Ofisi ya Waendesha Mashtaka kugeuka kuwa ofisi ya wafuta mashtaka kunatia doa mfumo wa haki nchini

Nimeshangaa sana kuona mtu anaandika sheria kandamizi 40 alizozitaja Jaji Nyalali zimefutwa na Bill of Rights
Unachokataa ni nini hapo? Kwani hazikufutwa?

Mwaka 1992, Tume ya Jaji Francis Nyalali ilikabidhi mapendekezo ya kuzitengua hizo sheria kwa Law Reform Commision, kisha Mwanasheria mkuu wa Serikali wa wakati huo akazipeleka Bungeni kwa ajili ya marekebisho kupitia WRITTEN LAWS MISCELLANEOUS (AMENDMENT BILL) 1994.

Nyingi zilifutwa na zingine zikarekebishwa.

Yote yameelezwa vyema kwenye HANSARD REPORT ya 29 November 1995. Page 732-734.

Haya yote yalifanyika baada ya kuja kwa Bill of Rights.

Bill of rights ndiyo iliyokuwa MIZANIA KUU ya KUPIMA ni kwa namna gani sheria husika ni kandamizi.

Hansard inaeleza vizuri dhima ya Bill of rights Katika Tume ya Jaji Nyalali.

Tume ya Jaji Nyalali iliundwa na Rais Mwinyi baada ya migongano kati ya Sheria na Bill of Rights ambayo ililetwa na mabadiliko ya Katiba ya 1984.

Dhima kuu ilikuwa kuzifanya sheria za zamani zishabihiane na Bill of Rights pale ambapo panaleta mkinzano.

Unachobisha wewe ni kitu gani hapo?
 
Moja ya kazi za DPP Ni kufuta mashtaka pale inabobainika kesi haina mashiko.
 
Kwanza kabisa ulisema zilirekebishwa katika Bill of Rights.

Bill of Rights ya mwaka gani? Tume ya Nyalali ripoti yake ilitoka mwaka gani?

Pili, sheria za Preventive Detention zikizolalamikiwa na Jaji Nyalali zimefutwa? Lini?

Tuanzie hapo.
 
Binafsi napingana na wewe,tungekuwa tunaweza kusimamia haki kwa mujibu wa Sheria na taratibu,Bila kubambikia watu kesi,Bila kuonea Bila kudhulumu,Bila kufanya maamuzi kwa kuzingatia ukanda na ukabila ningeunga mkono malalamiko yako,ila kwa njia tuliyokuwa tumeichagua tunapoteza uhalali hata wa kulalamikia yanayotokea leo.
Huna akili we mpuuzi na pimbi. Hoja hapa ni Ofisi ya mashitaka kukusanya ushahidi kisha kufungua kesi. Sio kufungua kesi na kukaa na watuhumiwa magerezani kisha kufuta kesi.
 
Pimbi ni mnyama kama binadamu yupo kundi hilo nawewe jikague,ya weza kuwa ndie mwenyewe hasaa halafu hujapata kujitambu,ila kimsingi kumbuka enzi za dhulma ,uonevu na ubabe,zimepita,Mama ana wanyoosha wote wa aina yako na wengine mfananao.
 
Bomu gani linalotegwa,binafsi Naina anategua mabomu yaliyotegwa ambayo yangeenda kuliangamiza taifa,kiuchumi na kijamii kwa kuendekeza ukanda ,ukabila na ubaguzi wa kiitikadi.
Ila kweli!
We fikiria unamuweka ndani Singasinga mtu aliyekuwa anaisaidia TANESCO kwa kumlipa tusenti tuchache tu!
 
Kwanza kabisa ulisema zilirekebishwa katika Bill of Rights..
Nimekwambia sheria hizo zilifutwa baada ya kuja kwa Bill of Rights, sio zilifutwa/kurekebishwa na/katika Bill of Rights.

Sijui ulinielewa?
 
