Ofisi ya Rais – TAMISEMI Special Thread: Karibu tukuhudumie, tupe Maoni, Maswali, Mapendekezo na Malalamiko

Pole sana kwa changamoto hii tafadhali naomba utume raarifa za kutosha ili tuweze kufuatilia suala hili
Hivi mna mpango gani wa kulipa mapunjo ya mishahara kwa watumishi waliopanda vyeo 2015 , Mimi binafsi ni muathirika wa hiyo kadhia, ulienda halmashauri maafisa utumishi wanakuonesha kwenye mfumo kuwa walishashughulikia imebaki Tamisemi, miaka 10 sasa!
 
na ziliwasilishwa na Katibu Tawala Mkoa wako
Kipi kitakachonijuza Kuwa ametuma au la taarifa zangu?.
Kelele zote za watumishi zinaanzia hapa,tukitofautiana kiitikadi unahisi atatuma taarifa zangu?.

Ningelikuwa Mimi Ndo Tamisemi,nikifumba macho kabla sijafumbua nishaitoa hiyo kero.
 
Habar za leo ,nikuulizen kuhusu vyeo vya mserereko lakin hamjibu kabisa,Sasa changamoto ni nini?
 
Mwaka wa nane huu mke wangu anahangaikia uhamisho, amekuja dodoma zaidi ya mara tano, ameandika barua zikiwa na viambatanisho vyote muhimu lakini kupo,

Kwanini mnakua hivyo? Seriously miaka nane kuwa mbali na familia inauma sana, naombeni fanyeni kitu muiunganishe familia yangu
 
Karibuni Sana TAMISEMI Hapa JF
Kubwa Sana Watazameni Tanesco Ni Member Hapa Wana Hai Wao Wanajibu Maombi, Ushauri, Malalamiko. Msikae Kimya Toleeni Ufafanuzi Kila Jambo Hapa Hadharani
 
Mtumishi mwenye Mkataba namba Na. SMC/CW/PF.113/3 amefika Ofisini kwetu na ameomba tupaze sauti kwa niaba yake. Hii hapa historia fupi ya malalamiko yake.

Wakati wa zoezi la uhakiki wa Watumishi wa Umma 2016/2017 mwajiri wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga alizuia, kusitisha na Hatimaye kumwondoa kwenye malipo ya mshahara akiwa masomoni kwa Shahada ya kwanza katika moja ya vyuo vikuu hapa nchini. (Zingatia kuwa alikuwa na sifa zote kwenda masomoni na kwa ufadhili wa Mwajiri wake). Huyu Mtumishi alilalamikia hatua hiyo na baada ya uhakiki mwajiri alijiridhisha pasi na shaka kwamba;

1. Si Mtumishi hewa.
2. Alikuwa na Ruhusa Rasmi ya kwenda Masomoni.

CHANGAMOTO
Kwa kuwa mwajiri alishazuia, kusitisha na kumwondoa kwenye malipo ya mshahara tangu Januari 2017, imekuwa ni vigumu kumrejesha Kazini licha ya juhudi kubwa za ufuatiliaji wa mara kwa mara na kwa muda wote anazoendelea kuchukua kwa Muda wa miaka 7.

sasa! Ikumbukwe kwamba kati ya Julai na Disemba 2021, Ndugu, Jamaa na Marafiki walilazimika kumchangia Fedha za kuweka kambi Ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ili kukwamua shauri lake.

Kwa ujumla alifanikiwa kwa hatua kadhaa maana kamati ya nidhamu ilimuita kwa barua yenye Kumb. Na.SMC/CW/PF.118/6 na kumhoji kwa maneno na kwa Maandishi. Kamati hiyo iliahidi kutoa taarifa yake kwa Mkurugenzi ili nae atoe uamuzi wake kulingana na Taratibu.

