Mangungo II
JF-Expert Member
- Jul 6, 2012
- 18,133
- 26,766
Bushiri alikuwa mfanyabiashara wa utumwaHuyu kiongozi hakuna hata kumbukumbu ya jina lake Kama shule, barabara, hospitali au chochote tu
Anauza na kununua watu
Pia na biashara zingine
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bushiri alikuwa mfanyabiashara wa utumwaHuyu kiongozi hakuna hata kumbukumbu ya jina lake Kama shule, barabara, hospitali au chochote tu
Mohamed said atakuambia Faida yakeSijui kama Mtanzania tunajivunia nini hapo. Huyo bwana alikuwa anafanya biashara ya kuwauza babu zetu.
La Milambo (na siyo Mirambo) kufanya biashara ya watumwa: kuwakamata, kuwanunua na kuwauza, nalisikia kwa mara ya kwanza kwako. Milambo alikuwa mtemi (chief), kama walivyokuwa Mkwawa, Marealle, n.k. Watemi walikuwa hawafanyi kazi. Watu (subjects) wao ndio walikuwa wakiwalimia mashamba na kuwafanyia kazi zigine zote. Kuibuka kuwa mtemi ni kwa kuzaliwa tu kwenye ukoo huo, na si kwa kujiendeleza hadi upate sifa zinazostahili. Hizo ndizo kasoro alizoziona Nyerere, na mwaka 1963 akafutilia mbali utemi, pamoja na kwamba hata yeye mwenyewe alikuwa mzaliwa wa ukoo wa kitemi na angeweza kuwa mtemi siku za usoni.Kumbe, Dar es Salaam uko Mtaa wa Mirambo. Bushiri alimilki watumwa, sijui sasa kama aliendesha biashara ya watumwa, lakini Mirambo alifanya biashara ya watumwa hakika. Kuwakamata, kuwanunua, kuwauza. Mtaa anao, sijui mingapi?
Wengi, kwa asilimia ngapi ya wananchi wote? Labda 1% walionusurika chujio. Nimekaa Uarabuni kwa miaka mitatu. Kwa hiyo ninafahamu ninachokisema. Marekani watu weusi wanafikia 10% ya Wamarekani wote.Saudia wko weusi wengi. OnaH![]()
Data za wapi na unalinganisha kwa kipindi gani? Transatlantic slave trade ilichukuwa muda wa miaka 400 (16th - 19th Century), na ilisafirisha kiasi ya waafrika million 12 (google info). Pia wao walikuwa wakifanya breeding ya binaadamu ili wapate watoto wa kinegro wakubwa na wenye nguvu kwa ajili ya kufanya kazi mashambani.Niweke data na picha? Ila Arabs ndio waliotuletea Dini yangu ya Kiislam hilo ndio mengine mhuu.
Hata kama hujasikia: Mirambo anajulikana sana kama mfanyabiashara wa meno za ndovu (hasa) pamoja na watumwa. Labda wenyeji wa huko wanapendelea kusahau sehemu hiyo ya historia yake.La Milambo (na siyo Mirambo) kufanya biashara ya watumwa: kuwakamata, kuwanunua na kuwauza, nalisikia kwa mara ya kwanza kwako. Milambo alikuwa mtemi (chief), kama walivyokuwa Mkwawa, Marealle, n.k. Watemi walikuwa hawafanyi kazi. Watu (subjects) wao ndio walikuwa wakiwalimia mashamba na kuwafanyia kazi zigine zote. Kuibuka kuwa mtemi ni kwa kuzaliwa tu kwenye ukoo huo, na si kwa kujiendeleza hadi upate sifa zinazostahili. Hizo ndizo kasoro alizoziona Nyerere, na mwaka 1963 akafutilia mbali utemi, pamoja na kwamba hata yeye mwenyewe alikuwa mzaliwa wa ukoo wa kitemi na angeweza kuwa mtemi siku za usoni.
Milambo hakuwa tofauti na watemi wengine. Kusema kwamba alikuwa akifanya biashara ya watumwa ni ajabu sana. Sijui kama kuwafanyisha watu wake kazi ndiko unakuita kufanya biashara ya watumwa. Ni kweli kwamba alikuwa mpiganaji hodari wa vita. Waarabu hawakuweza kamwe kuchukuwa watumwa ndani ya himaya yake. Hata misururu ya watumwa iliyokuwa ikitokea Kongo haikuruhusiwa kupita kwenye himaya yake mpaka ilipiwe hongo na Mwarabu mwenye msafara. Sijui kama hiyo pia ndiyo unaiita kufanya biashara ya watumwa. Mwarabu ndiye alidiriki kukamata babu zetu, kuwafunga minyororo, na kuwasafirisha hadi Uarabuni kupitia Bagamoyo. Sikioni kabisa kisa cha kung'ang'ania kumuenzi mtu aliyetufanyia unyama huo.
