Ofisi ya Kata wanashirikiana na baba yangu mzazi kuninyima haki yangu ya mali

Mzee lazima aingie kwenye lawama maana hajakuza vizuri ile spirit ya uchapaji kazi hakuiingiza ndani ya mwanae uyo ndio maana ana lilia mali.

Trust me Malezi yanachangia big time kumshape mtoto. Kama asifiwavyo mzazi pale mwanae afanyapo mazuri basi vice versa is true lawama ziende kwao kokote waliko
 
Komaaa mwanangu ukiweza kumuone Raisi. hii ni kesi ya uhujumu uchumi 🤣🤣🤣
 
Ungekuwa chini ya miaka 18 ungesaidiwa
usipoteze mda ndio nyie mnaua wazazi mpate uridhi mikono si unayo ungekuwa mlemavu sawa
 
Ni Kikohozi kweli kweli!
Mwenye mali anauza mali yake kuna mtu si mali yake anataka mgao utani huu.
Unatakiwa kupigwa na bomba la kufungulia tairi kichwani maana huna faida yoyote, labda uwe unafanya mzaha.
 
Ulivyoandika wengi hawajakuelewa, Mimi binafsi nimehangaika na familia ya Baba yangu, nimepoteza muda mwingi kuwahangaikia wadogo zangu na kaka zangu, nimewatafutia kazi wote, sasa hivi wana maisha mazuri sana. Lakini wote wamenitosa , hata kuwaona watoto wangu tu hawataki wanasema kila mtu ahangaike na mzigo iiiii
 
Ila Mungu mkubwa, sasa hivi wenyewe ndio wanakuja kuniomba msaada, nawaangalia tu, ila nawasidia ingawaje wanajisikia aibu. Mali za Baba nilisha waachia walinipa kadri walivyopenda.
Ila maisha yangu yanasonga kwa kiwango cha sgr
 
Nina waswas na maisha ya mzee....aisee maana watoto shetan anawatumia mbaya
 
Ushauri wa mwisho, wakatae watakutafuta, jasho la mtu halipotei kizembe
 
Nakubaliana na wewe mkuu malezi yanachangia pakubwa kumshape mtu tabia.
 
Ni Kikohozi kweli kweli!
Mwenye mali anauza mali yake kuna mtu si mali yake anataka mgao utani huu.
Unatakiwa kupigwa na bomba la kufungulia tairi kichwani maana huna faida yoyote, labda uwe unafanya mzaha.
Mkuu, nilichogundua kwa mtoa mada ni kwamba amechangia pakubwa kuendeleza familia, ila kuna baadhi ya ndugu hawana shughuli yoyote wameamua kumtenga kwa maana yeye ana uwezo. Ni shida moja mbaya sana.
 
Duh Mzee bado anakaza mkuu?[emoji3][emoji3]

Sasa dawa yake jinyonge ili aumie kukupoteza kwa sababu ya Tamaa zake za Mali.[emoji3]
 
Wewe jamaa nilikuambia kwenye thread ya mwanzo mambo ya msingi sana, kama unaweza naomba urudi ukasome. Usiposikia haya unayoambiwa, kuna siku utakuja kujuta sana.
Mind yako inakudanganya sana, utakuja kumchukia mzazi wako bure au kufanya kitendo kibaya zaidi kama kwenda kwa waganga au kumuua mzee wako. Wanaokushauri uendelee na unachofanya hawakutakii mema.
 
Kwa majibu ambayo mtoa mada aliyapata kwenye thread yake ya awali, sikutarajia kama angeandika uzi unaofanana na wa awali.

Kwa umri huo hata uende mahakama kuu, watasikiliza tu halafu waendelee na mengine. Huwezi pata chochote,maana haingii akilini udai mali ambazo sio zako. Ukizingatia mwenye mali yupo na afya tele.
 
Kisheria,Mali hizo no A babako na mamako. Hats ukienda mahakama gani hautapata chochote. Acha uvivu,tafuta vya kwako.
 
Miaka 42 una mke bado unalilia mali ya baba??.uyo mwanamke nae bado anakuvumilia tu
Kwani mkuu limesema lina mke? Kwanza miaka 42 siyo kijana huyo! Halafu inakuwaje miaka 42 bado linajambia makochi ya mzee tu? Mimi ningekuwa ndiye babake na hili tutusa ningelipeleka kwanza kupima DNA huenda siyo kitoto langu!
 
Nilianza kujitegemea mara tu nilipomaliza chuo bila kujalisha sina ajira na niwashukuru wazazi kwa urithi sahihi wa elimu walionipa.

Nakosa nikushauri nini ila unaidhalilisha elimu ya UDSM kwa upofu wa nawazo. Pambana kutafuta mali zako kaka acha uboya huo. Miaka 42 eti kijana?? Wewe ni mzee usie jielewa. Kwenye kuna shida sana hapa bongo
 
Pole sana baba ako anayo roho mbaya sana amepata zaidi ya milioni mia anashindwa hata kukupa milioni 2 kweli lakini inawezekana baba ako analishwa maneno na mtu wake wa karibu kama mama yako ni wakambo basi tegemea ndugu kukosa kabisa.kwa kweli ni aibu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…