Nyumba iliyojengwa na Bushiri Ali Harthi bado iko Pangani mkoa wa Tanga

Unadhani waarabu ni ndugu zako?
 
Liber...
Nilichosema ni kuwa ikiwa tutahangaishwa na utumwa wa Zanzibar na tukaacha kusoma historia nyingine ya utumwa tutakuwa hatuna elimu ya kutosha kufanya mjadala.

Bahati mbaya unanishambulia.
 
Liber...
Nilichosema ni kuwa ikiwa tutahangaishwa na utumwa wa Zanzibar na tukaacha kusoma historia nyingine ya utumwa tutakuwa hatuna elimu ya kutosha kufanya mjadala.

Bahati mbaya unanishambulia.
Mzee Mohamed Said tatizo lako kubwa ni kuhangaika kuwanasua Waarabu kwenye jinai ya uhalifu dhidi ya binadamu kwa biashara yao haramu ya utumwa waliofanya. Wazungu wameifanya hiyo jinai pia and it's well documented kila mahala.
Shida yako wewe ni kwamba unadhani wakitajwa Waarabu kwenye jinai hii unadhani kinachotajwa ni dini ya Kiislamu kitu ambacho ni upotofu.
Impliedly wewe kwa hulka yako ya kuhangaika kuwanasua Waarabu kwenye jinai hiyo ndiye unajikuta unaunasibisha Uislam na jinai hiyo kitu ambacho si sahihi.
Wazungu walifanya hiyo jinai on their own, na hiyo jinai yao has nothing at all to do with their faiths.
Mimi kwa unyenyekevu ninakushauri, wacha Uislam usimame peke yake kama imani bila kuunasibisha na Uarabu. Waache Waarabu wajitetee wenyewe kuhusu hii jinai waliyoifanya dhidi ya ubinadamu bila kuwanasibisha na Uislam
 
Nitajie hao waafrika huku tanzania walikua waarabu au machotara wa kiarabu. Huku sisi hatujawahi uzana ni baada ya ukoloni ndio tumekuwa mazipe zipe tunauza nchi yetu
Kaka Mwarabu alipata wapi wafungwa ili kuwapeleka Unguja? Nani alimwuzia?

Ukifika Bagamyo, ingia makumbusho pale kanisa katoliki. Utaona habari za watu wengi waliokuwa watumwa . Mara kwa mara utaona walizaliwa sehemu za Kilimajaro, Usambara, Lindi ,,,,,, Mtu aliweza kufungwa na kuuzwa baada ya kushtakiwa katika jamii yake eti ni mwizi, mzinzi, mchawi . . . . Kuna watoto waliouzwa kwa sababu wazazi walikuwa na madeni .. .

Unapata viongozi kama Mirambo waliouza wafungwa wa vita ili wapate hela kwa ajili ya silaha . . . Hao wote waliolisha soko la watumwa. Kwa Mirambo (wengine wanapenda kukumbuka kama "shujaa") msingi wa jeshi alilojenga ulikuwa faida alizowahi kupata kama mwendesha misafara ya meno ya ndovu pamoja na watumwa baina Ziwa Tanganyika na pwani. Alikuwa na akili ili asiache biashara hiyo kwa Waarabu.

Je unahitaji mifano zaidi?
 
Naona upande mwigine wa Afrika (Afrika Magharibi) majadiliano ni tofauti kuliko hapa. Labda vitabu vyao vya shule ni bora?
Ona African President apologizes for Africans selling Black People to Whites .

Soma: BENIN OFFICIALS APOLOGIZE FOR ROLE IN U.S. SLAVE TRADE

Soma: The Civil Rights Congress of Nigeria has written to tribal chiefs saying: "We cannot continue to blame the white men, as Africans, particularly the traditional rulers, are not blameless."
(je, ni kweli pia kuhusu Waarabu na Afrika Mashariki? Maana ukinyosha kidole dhidi yao, vidole vingapi vinaelekea nyuma kwa historia ya Afrika?)
 
Mungu katupa subra na upendo
Imagine kama tungeamua kulipa kisasi
Yaani jamaa walijua kuwatesa na kuwadhalilisha binadamu wenzao

Haitoshi na waliowachukua wakawaharibia mila na desturi zao

Inauma sana
unalipa kisasi kwa nani maana wote wameshakufa
 
Huyu kiongozi hakuna hata kumbukumbu ya jina lake Kama shule, barabara, hospitali au chochote tu
Yaani tumuenzi mtu aliyekuwa akifanya biashara ya watumwa? Ni sawa Sky Eclat anavyosema kwamba historia haina budi kusemwa kama ilivyotokea. Lakini si sahihi kwako Nditolo kudai tuienzi historia mbaya ya Bushiri kwa kuiipa jina lake shule, barabara au hospitali.
 
unalipa kisasi kwa nani maana wote wameshakufa

Hayo yamepita hatuwezi kufanya hivyo
Lakini hebu angalia kuna mataifa mpaka leo bado wanapigana tangu enzi na enzi
Unafikiri visasi hakuna kwenye dunia hii hata kama waliofanya na kufanyiwa wamekufa?
 
Kumbe, Dar es Salaam uko Mtaa wa Mirambo. Bushiri alimilki watumwa, sijui sasa kama aliendesha biashara ya watumwa, lakini Mirambo alifanya biashara ya watumwa hakika. Kuwakamata, kuwanunua, kuwauza. Mtaa anao, sijui mingapi?
 
Slave trade ilikuwa mbaya sana na hatari kabisa. Upande huu wa bara la Africa(east) slaves wengi waliuzwa Arab countries. Na waarabu wakawahasi babu zetu iliwasizaliena ndio maana hata sasa huwezi kukuta watu weusi nchi za kiarabu huu ulikuwa unyama usiofikirika. Unlike Arabs upande ule wa magharibi watumwa wengi walipelekwa America na carribean waafrica wapo nchi hizo hadi leo wanaishi. Kwenye modern slavery ndio usiseme kwa wafrica wanaoenda kufanya kazi za ndani in Arab countries ndio wanaoteswa zaidi duniani ikiwamo kunyufolewa viungo vya mwili kama figo, moyo na inni very sad.
 
Bushiri bwana heri, huyu mwamba nilimsomaga kwenye historia, ila tusiwe wanafki mababu zetu nao walikua wazembe sana kugeuzwa watumwa.
 

Pitia YouTube kucheki jinsi Slaves wanavyoteswa hapo Nchi ya Libya
 
Saudia wko weusi wengi. Ona
 
Shida ya hapa kwetu tunakariri yale tuliyoambiwa tu, na kwa bahati mbaya tuliambiwa nusu tu ya hadithi yenyewe.
 
He! wacha uongo wa vijiweni wewe!
 
ni kweli kuna editing imefanyika, mwaka 1880 sidhani kulikuwa na mabati ya aina hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…