tanzania ambaye babu yake hakuhusika kwenye biashara ya utumwa
 
Ndugu zanguni,
Ikiwa mnataka historia ya utumwa ni vizuri sana mkasogea mbele na kusoma The Across Atlantic Slave Trade na Belgian Congo Slave Trade.
Wazungu ndio walifanya biashara ya watumwa wala hatukatai ila hapa kwetu tanzania waarabu ndip walikua vinara wa biashara ya utumwa na wareno mzee acha kutetea warabau kwasababu ya dini
 
Mzee mheshimiwa,
kama ulitaka kudokeza kwamba katika kilio kuhusu biashara ya Waarabu (Waislamu) tusisahau biashara kubwa zaidi ya Wazungu (Wakristo), hii ni sawa ila biashara ya Kongo si mfano mzuri sana kwa kusudi lako.
Maana hapa tunamkuta Hamad bin Muhammad bin Juma bin Rajab el Murjebi (amejulikana zaidi kwa jina la Tippu Tip) kuwa sio mfanyabiashara ya watumwa pekee, lakini pia mvindaji wa watumwa katika Kongo (ambayo haikuwa kawaida kwa Waarabu), na pia yeye yule kama gavana wa mfalme wa Ubelgiji katika mashariki ya Kongo.

Mzee huyu ni mdini .. yupo kwenye denial kuwa waarabu(waislamu) kuhusika kwenye biashara ya utumwa
 
Madam Sky,

Hivi hawa Kina Bakari na Juma Harith (Harthi) Mwapachu sio masalia ya huyu Al Bashir kweli ? Please if you can dive below headlines and enlighten us !
Harith ni jina la 'me, Al Harthi ni moja kati ya makabila ya waarabu.
 
Al Bashir ibn Salim al-Harthi also known by the name Abushiri was a wealthy merchant and plantation owner of Omani Arab parentage who is known for the Abushiri Revolt against the German East Africa Company in present-day Tanzania.Wikipedia

View attachment 1997835

Allah amrehemu ndugu yetu sheikh Al bashir na amuingize katika pepo ya firdaus,,,Aamiin.
 
Nyumba ya Bushiri Ali Harthi, iliyojengwa kwa Matumbawe na udongo, bado ina nguvu kama ilivyo, inayopatikana Pangani, mkoani Tanga. Nyumba ina basement, ambapo mazungumzo ya watumwa yamefichwa.

Bushiri alipigana vita na Wajerumani (Bushiri Revolt 1888 - 1889) na kushindwa sana, kukamatwa na kuhukumiwa hukumu ya kifo, kunyongwa tarehe 15 Dec 1889 huko Pangani.

_________

Bushiri Ali Harthi's House, built from Coral and clay, still strong as it is, found in Pangani, Tanga region. The house has basement, where a chattel of slaves hidden.

Bushiri fought a war with Germans (Bushiri Revolt 1888 - 1889) and desperately defeated, apprehended and sentenced to a death sentence, hanged on 15th Dec 1889 in Pangani.

Wazungu mnawashobokea but hawakuwa watu wazuri,,,,
 
Wazungu mnawashobokea but hawakuwa watu wazuri,,,,
Biashara ya utumwa iliendelezwa na Ottomans, soko kubwa la awali lilikua Misri mpaka Arabuni. Wazungu walianza kununu watumwa baada ya kupata makoloni na kuanza kulima kuanzia Brazil, Mexico, Jamaica mpaka North America.
 
Historia haibadiliki ila inatufunza tusirudie makosa. Ni kweli kabisa.

Hivi kuna historia haibadiliki inapotakiwa kubadilishwa!!! Wazungu walikuwa washenzi sana, wakiamuwa kuibadilisha historia ili waonekane walikuwa wema sana na kuwachafuwa waarabu watashindwaje!!!!! Endeleeni kufata vihistoria vya mzungu ndiyo kawaida yenu kuamini vya mzungu na kupuuza vya wengine 😁

Mimi huwa nawachana live tuu
 
Biashara ya utumwa iliendelezwa na Ottomans, soko kubwa la awali lilikua Misri mpaka Arabuni. Wazungu walianza kununu watumwa baada ya kupata makoloni na kuanza kulima kuanzia Brazil, Mexico, Jamaica mpaka North America.

Lazima muwasakame na kuwazushia waisilamu, tangu lini muzungu akawa mzuri kwa waturuki, waarabu na waisilamu kwa ujumla!!! Huyo mzungu atakuwa mpumbavu kiac gani aandike ama a2nge historia ya uovu wao icpokuwa upotoshaji dhidi ya waarabu na waislamu kwa ujumla ili tuu waonekane wabaya!!

Daima waga siamini vijihistoria vya muzungu, kuna sheik hapo darisalama amefafanuwa vizuli sana kuhusu utumwa uriofanywa na wazungu, nikipata clipu yake nitakutagi bibie
 
Biashara ya utumwa iliendelezwa na Ottomans, soko kubwa la awali lilikua Misri mpaka Arabuni. Wazungu walianza kununu watumwa baada ya kupata makoloni na kuanza kulima kuanzia Brazil, Mexico, Jamaica mpaka North America.
Wazungu waligawana Africa (makoloni) mwaka gani? Utawala wa ottoman ulianza kwaka gani?
 
Wazungu waligawana Africa (makoloni) mwaka gani? Utawala wa ottoman ulianza kwaka gani?

Origins of the Ottoman Empire​

Osman I, a leader of the Turkish tribes in Anatolia, founded the Ottoman Empire around 1299. The term “Ottoman” is derived from Osman’s name, which was “Uthman” in Arabic.

The Ottoman Turks set up a formal government and expanded their territory under the leadership of Osman I, Orhan, Murad I and Bayezid I.

The Ottoman Empire was one of the mightiest and longest-lasting dynasties in world history. This Islamic-run superpower ruled large areas of the Middle East, Eastern Europe and North Africa for more than 600 years. The chief leader, known as the Sultan, was given absolute religious and political authority over his people. While Western Europeans generally viewed them as a threat, many historians regard the Ottoman Empire as a source of great regional stability and security, as well as important achievements in the arts, science, religion and culture.
 
Nyumba ya Bushiri Ali Harthi, iliyojengwa kwa Matumbawe na udongo, bado ina nguvu kama ilivyo, inayopatikana Pangani, mkoani Tanga. Nyumba ina basement, ambapo mazungumzo ya watumwa yamefichwa.

Bushiri alipigana vita na Wajerumani (Bushiri Revolt 1888 - 1889) na kushindwa sana, kukamatwa na kuhukumiwa hukumu ya kifo, kunyongwa tarehe 15 Dec 1889 huko Pangani.

_________

Bushiri Ali Harthi's House, built from Coral and clay, still strong as it is, found in Pangani, Tanga region. The house has basement, where a chattel of slaves hidden.

Bushiri fought a war with Germans (Bushiri Revolt 1888 - 1889) and desperately defeated, apprehended and sentenced to a death sentence, hanged on 15th Dec 1889 in Pangani.

Nilivuoona Title Nikajua Dr Bashiru Ali ameporomosha Mansion Tanga.
 
Back
Top Bottom