Nyumba iliyojengwa na Bushiri Ali Harthi bado iko Pangani mkoa wa Tanga

You can never protect Arabs from slave trade period. Hata huyo Bwana mwenye jengo nae alikuwa Mwarabu. Acha theory zako potofu. Wajerumani walikuja hapa na kufuta biashara ya watumwa ambayo ilishamiri wakati wa utawala wa Waarabu. Hawasafishiki kirahisi hivyo.
 
Promotion ya site kama hizi ni ndogo sana
 
Unaosha mkaa kwa sabuni?
 
DO NOT DISTORT THE East African HISTORY! THE ARABS WERE SLAVE TRADERS.
Kaka soma nilichoandika. Kweli kabisa walikuwepo Waarabu waliofanya biasharaya watumwa. Walikuwa muhimu sana kwa biashara hiyo. Ila katika kila biashara kuna angalau pande mbili. Anayenunua na anayeuza, sivyo?
Upande wa wauzaji Waafrika walikuwa wengi.
Kwenye miaka ya nusu ya pili ya karne ya 19 kuna pia taarifa za Waarabu waliokamata wafungwa (Kongo, Malawi), lakini ukitazama miaka yote hii haikuwa kawaida. Biashara hiyo inajulikana kuwepo tangu karne nyingi.

Idadi kubwa ya wafungwa waliuzwa na watawala wa bara, walikuwa ama wafungwa wa vita au watu waliohukumiwa kwa makosa mbalimbali.
Ila wakati faida ya kuuza watumwa iliongezeka pamoja na njaa ya bidhaa za nje, watawala walitumia sababu yoyote kumhukumu mtu awe mtumwa.
Ukiwa na habari tofauti, lete!
 
Ndugu zanguni,
Ikiwa mnataka historia ya utumwa ni vizuri sana mkasogea mbele na kusoma The Across Atlantic Slave Trade na Belgian Congo Slave Trade.
Mzee mheshimiwa,
kama ulitaka kudokeza kwamba katika kilio kuhusu biashara ya Waarabu (Waislamu) tusisahau biashara kubwa zaidi ya Wazungu (Wakristo), hii ni sawa ila biashara ya Kongo si mfano mzuri sana kwa kusudi lako.
Maana hapa tunamkuta Hamad bin Muhammad bin Juma bin Rajab el Murjebi (amejulikana zaidi kwa jina la Tippu Tip) kuwa sio mfanyabiashara ya watumwa pekee, lakini pia mvindaji wa watumwa katika Kongo (ambayo haikuwa kawaida kwa Waarabu), na pia yeye yule kama gavana wa mfalme wa Ubelgiji katika mashariki ya Kongo.

 
Mwana...
Ungechukua muda ukasoma historia hizo ungepata maarifa mengi na usingerudi hapa na hayo uliyoandika.

Ungeandika hapa maneno mazito kushinda hayo ya Tippu Tip.
Bahati mbaya umekuwa na haraka ya kunjibu.
 
Nilifika hapo Dada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…