OMBI LAKE KWA MAMLAKA HIZI
Anaomba Mamlaka zimsaidie kujua.
A) Mchakato uliotumika kuzuia, kusimamisha na Hatimaye kumwondoa kwenye malipo ya Mshahara January 2017.
B) Majibu ya Kamati ya Nidhamu chini ya Ofisi Mwajiri wake iliyomuita na kumhoji tarehe 11.11.2021 kwa Barua yenye Kumb.Na SMC/CW/PF.118/6
C) Endapo hatua A na B hapo juu hazikuzingatia Kanuni za Utumishi wa Umma, basi aruhusiwe kuendelea kutumikia mkataba wake wa Ajira kama ulivyo na Marekebisho yake.
D) Na iwapo alishaondolewa Kazini, ni haki ajulishwe kwa Barua Rasmi kulingana na Sheria, Taratibu na Kanuni za Kiutumishi.

IKUMBUKWE KUWA
Mheshimiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kwa waliokuwa watumishi hewa kurejeshewa sehemu ya iliyokuwa michango yao. Lakini kwa kesi ya Mtumishi huyu imekuwa ni vigumu maana si Mtumishi hewa na hana Barua yoyote inayoelezea hatima ya Mkataba wake vs Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.

Amejaribu kudai mafao yake PSSSF, Jambo hili nalo limekuwa gumu na kwa ufupi limeshindikana maana hana fao analoweza kuangukia.

TETESI ZILIZOPO KUHUSU UGUMU WA JAMBO HILI
Inasadikika kwamba Afisa Utumishi katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa wakati huo Bwana Shaphat Samuel Kaponela, alificha Jalada (Kama siyo kulipoteza kabisa) la Mtumishi huyu na hivyo kwa sasa inakuwa vigumu kwa Watendaji waliopo kufanya Uamuzi Sahihi.

Afisa huyo alichukua Uamuzi huo wa ajabu baada ya kubaini kuwa aliipotosha Mamlaka kufikia maamuzi ya kufaa. Kwa sasa Afisa huyo amehamishwa. Tunazo nyaraka nyingi kuhusiana na shauri hili na tunapanga namna ya kumsaidia huyu mwenzetu ili haki yake ipatikane maana Jambo hili limekuwa ni mateso kwake yeye na familia yake. Amerudi kwao kijijini na anajitafuta kutokea huko. Mamlaka na wadau mbalimbali mvusheni mwenzetu.
 
OR TAMISEMI , nitakuwepo hapa kusubiri majibu ya post hiyo hapo juu. Mawili, mnaweza kujibia hapa hapa au iko hiyo thread inajitegemea. Mnaweza kunijibu kwenye thread husika. Asanteni.
 
Hawajajipanga vizuri hawa TAMISEMI Wanajibu maswali kwa kuvizia au nao Wanauliza sehemu nyengine wakipewa majibu ndo wanakuja kujibu hapa. Ushauri TAMISEMI Jipangeni upya kisha mje sasa
 
Utaandika barua hadi uchakae, serikali kumejaa wala rushwa na wala sio haki.
 
We unayesubiri uhamisho usijipe matumaini sana,tangu january majibu ni yaleyale na ndo hawahawa customer care, unatumaje barua si utoe mkeka? barua zikifika halmashauri waanze kuzificha tena
 
Kuna hawa watu wanaitwa maafisa afya ni hovyo kabisa
  1. Wanakula sana rushwa kwa wamiliki wa bar, matangazo ya biashara na wauza CD kelele za miziki mijini zinaumiza sana ukiwafikishia malalamiko hawafanyi kazi yoyote.
  2. Kuna migahawa inauza vyakula vibovu vilivyolala hata siku mbili na kuzimuliwa na vyakula vipya, ukiwapa taarifa hawachukui hatua zozote
Napendekeza iwepo central numbe TAMISEMI ili malalamiko ya wananchi yawe yanapelekwa huko, kisha uongozi TAMISEMI utoe maagizo kwao na mwisho wa siku waombe taarifa za utekelezaji wa majukumu waliyopewa, wapimwe uwezo wao wa kazi tokea juu
 
Kabla sijafikisha malalamiko, naomba kuuliza, hivi hapa panahusika na malalamiko ya mitandao ya mawasiliano? Wengine hatuelewi category za sekta lakini tuna hoja muhimu sana
 
Natamani sana kuja kudeal na wala RUSHWA. Hawa watu ndio wanafanya nchi isiendelee...
 
Mimi nikijitahidi kuvumilia ni week 2 basi, napo nakuwa nafanya na issue nyingine, vinginevyo me nakosa huduma nahakikisha na yeye hana kazi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…