Kaka Mwarabu alipata wapi wafungwa ili kuwapeleka Unguja? Nani alimwuzia?
Ukifika Bagamyo, ingia makumbusho pale kanisa katoliki. Utaona habari za watu wengi waliokuwa watumwa . Mara kwa mara utaona walizaliwa sehemu za Kilimajaro, Usambara, Lindi ,,,,,, Mtu aliweza kufungwa na kuuzwa baada ya kushtakiwa katika jamii yake eti ni mwizi, mzinzi, mchawi . . . . Kuna watoto waliouzwa kwa sababu wazazi walikuwa na madeni .. .
Unapata viongozi kama Mirambo waliouza wafungwa wa vita ili wapate hela kwa ajili ya silaha . . . Hao wote waliolisha soko la watumwa. Kwa Mirambo (wengine wanapenda kukumbuka kama "shujaa") msingi wa jeshi alilojenga ulikuwa faida alizowahi kupata kama mwendesha misafara ya meno ya ndovu pamoja na watumwa baina Ziwa Tanganyika na pwani. Alikuwa na akili ili asiache biashara hiyo kwa Waarabu.
Je unahitaji mifano zaidi?