Ole Sabaya afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na kufunguliwa kesi mpya. Amkataa Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU

Ole Sabaya afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na kufunguliwa kesi mpya. Amkataa Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, amemkataa Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Tumaniel Kweka kwa kuwa anatokea wilaya ya Hai.

Amewasilisha hoja hiyo leo Jumatano June Mosi, 2022 mbele ya Hakimu Mkazi, Salome Mshasha, Sabaya amesema hana imani na mwendesha mashitaka huyo kwa kuwa anatokea katika wilaya hiyo na kwamba ni mtu aliyedai ni wa visasi na anatumika kisiasa.

Sabaya na washtakiwa wenzake wanne wanaokabiliwa na mashitaka saba.

Sabaya amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati kesi hiyo.

Mbali na hoja hiyo lakini kulijitokeza hoja nyingine kupitia kwa wakili Hellen Mahuna, aliyedai washitakiwa hao hawakupelekwa mahakamani hapo kwa kufuata taratibu za kisheria na kwamba mawakili wao hawakupewa taarifa.

Kutokana na malumbano hayo, Hakimu Mshasha ameahirisha kesi hiyo kwa muda wa dakika 10 hadi 15 ili kupitia hoja hizo ili kutoa uamuzi mdogo.
 
Yeye ajipange kupangua mashtaka, hawezi kuichagulia serikali wakili wa kuiwakilisha,kama ambavyo serikali haiwezi kumchagulia wakili.

It is not over till it's over.

The saga continues
 

Sabaya afikishwa mahakamani Moshi kufunguliwa kesi mpya​

WEDNESDAY JUNE 01 2022​



sabaya pic 2

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kufunguliwa kesi mpya.

Summary

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kufunguliwa kesi mpya.
ADVERTISEMENT

janet josephpic

By Janeth Joseph
More by this Author

Moshi. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kufunguliwa kesi mpya.

sabaya pic1

Sabaya amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Juni Mosi saa 11:40 asubuhi.
 
Back
Top Bottom