Binafsi napingana na wewe,tungekuwa tunaweza kusimamia haki kwa mujibu wa Sheria na taratibu,Bila kubambikia watu kesi,Bila kuonea Bila kudhulumu,Bila kufanya maamuzi kwa kuzingatia ukanda na ukabila ningeunga mkono malalamiko yako,ila kwa njia tuliyokuwa tumeichagua tunapoteza uhalali hata wa kulalamikia yanayotokea leo.
Safi kabisa
 
Wewe utakuwa siyo mzima, unafurahia watu walivyokuwa wanateswa magerezani bila sababu za msingi? mpuuzi kabisa
 
Laana inayolitesa bara la afrika chanzo chake ni uonevu uliopo katika mifumo ya utoaji haki.

Kesi 147 za takukuru za uonevu zinapofutwa inabidi tuangalie kwa kina na kujadili ni wangapi wameteseka ambao maisha yao yanawategemea wote waliobambikiwa kesi.
Kabisa
 
Nimekwambia sheria hizo zilifutwa baada ya kuja kwa Bill of Rights, sio zilifutwa/kurekebishwa na/katika Bill of Rights.

Sijui ulinielewa?
Your timeline does not make sense.

Kwa sababu Bill of Rights ilikuwepo kabla ya Tume ya Jaji Nyalali.

Sheria hizo hazikurekebishwa kabla ya Tume ya Nyalali. Ndiyo maana Jaji Nyalali akazipigia kelele.

Sasa Bill of Rights 1984, Tume ya Nyalali 1990s imelalamikia sheria hizo hizo. Hata kama zimefutwa baada ya Tume ya Nyalali kusema zimefutwa baada ya Bill of Rights ni smokescreen tu hapo.

Ni kama umezaliwa 1980, unaulizwa umezaliwa lini, badala ya kusema umezaliwa 1980, unasema umezaliwa baada ya Yesu.No specificity of events in your timeline!

Zaidi, hujasema sheria ya preventive detention imefutwa lini.

Kikubwa kuliko yote, mpaka sasa bado unapingana na due process na constitutional rights kama presumption of innocence. Naona haya umeyaruka hutaki kuyarudia kuonesha ugubegube wako unaotaka kutupeleka Kampuchea ya Pol Pot.
 
Your timeline does not make sense.

Kwa sababu Bill of Rights ilikuwepo kabla ya Tume ya Jaji Nyalali.

Sheria hizo hazikurekebishwa kabla ya Tume ya Nyalali. Ndiyo maana Jaji Nyalali akazipigia kelele.
Sijui unaelewa unachoandika lakini?

Sheria zingerekebishwa vipi kabla ya Bill of Rights wakati Bill of Rights ndicho kilikuwa KIGEZO na KIPIMO cha msingi cha kurekebisha sheria?

Bila Bill of Rights wasingeweza kurekebisha hizo sheria kwa sababu sheria zenyewe kama zenyewe ambazo zinadaiwa kuwa "kandamizi" zilipaswa kupimwa katika uzani wa HAKI ZA BINADAMU ambazo zimeelezwa katika Bill of Rights ili kujua kama kweli ni kandamizi na zinakiuka haki za msingi.

Unawezaje kusema haki za watu zimevunjwa pasipo uwepo wa haki hizo?

Tutajuaje kama haki ni haki kweli bila benchmark fulani ya kutizamia?

Sijui unaelewa?

What kind of timeline do you want?

Bill of Rights imekuja 1984, Tume ya Nyalali ikaja 1991, miaka sita baadaye.

Ilikuwa ni mchakato. Sio swala la kukurupuka tu na kubadilisha sheria kesho yake.

Well, inaweza ikawa ni muda mrefu, but what is the point?

Pointi ya msingi hapa ni kwamba, mabadiliko ya sheria kupitia Tume ya Nyalali YALICHAGIZWA na ujio wa Bill of Rights!
 
