Nyundo na wenzake wakutwa na hatia, wahukumiwa kifungo cha Maisha Jela

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
242
Reaction score
1,141
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, imewahukumu kifungo cha maisha gerezani washtakiwa wanne maarufu ‘waliotumwa na afande’, baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti, mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam.

Ni katika kesi ya jinai namba 23476 ya mwaka 2024 iliyokuwa inawakabili washtakiwa hao akiwamo MT 140105 Clinton Damas, maarufu Nyundo ambaye ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu, Septemba 30, 2024. Pia, Mahakama hiyo imewataka kila mmoja kumlipa binti huyo fidia ya Sh1 milioni.

Pia soma
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, imewahukumu kifungo cha maisha gerezani washtakiwa wanne maarufu ‘waliotumwa na afande’, baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti, mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam...
Safi sana ,hii itatoa fundisho kwa WASHENZI wengine wanaofanya ufirauni.
 
Kesi imesikilizwa kwa haraka mno maana yake walishahukumiwa kabla haijasikilizwa, na wahanga wa ubakaji wengine nao kesi zao hazisikilizwi haraka hivyo sababu hawakurekodiwa video na kurushwa ktk social medias!!

Ule unyama ni hatari ,wafungwe tu fasta ,kesi nyingine za ubakaji ni kusingiziwa tu kutokana na chuki ,ila ile vodeo kila kitu kinoanekana.
 
SASA MPUMZISHENI MAMA SAMIA MWENYE KUSIMAMIA HAKI. WALIKUWA WANAMCHAFUA KUWA SERIKALI YAKE HAITENDEI HAKI WATU. VIVA SAMIA . MITANO TENA . MIHIMILI YOTE IKO FAIR FAIR FAIR FAIR
Nyie ndio mnasababishwa Rais anatukanwa mana kumtaja kwenye mambo kama haya ndio kunaibua mengine ,ungetoa maoni yako bila kumtaja ungepungua nini au una lako jambo?
 
Back
Top Bottom