Ole Sabaya amkana mshirika wake katika kesi

Ole Sabaya amkana mshirika wake katika kesi

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Arusha .

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro Lengai o Sabaya amemkana mshirika wake katika kesi hiyo ya unyang'anyi wa matumizi, Sylvester Nyegu, kuwa hakuwa msaidizi wake.

Sabaya na wawili wawili, Nyegu ambaye anadaiwa na upande wa mashtaka kuwa msaidizi wake binafsi na Daniel Mbura aliweza kuona kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo.

Katika kesi hiyo ambayo iko katika hatua ya utetezi, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya unyang'anyi wa kutumia silaha katika duka la Mohamed Saad eneo la bondeni jijini Arusha.

Akihojiwa na mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Baraka Mgaya leo Jumatano Agosti 18, 2021 kuhusu uhusiano wake na mshtakiwa huyo wa pili, Sabaya ameeleza mahakama hiyo kwa kuwa anajua Nyegu lakini hakuwa msaidizi wake binafsi.

Amedai kuwa alipangiwa kufanya naye kazi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai.

Lakini alipoulizwa kuwa Nyegu alipangiwa na mkurugenzi kufanya naye kazi kama nani, Sabaya amedai kuwa hafahamu kuwa alipangiwa kama nani huku akimrushia mpira Nyegu mwenyewe kuwa ndiye anayeweza kueleza.

Sabaya ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ya upande wa utetezi, alikuwa akihojiwa na upande wa mashtaka baada ya kumaliza kukamilisha kutoa utetezi wake ambapo hata hivyo amekwepa kujibu maswali mengi akidai kuwa hawezi kuelezea kwa kuwa siri

[emoji2398] Mwananchi
 
Movie ilisha isha amna wa kufungwa apa zimebaki porojo tu
 
Huyu akicheza anafungwa. Haiwezekani mahakamani useme ni siri halafu eti unasema mtu alipangiwa kwako na ofisi ya Mkurugenzi lakini haujui majukumu yake ni yapi. Lengai Lengai umeanza kuchanganyikiwa.
Amechanganyikiwa hasa ukizingatia hana pesa sasa hv akiba yote mawakili wameilamba plus kunaribu kuhonga..
 

kesi sabayapic


Arusha. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro Lengai ole Sabaya amemkana mshirika wake katika kesi hiyo ya unyang’anyi wa kutumia silaha
Sylvester Nyegu, kuwa hakuwa msaidizi wake.
Sabaya na wenzake wawili, Nyegu ambaye anadaiwa na upande wa mashtaka kuwa alikuwa msaidizi wake binafsi na Daniel Mbura wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha,

Amedai kuwa alipangiwa kufanya naye kazi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai.
Lakini alipoulizwa kuwa Nyegu alipangiwa na mkurugenzi kufanya naye kazi kama nani, Sabaya amedai kuwa hafahamu kuwa alipangiwa kama nani huku akimrushia mpira Nyegu mwenyewe kuwa ndiye anaweza kueleza.




Sehemu ya mahojiano baina yake Sabaya na waendesha mashtaka ilikuwa kama ifuatavyo:

Wakili Mgaya: Shahidi, Julai 16 mwaka huu wakati mnasomewa maelezo ya awali, Nyegu alikubali kuwa alikuwa msaidizi wako binafsi, ni sahihi au si sahihi.
Sabaya: Sina msaidizi binafsi, swali hilo aulizwe Nyegu mwenyewe
Wakili: Ulieleza kuwa uliishi kama mkimbizi kwa wiki mbili ukiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, nani walikutishia na waliwahi kufikishwa mahakamani kwa kukutishia kukuua?
Sabaya: Wapo, siwezi kuwataja,vyombo vya dola walifanyia kazi.


Katika hatua nyingine wakati akihojiwa na mwendesha mashtaka Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka, Sabaya ameieleza mahakama kuwa hakuwa anamfahamu jina kiongozi wake wa kazi, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, marehemu Ana Mughwira, siku aliyomuapisha kuwa mkuu wa wilaya hiyo.

Sabaya amesema kuwa aliapishwa Agosti Mosi, 2018 kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro na kwamba kabla ya hapo hakuwa anamjua Mkuu wa Mkoa kwa jina.
Lakini alipoulizwa majukumu yake mara nyingi Sabaya hakuwa tayari kueleza majukumu mengine ambayo katika utetezi wake alieleza kuwa yalikuwa ni maalumu aliyopewa na mamlaka ya uteuzi wake na mengine akidai kuwa ni siri hadi alipoonyeshwa sheria ambayo imeanisha majukumu ya Mkuu wa Wilaya.


Sehemu ya mahojiano baina ya Sabaya na Wakili Kweka ilikuwa hivi.
Wakili Kweka. Ulianza lini kuwa mtumishi umma.
Sabaya. Siwezi kueleza Mahakama
Wakili: Ulisema kuwa unakumbuka 9/2/2021 ukiwa unaendelea na kikao ulieleza ulipokea simu kutoka Mamlaka ya uteuzi wako na ukapokee wageni uwanja wa ndege, ni sahihi? .
Sabaya: Ndio nilieleza.
Wakili: Je ulienda kuongoza timu kama nani?
Sabaya: Siwezi kueleza
Wakili: Lengai ole Sabaya umesema miongoni mwa majukumu yako ni pamoja na kuongoza Kamati ya Ulinzi na usalama, ni kweli?
Sabaya: Ni kweli.
Wakili : Je, utakubaliana na mimi kuwa cheo hicho kimeundwa kisheria na majukumu yake yapo kisheria?.
Sabaya: Ni sahihi.
Wakili: Kwa sheria iliyotungwa na Bunge?.
Sabaya: Kwa mujibu wa sheria.
Wakili: Sabaya utakubaliana na mimi kuwa muundo wa kazi na majukumu sio siri, yameundwa kisheria kwa hiyo sio siri?.
Sabaya: Siri.
Wakili: Kwa hiyo kazi za Kamati zimeanishwa na sheria kwa hiyo sio siri, ni sawa?
Sabaya: Siri.
Wakili: Soma hii Sheria namba 8 ya mwaka 2010 The National Security Council Act, number 2010, section 11.
Sabaya: Anasoma kifungu hicho cha sheria hiyo
Wakili: Kwa hiyo majukumu ya Kamati ya Ulinzi na usalama yanajulikana na kila mtu akitaka anaweza kuisoma
Sabaya: Ndio zimeainishwa
 
Back
Top Bottom