Kikubwa kuliko yote, mpaka sasa bado unapingana na due process na constitutional rights kama presumption of innocence. Naona haya umeyaruka hutaki kuyarudia kuonesha ugubegube wako unaotaka kutupeleka Kampuchea ya Pol Pot.
Hakuna sehemu nimepingana na due process za Constitutional rights!

Tatizo ni kwamba wanaharakati wanatumia Kichaka cha haki za binadamu kupalilia uhalifu.

Magaidi yamekamatwa yametiwa ndani, wanaharakati hawaishi kuyoyoma.

Kumbe ilitakiwa iweje? Magaidi waachiwe huru wakalipue makanisa?

Mlitaka magaidi wafanyiwe nini hasa?

Nilishakueleza kuhusu maswala ya upelelezi. Hiyo ni taaluma.

Huwezi kufix time-limit ya upelelezi kwenye sheria. Mambo yatafeli.

Kuna makesi yanachukua hata miaka minne huko, waiting for correspondences from foreign jurisdiction! — Nyaraka zitumwe, zijibiwe, zijibiwe tena na tena, uandae viapo vya wakemia sijui manini!

Ukiwaambia wapeleleze kwa miezi minne, unatarajia nini?

Muda uliopangwa kufanya upelelezi ukiisha, magaidi waachiwe wakachafue nchi?
 
Sijui unaelewa unachoandika lakini?

Sheria zingerekebishwa vipi kabla ya Bill of Rights wakati Bill of Rights ndicho kilikuwa KIGEZO na KIPIMO cha msingi cha kurekebisha sheria?

Bila Bill of Rights wasingeweza kurekebisha hizo sheria kwa sababu sheria zenyewe kama zenyewe ambazo zinadaiwa kuwa "kandamizi" zilipaswa kupimwa katika uzani wa HAKI ZA BINADAMU ambazo zimeelezwa katika Bill of Rights ili kujua kama kweli ni kandamizi na zinakiuka haki za msingi.

Unawezaje kusema haki za watu zimevunjwa pasipo uwepo wa haki hizo?

Tutajuaje kama haki ni haki kweli bila benchmark fulani ya kutizamia?

Sijui unaelewa?

What kind of timeline do you want?

Bill of Rights imekuja 1984, Tume ya Nyalali ikaja 1991, miaka sita baadaye.

Ilikuwa ni mchakato. Sio swala la kukurupuka tu na kubadilisha sheria kesho yake.

Well, inaweza ikawa ni muda mrefu, but what is the point?

Pointi ya msingi hapa ni kwamba, mabadiliko ya sheria kupitia Tume ya Nyalali YALICHAGIZWA na ujio wa Bill of Rights!
Hapo unakuwa argumentative.

Nakuuliza wewe baba yako nani? Unanijibu kwamba ukoo wenu ulitokea Afrika Kusini kwenye majeshi ya Shaka Zulu!

Naona umeruka kabisa kuongelea presumption of innocence ambayo ilikuwepo kabla ya Bill of Rights.

Ume suspend constitutional rights kwa kuwaita magaidi watu ambao hawajahukumiwa na mahakama kuwa magaidi. Serikali imeona hapa hamna kesi, imeamua kuwaachia, wewe bado unawaita magaidi.

Pia, mpaka sasa hujasema sheria ya preventive detention imefutwa lini.
 
Ume suspend constitutional rights kwa kuwaita magaidi watu ambao hawajahukumiwa na mahakama kuwa magaidi. Serikali imeona hapa hamna kesi, imeamua kuwaachia, wewe bado unawaita magaidi.
Hizo ni siasa tu.

Serikali imeamua kuwaachilia magaidi kwa hiyari yake. Siwezi kujadili siasa za aina hiyo.

Dhima ya "presumption of innocence" ni kwa ajili ya kuwalinda watuhumiwa wasionewe ama wasitwezwe utu wao wanapokuwa mikononi mwa vyombo vya dola.

