Oktoba 28 ni mashindano kati ya Reality vs Ahadi Hewa? Je, Watanzania watachagua nini kati ya visible, tangible Deliverables vs The Empty Promises?

Huwezi kuwa mchambuzi huru wakati ukiwa na upande katika sehemu au pande unazochambua. Kuna upande wa Vissible tangible deliverable( CCM) na Promises(Upinzani).Umedeclare interest wewe ni kada wa CCM sijui km uchamabuzi wako haupo biased. Hapo ndo tatizo, Kazi za kiuchambuzi, political analysis tuwaachie ambao Ni non alligned. Sio Kada wa chadema au CCM aje hapa afanye analysis ya kisiasa halafu tutegemee kupata hoja za msingi zisizoegemea upande wake.

Nilikuwa nafuatilia kongamano ambalo liliandaliwa Jana Na TBC lililohusu vijana lililokuwa na mada isemayo "Matarajio ya vijana na uongozi wa baade" km sijakosea mada, lakn maudhui nzima ilikuwa hivyo, mgeni rasmi alikuwa Spika Mstaafu wa Bunge la JMT Mama Anna Makinda. Wakati anatoa hotuba yake kuhusu mada hiyo alisema tatizo linalotukumba vijana Ni inconsistence yaani hujui unataka kuwa Nani na hoby yako Ni Nini hasa katika kulijenga taifa lako. Akaeleza namna yeye alivyoingia kwenye siasa na Baadae kuwa Spika na Hadi amestaafu Kazi ya siasa akiwa bungeni. Alisema yy professional Ni Auditor lkn alipiachana na professional yake na kuingia kwenye siasa hakuwa na ndoto zingine.

Alimaanisha Nini? Km kijana inatakiwa kuwa consistence na Nini unataka kufanya. Km unaamua kuwa mwandishi Basi lisaadie Taifa kwa taaluma yako ya uandishi, na km wewe Ni mwalimu halikadhalika fanya hivyo na sio huku unafanya kidogo na huku kidogo, Baadae unakuja kuchanganya mambo na kuharibu kabisa

Kwahyo Kaka Pascal Mayalla lisaidie Taifa Hili kwa Taaluma yako ya uandishi wa habari na sio huku mwandishi wa habari na huku ni kada wa Chama Fulani. Heshima yako ya kitaaluma unashuka Sana
 
Makini sana
 
Masimango si kitu kizuri. Mtu akikuambia nimekununulia hiki au nimekupa kile ili na wewe umpe kile hayo ni masimango. Mwache apime na aamue mwenyewe. Watanzania tuachwe tuamue wenyewe kwa sababu yeyote angeweza kufanya jambo kwa sababu anatumia kodi zetu. Kwa nini sasa asingefanya kitu?
Sasa kama alitumia hela zetu kufa kitu si sawa tu? maana pia tutaendelea kulipa kodi na yeyote ajaye hataitumbukiza chooni. Masimango tuache!

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kuna makosa mengi hayo ni makadirio.
Hiyo sensa nayo haijafanyika sawa sawa sababu ya maandalizi hovyo.
Kama ingefanyika kama ya Yoseph na Maria walioenda kuhesabiwa kwa amri ya Kaisari nadhani asili mia 95 wangehesabika.
Na ujinga huu umeendekezwa kwa kutegemea misaada ya wafadhili kwa vitu vya msingi.
Pia kuna mkono wa kisiasa na World Bank.Sharti mmoja ilikuwa kuzingatia uzazi wa mpango.
Kwa kuwa halikufanyika sawa sawa utakuta idadi ya kweli ambayo naamini ni kubwa ingeenda kinyume na masharti ya Taasisi hizo Kifedha na kuzua balaa jingine kwa kupewa mikopo au misaada.
 
hakika mh alimanisha aliposema mayala maana yake njaa
 
Yaani kwa bandiko hili pascal nimekupuuza kabisaaaa....yani wee andazi kabisa
 

Kama ww huna Data kamili, acha wenye nazo waziweke. Ila hata kama kungekuwa na data kamili hakuna uwezekano wa wapiga kura kufika 29m+. Hivyo tume ya uchaguzi ina majibu anayotaka Magufuli tayari.
 