Yale niliyoona mimi UAE na Saudia ni asilimia kubwa zaidi. Si ajabu, maana hata kama walihasa sehemu ya watumwa wanaume, walizaa na wanawake watumwa. Hapo utumwa wa Waarabu ulikuwa tofauti na wale Wazungu Waprotestanti wa Marekani: mara mtumwa alikuwa Mwislamu aliweza kupokelewa katika jamii, na watoto wa mama mtumwa walitambuliwa kama watoto. Jamii yao haikuwa na ubaguzi mkali kama Marekani walipofuata "1-drop-rule", yaani kama mtu alionekana alikuwa na na babu Mwafrika alibaki "black" .Wengi, kwa asilimia ngapi ya wananchi wote? Labda 1% walionusurika chujio. Nimekaa Uarabuni kwa miaka mitatu. Kwa hiyo ninafahamu ninachokisema. Marekani watu weusi wanafikia 10% ya Wamarekani wote.
Umeandika ukweli mtupuLa Milambo (na siyo Mirambo) kufanya biashara ya watumwa: kuwakamata, kuwanunua na kuwauza, nalisikia kwa mara ya kwanza kwako. Milambo alikuwa mtemi (chief), kama walivyokuwa Mkwawa, Marealle, n.k. Watemi walikuwa hawafanyi kazi. Watu (subjects) wao ndio walikuwa wakiwalimia mashamba na kuwafanyia kazi zigine zote. Kuibuka kuwa mtemi ni kwa kuzaliwa tu kwenye ukoo huo, na si kwa kujiendeleza hadi upate sifa zinazostahili. Hizo ndizo kasoro alizoziona Nyerere, na mwaka 1963 akafutilia mbali utemi, pamoja na kwamba hata yeye mwenyewe alikuwa mzaliwa wa ukoo wa kitemi na angeweza kuwa mtemi siku za usoni.
Milambo hakuwa tofauti na watemi wengine. Kusema kwamba alikuwa akifanya biashara ya watumwa ni ajabu sana. Sijui kama kuwafanyisha watu wake kazi ndiko unakuita kufanya biashara ya watumwa. Ni kweli kwamba alikuwa mpiganaji hodari wa vita. Waarabu hawakuweza kamwe kuchukuwa watumwa ndani ya himaya yake. Hata misururu ya watumwa iliyokuwa ikitokea Kongo haikuruhusiwa kupita kwenye himaya yake mpaka ilipiwe hongo na Mwarabu mwenye msafara. Sijui kama hiyo pia ndiyo unaiita kufanya biashara ya watumwa. Mwarabu ndiye alidiriki kukamata babu zetu, kuwafunga minyororo, na kuwasafirisha hadi Uarabuni kupitia Bagamoyo. Sikioni kabisa kisa cha kung'ang'ania kumuenzi mtu aliyetufanyia unyama huo.
Yule huwa anajitoa ufahamu ni mtumwa wa waarabuMohamed said atakuambia Faida yake
Unajuaje? Lete ushahidiUmeandika ukweli mtupu
55⁸⁸ý
[QUOTE1zah="koro-boy, post: 40692437, member: 456654"]Sijui kama Mtanzania tunajivunia nini hapo. Huyo bwana alikuwa anafanya biashara ya kuwauza babu zetu.
Utumwa ulianza kuyumba kuanzia 1822 na kuwa haramu 1873.Je kuna ushahidi gani? Nyumba jinsi inavyoonekana ama imebadilishwa sana au si kweli. Wakati ule hawakujenga kwa namna hiyo. Nikiona paa, inawezekana kwa kutumia mabati tu. Zamani ile paa zote zilikuwa za makuti. Makuti haiwezekani kwa mtelemko kama huo.
Halafu watumwa wafiche ya nini? Utumwa ulikuwa halali hadi kuja kwa Wajerumani, hakuna haja ya kumficha mfungwa.
Hata kama wenyeji wanasimulia hadithi za aina hii, huwezi kuamini kila kitu.
Haikuwa vile. Mkutano wa Vienna kwenye mwaka 1815 ulitoa tamko la kwanza la kimataifa kukomesha biashara ya watumwa kutoka Afrika, lakini haikulenga utumwa mwenyewe bado. Harakati ya kukomesha utuma iliendelea katika nchi mbalimbali za Ulaya, hadi Uingereza kumaliza utumwa katika koloni zake zote kwenye mwaka 1838. Hata hivyo, utumwa uliendelea Marekani hadi 1865 na katika Brazil hadi mwaka 1888.Utumwa ulianza kuyumba kuanzia 1822 na kuwa haramu 1873.