Sio kwa ajili ya ku-limit maoni ya watu.

Huwezi kunizuia nisiwaite Magaidi. Umekosea muktadha.

I believe they are terrorists, and i am entitled to that opinion.
 
Hakuna sehemu nimepingana na due process za Constitutional rights!

Tatizo ni kwamba wanaharakati wanatumia Kichaka cha haki za binadamu kupalilia uhalifu.

Magaidi yamekamatwa yametiwa ndani, wanaharakati hawaishi kuyoyoma.

Kumbe ilitakiwa iweje? Magaidi waachiwe huru wakalipue makanisa?

Mlitaka magaidi wafanyiwe nini hasa?

Nilishakueleza kuhusu maswala ya upelelezi. Hiyo ni taaluma.

Huwezi kufix time-limit ya upelelezi kwenye sheria. Mambo yatafeli.

Kuna makesi yanachukua hata miaka minne huko, waiting for correspondences from foreign jurisdiction! — Nyaraka zitumwe, zijibiwe, zijibiwe tena na tena, uandae viapo vya wakemia sijui manini!

Ukiwaambia wapeleleze kwa miezi minne, unatarajia nini?

Muda uliopangwa kufanya upelelezi ukiisha, magaidi waachiwe wakachafue nchi?
Hakuna sehemu umepingana na due process za constitutional rights?

Hukuongekea habari za reality on the ground ku trump due process hapa?

Unaelewa kwamba kuwaita watu magaidi, watu ambao mahakama imeshindwa kuwakuta na hatia ya ugaidi, mahakama imewafutia kesi ma kuwachia huru, ni kuvunja haki zao za kikatiba za presumption of innocence?
 
Hizo ni siasa tu.

Serikali imeamua kuwaachilia magaidi kwa hiyari yake. Siwezi kujadili siasa za aina hiyo.

Dhima ya "presumption of innocence" ni kwa ajili ya kuwalinda watuhumiwa wasionewe ama wasitwezwe utu wao wanapokuwa mikononi mwa vyombo vya dola.

Sio kwa ajili ya ku-limit maoni ya watu.

Huwezi kunizuia nisiwaite Magaidi. Umekosea muktadha.

I believe they are terrorists, and i am entitled to that opinion.
You are entitled to your own opinion, but not your own fact.

Fact, mahakama haijawakuta watu na hatia ya ugaidi, ukiwaita magaidi umewavunjia haki yao ya kikatiba ya presumption of innocence.
 
Unaelewa kwamba kuwaita watu magaidi, watu ambao mahakama imeshindwa kuwakuta na hatia ya ugaidi, mahakama imewafutia kesi ma kuwachia huru, ni kuvunja haki zao za kikatiba za presumption of innocence?
Kwanza mahakama haikuwafutia kesi.

DPP ndiye aliyewafutia kesi, kisha mahakama "ikapokwa" mamlaka yake ya kushugulikia jinai kwa minajili hiyo.

Their release was not based on the merits of the court findings.

Kwahiyo hao magaidi waliachiliwa huru si kwa sababu hawakuwa na hatia, isipokuwa kwa sababu DPP aliamua kuwaachilia huru kwa sababu zozote zile anazozijua mwenyewe na ofisi yake.

When you are PRESUMED to be innocent, it does not necessarily mean you are innocent.

You are simply given a benefit of doubt to avoid any possible abuse of power by the police and other organs of the state.

KUDHANIWA kwamba hauna hatia, hakukufanyi usiwe na hatia. Tuelewana hilo kwanza.

Inawezekana hao magaidi wana hatia ama hawana hatia.

They are simply PRESUMED innocent!

Kuwatetea na kushabikia kwamba HAWANA HATIA ni kutoelewa muktadha wa hiyo dhana nzima.
 
Back
Top Bottom