Oktoba 2026: Tibeli women, mwanamke mjenzi. Nitasimama

Oktoba 2026: Tibeli women, mwanamke mjenzi. Nitasimama

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
OKTOBA 2026: TIBELI WOMEN, MWANAMKE MJENZI.
NITASIMAMA.

Kwa wale Wanawake na Mabinti za Tibeli, na Wanaume wenye mabinti, Wake na wanaopenda Wanawake zao.

Mimi Mtibeli, Baba yenu. Nimeutenga mwezi huu mzima. Utakuwa Mwezi wa wanawake wa Tibeli, MWANAMKE MJENZI, kauli mbiu yetu itakuwa NITASIMAMA.

Oktoba hii tunaanza safari mpya.
Safari ya mwanamke anayekataa kubaki mtazamaji wa maisha yake. Mwanamke anayekataa kuwa mzigo na tegemezi.

Mwanamke anayetaka maarifa. Anayetafuta ujuzi na uwezo.
Anayejenga kipato kwaajili yake, familia na Taifa lake.
Anayejifunza kusimamia fedha. Kuitumia fedha kama silaha na ulinzi.
Na anayetamani kuwa na maisha anayoyasimamia kwa hekima na heshima.

Huyu ndiye Mwanamke Mjenzi. Mwanamke wa Tibeli.

Kwa mwezi mzima wa Oktoba, Tibeli Women tutazungumza kuhusu mwanamke, uchumi, kazi, biashara, fedha, mali, familia, nidhamu na kujijenga.

Hatutazungumza tu.
Tutajifunza. Tutapanga. Tutafanya kisha Tutajenga na malkia wa Tibeli.

Na safari hii itaanza kesho.
3 OKTOBA 2026

Kama wewe ni mwanamke unayetaka kujijenga zaidi kiuchumi na kimaisha, hii ni safari yako. Unaweza kumualika na kumtag mwanamke au binti unayempenda akae karibu na kampeni hii.

Andaa kabisa kitabu, notes na kalamu. Mwezi huu utakuwa wenu wanawake. Utajifunza, utauliza, utashare hisia zako, utapata wa kumwambia mambo yako, hisia zako, wanawake wa Tibeli wapo kibao wenye uwezo, nguvu, akili, na upendo.

MWANAMKE MJENZI.

NITASIMAMA.

#TibeliWomen #MwanamkeMjenzi #Nitasimama #Tibeli #WomenEmpowerment #WomenAndWealth #mwanamkenauchumi
 
Tuelewane hapa;

1. NITASIMAMA haimaanishi; sitawahi kuanguka.

2. NITASIMAMA haimaanishi sitahitaji msaada.

3. NITASIMAMA haimaanishi sitakosea.
Hapa wengi ndio hukwama. Ndio maana hawakubali ukweli, kuambiwa makosa yao, hawataki kuwajibika na hiyo huwafanya washindwe kusimama kwa sababu hawataki kulaumiwa kwa kukosea kwao. Na hiyo huhalalisha makosa yao.


MAANA YAKE NI:
Nikianguka, nitajifunza.
Nikikosea, nitajirekebisha.
Nikikosa mtaji, nitaanza na nilichonacho.
Nikikosa maarifa, nitajifunza.
Nikichelewa, sitakata tamaa. Nitaendelea.

NITASIMAMA!

Tutaenda hatua kw hatua.
 
Kesho itakuwa siku ya ufunguzi.

Swali kuu litakuwa ni hili, ambalo nalitoa hapa kama homework yako. Kama unamajibu utanipa hapa hapa.

Swali lenyewe ni hili;
Ni nani unayemsubiri aje kubadilisha maisha yako?

Swali hilo ndio swali la ufunguzi.
NITASIMAMA
 
Back
Top Bottom