Lorenzo Samike
JF-Expert Member
- Jun 18, 2021
- 1,187
- 1,914
Unachokataa ni nini hapo? Kwani hazikufutwa?Nimeshangaa sana kuona mtu anaandika sheria kandamizi 40 alizozitaja Jaji Nyalali zimefutwa na Bill of Rights
Mwaka 1992, Tume ya Jaji Francis Nyalali ilikabidhi mapendekezo ya kuzitengua hizo sheria kwa Law Reform Commision, kisha Mwanasheria mkuu wa Serikali wa wakati huo akazipeleka Bungeni kwa ajili ya marekebisho kupitia WRITTEN LAWS MISCELLANEOUS (AMENDMENT BILL) 1994.
Nyingi zilifutwa na zingine zikarekebishwa.
Yote yameelezwa vyema kwenye HANSARD REPORT ya 29 November 1995. Page 732-734.
Haya yote yalifanyika baada ya kuja kwa Bill of Rights.
Bill of rights ndiyo iliyokuwa MIZANIA KUU ya KUPIMA ni kwa namna gani sheria husika ni kandamizi.
Hansard inaeleza vizuri dhima ya Bill of rights Katika Tume ya Jaji Nyalali.
Tume ya Jaji Nyalali iliundwa na Rais Mwinyi baada ya migongano kati ya Sheria na Bill of Rights ambayo ililetwa na mabadiliko ya Katiba ya 1984.
Dhima kuu ilikuwa kuzifanya sheria za zamani zishabihiane na Bill of Rights pale ambapo panaleta mkinzano.
Unachobisha wewe ni kitu gani hapo?