Na huu ndio ujinga unaoenezwa,lakini miak 5 ijayo wataelewa.
 

Ukishakuwa verified user akili yako inakuwa matope, takataka and the like. Huwezi kuandika ukweli wako ulio moyoni! Kwahiyo wewe ni wa kupuuza. Moreover umechanganyikana kuwa influenced na ukabila katika kufikiri kwako, huwezi kuwa rational, hivyo wewe ni wa kupuuza!
 
Kumbe mtu anaweza akawa mtu mzima kama Paskali Mayala na bado akawa mpuuzi.

PS
 
Paskali amesahau kuwa 2015 Magufuli hakuwa na tangibles za kuonesha bali alibebwa na promises. Watanzania siyo wajinga kiasi kwamba washindwe kutathmini na kubaini credible promises and un-promised tangibles. Swali: Is what Magufuli promised (2015) consistent with the deliverables during his leadership tenure?
Where are our freedoms? Our crops returns? Our private sector operatives? Our civil society sector operatives? Our constitutional supremacy? list ni ndefu!@Pascal Mayalla
 
Bado safari ni ndefu kidogo kuhusu umuhimu wa mbunge na serekali. Nani anamajukumu gani katika harakati za maendeleo. Kunamambo ambayo Watanzania wengi hatuyaangalii kwa makini kama jukumu la mbunge, wengi tunaishia kuangalia vitu kama ndio kipimo cha mbunge. Lazma watu wajue mradi fulani ukifanyika kwenye mkoa au wilaya fulani ambalo ndio jukumu la serekali lazima mbunge na diwani atapatia hapo Kiki lakini kiukwel hilo lilikua jukumu la serekali. Wapimeni wabunge kwa kuweza kuisimamia serekali hususani kwenye kupitisha sheria za kustawisha nchi yetu. Sioni sababu ya kujisifu mbunge kapata Kiki kupitia barabara iliyojengwa na serekali wakati huohuo kapitisha sheria ya zarura ya madini au gesi ambayo ni km imempa Mali yetu bure kwa mwekezaji. Sioni sababu ya kumsifu mbunge ambaye anaishia kusifu kujengwa zahanati ambayo ni jukumu la serekali wakati huohuo C.A.G katoa ripot ya upotevu mkubwa wa pesa katika mashirika ya uma lakini Hana uwezo wa kuhoji na kuwawajibisha wahusika na kuishia kupiga maneno mengi alafu ishu inaishia hewani. Yapo Mambo ya msingi ambayo mbunge anayotakiwa kufanya wakishirikiana na wabunge wengine kwa pamoja ambayo wengi hatuyaoni ni ya muhimu japo yana madhara makubwa sana kiuchumi indirect. Tunaishia kutaja vitu, hvyo ni vya serekali ndio mkusanya Kodi. Pia mbunge anaweza kuikontrol serekali katika ugawaji sawa wa huduma katika nchi.
 
idiot;
tribal;
citizen.
 
Wajumbe ni akina nani ?

#Naomba definition yako
#ndugu mwandishi una nn chakuwaambia wajumbe?
 
[QUOTE="G Sam, post: 36454636, .

Halafu pia ulinikera ulivyoandika eti "Wapo watu wenye nia ya kugombea ubunge kwa dhati ya kusmaidia Magufuli"
Naomba nikueleze kuwa kazi ya bunge siyo kumsaidia Magufuli, kazi ya bunge ni kusimamia na kuiongoza serikali. Kuza akili yako mzee, uccm usikulemaze kiasi hicho!
[/QUOTE]
Japo umeteleza uliposema kuiongoza serikali lakini mengine umefanya vyema Ni kweli Huyu kadhalilisha nafasi
 
Matokeo ya kupata kura moja yanaanza mdogomdogo
 
Kwanza chadema nzima inawatukana wasukuma kwamba ni washamba,
Juzi Lisu kasema ule uwanja wa chato Magufuli kajenga kwa ajili yake na mamaake!
.
Watu wa kanda ya ziwa wanawachora tu, wamejikalia kimya majibu yao watayatoa oktoba.
Hoja vichekesho zinaongezeka kwa kasi sana siku hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…