Ole Sabaya amkana mshirika wake katika kesi

Ole Sabaya amkana mshirika wake katika kesi

Wewe labda hujui namna ya kutoa usjahidi yupo very composed na ushahidi wake kashauset na anauhakika wa anachokifanya kipo relevant katika ku disprove allegations against him
Hakuna kitu hapooo, DED hana mamlaka ya kupeleka mtumishi ofisi ya DC
 
Huyu akicheza anafungwa. Haiwezekani mahakamani useme ni siri halafu eti unasema mtu alipangiwa kwako na ofisi ya Mkurugenzi lakini haujui majukumu yake ni yapi. Lengai Lengai umeanza kuchanganyikiwa.
Kaulizwa kwa nini ulipokuwa unaenda huko Arusha ulikuwa humjulishi bosi wako (RC Kilimanjaro)? Eti anajibu iulizwe mamlaka ya uteuzi [emoji1787][emoji1787]
 
Kaulizwa kwa nini ulipokuwa unaenda huko Arusha ulikuwa humjulishi bosi wako (RC Kilimanjaro)? Eti anajibu iulizwe mamlaka ya uteuzi [emoji1787][emoji1787]
Kuchanganyikiwa huyu dogo
 
Arusha .

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro Lengai o Sabaya amemkana mshirika wake katika kesi hiyo ya unyang'anyi wa matumizi, Sylvester Nyegu, kuwa hakuwa msaidizi wake.

Sabaya na wawili wawili, Nyegu ambaye anadaiwa na upande wa mashtaka kuwa msaidizi wake binafsi na Daniel Mbura aliweza kuona kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo.

Katika kesi hiyo ambayo iko katika hatua ya utetezi, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya unyang'anyi wa kutumia silaha katika duka la Mohamed Saad eneo la bondeni jijini Arusha.

Akihojiwa na mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Baraka Mgaya leo Jumatano Agosti 18, 2021 kuhusu uhusiano wake na mshtakiwa huyo wa pili, Sabaya ameeleza mahakama hiyo kwa kuwa anajua Nyegu lakini hakuwa msaidizi wake binafsi.

Amedai kuwa alipangiwa kufanya naye kazi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai.

Lakini alipoulizwa kuwa Nyegu alipangiwa na mkurugenzi kufanya naye kazi kama nani, Sabaya amedai kuwa hafahamu kuwa alipangiwa kama nani huku akimrushia mpira Nyegu mwenyewe kuwa ndiye anayeweza kueleza.

Sabaya ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ya upande wa utetezi, alikuwa akihojiwa na upande wa mashtaka baada ya kumaliza kukamilisha kutoa utetezi wake ambapo hata hivyo amekwepa kujibu maswali mengi akidai kuwa hawezi kuelezea kwa kuwa siri

[emoji2398] Mwananchi
Kapoteza kumbukumbu
 
Back
Top Bottom