Nyundo na wenzake wakutwa na hatia, wahukumiwa kifungo cha Maisha Jela
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma (Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki) leo September 30,2024 imewahukumu kifungo cha maisha jela na faini ya milioni moja kila mmoja Washtakiwa wanne wakiwamo Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Magereza baada ya kuwakuta na hatia katika makosa yote mawili walioshtakiwa nayo la kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile Binti Mkazi wa Yombo Dovya, Jijini Dar es Salaam.

Kesi hii ya jinai namba 23476 ya mwaka 2024 ilikuwa inawakabili Washtakiwa wanne akiwamo MT 140105 Clinton Damas maarufu Nyundo ambaye ni Askari wa JWTZ, Askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.

Kesi hii maarufu ‘Waliotumwa na Afande’ imesikilizwa faragha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma ambapo upande wa Jamhuri uliwasilisha Mashahidi 18 na vielelezo 12 kuthibitisha mashtaka dhidi ya Washtakiwa.

Washtakiwa walifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza August 19, 2024 na kusomewa mashtaka mawili ya kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile Binti huyo ambaye Mahakamani anatambulika kwa jila la XY ambapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Zabibu Mpangule Washtakiwa hao baada ya kusomewa mashataka walikana na kutokana na unyeti wa kesi hiyo hawakupatiwa dhamana ambapo baada ya kesi kusikilizwa kwa siku kadhaa leo wamesomewa hukumu na kukutwa na hatia hivyo kuhukumiwa kifungo cha maisha.
 
SASA MPUMZISHENI MAMA SAMIA MWENYE KUSIMAMIA HAKI. WALIKUWA WANAMCHAFUA KUWA SERIKALI YAKE HAITENDEI HAKI WATU. VIVA SAMIA . MITANO TENA . MIHIMILI YOTE IKO FAIR FAIR FAIR FAIR
Bila shinikizo hii kesi ingeshakufa.

Usijitie wehu. Mwambie atueleze wapi alipo Soka na wengine.

Nani alimuua mzee Kibao.

BAWACHA wameanza kuchoma.vitenge vyenye picha yake nchi nzima
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki
imewahukumu kifungo cha maisha jela washtakiwa wanne baada ya kuwakuta na hatia katika makosa yote mawili walioshtakiwa nayo la kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile Binti Mkazi wa Yombo Dovya mkoani Dar es Salaam.

Kesi hiyo ilikuwa inawakabili washtakiwa wanne akiwamo MT 140105 Clinton Damas maarufu Nyundo ambaye ni askari wa Jeshi LA Ulinzi LA Wananchi wa Tanzania (JWTZ), askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson
'Machuche' na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la
Kindamba.

Kesi hiyo imesikilizwa faragha
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma ambapo upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi 18 na vielelezo 12 kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa.
 
Hatimaye haki imepatikana kwa binti huyo aliyefanyiwa unyama. Afande aliyewatuma hatma yake ni ipi?
Haki imepatikana kwa waharifu,......Binti kama alikua anajiuza aache,kama alikua anatembea na waume wa za watu,inabidi atubu,.........atakuja BOYA mmoja WA generation Z kumvisha Pete huku akibubujikwa na machozi,Binti aliyefir.rw.a vilivyo
C.C Natafuta Ajira
 
Iwe fundisho kwa wengine,

Starehe ya madakika tu inafanya maisha yako yote yaliyobaki yaishie Jela,

Hata siku moja usikubali kutumwa kwenda kufanya jinai ili kumfurahisha mwingine au kwa malipo,

Ur life belong to you and life is too short,

Sasa hivi wanajuta ila ndio imeshakua too late.
Bora ufukara na umasikini uraiani
 
Back
Top Bottom